Ndugu zangu,
Haya ni maoni yangu binafsi nisije nikaanza kuviziwa kutolewa roho na wale wasiopenda kukosolewa.
Nimefuatilia kwa umakini mkubwa kilichotokea Congo kwenye uchaguzi na uhusika wa kanisa katoliki ktk kupigania haki za wananchi.
Kwa leo sitapenda kuzungumzia umuhimu wa dini kwenye jamii ila ninalipongeza kanisa kwa kufuata misingi ya ki MUNGU kutatua migogoro,ni vema na kanisa katoliki tanzania kuiga na kufuata njia hizo,achana na hivi vikanisa uchwara vinavyowalamba miguu wauaji na kuwasifia hadharani.
Pia kinachoendelea zimbwabwe mpaka muda huu naandika kinasikitisha,bw.Mugabe ameshaiharibu nchi ile na wananchi wanateseka na uchumi wakati yeye kwa sasa amekaa kwa raha anakunywa juice ya baridi bila shida akiwacheka wananchi wake.
Ifike mahali chama cha mapinduzi kijifunze kutokana na matukio ya vyama vilivyoharibu nchi zao kwa kuwakumbatia viongozi wanaoharibu badala ya kujenga.
Ni vema kukawepo na mbadala pale ambapo kiongozi aliyeko madarakani anapoharibu basi asiruhusiwe kiendelea kuharibu na badala yake awepo mbadala na hatimae nchi isonge mbele,
2020 ili kuokoa taifa letu la tanzania na mateso ya wananchi ya kiuchumi,kutekwa,kuuawa,kupotezwa na hata kuweka mahusiano kwa vyama vya upinzani na hatimaye kujenga nchi moja isiyo na upendelea wa kikabila au kikanda ni vema ccm mkawa na plan b ambayo ni Bernad Membe kuwa mgombea wa uraisi,chama kinapaswa kuwa imara na kisimuonee haya wala huruma anayeharibu misingi ya chama.
Na kama ccm haitaliona hilo kama la maaana,ninawahakikishia 2025 mtayaona yaliyotokea Congo.
Yangu machache hayo.
@#Swelana.
Sent using
Jamii Forums mobile app