Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Mabuludoza sio standard ya Membe.
Mabuludoza hajui Kiingereza
Mabuludoza hana utu
Mabuludoza hajui lolote kuhusu diplomasia na uhusiano wa kimataifa.
Mabuludoza hajui kufanya risk assessment.
Mabuludoza ana kisasi
Mabuludoza is wicked.
Ongezea kuhusu biashara ya korosho
 
Wakuu.
Tuache Utani jamaa anaakili hadi anaudhi, yaani mtu anajieleza Kwa umakini na unahisi kweli kiongozi anaongea
Anatumia busara kuelezea kitu, hafokifoki kama mtu tu wamtaani.
Hana hasira na anaonekana ni kiongozi aliyeiva sana kwenye masuala nyeti kabisa ya nchi kuliko viongozi wengi,
Membe usihi Daima nitazidi kukuombea kwa Mungu uwe na umri mrefu.
Nasimama na membe 2020 hili ghasia[emoji481] [emoji107]
 
Bado nina kiu ya kupata kiongozi atakayekubalika na moyo wangu hawa wote naona kabisa hawana dhamira ya kweli ya kututoa hapa tulipo.
 
C C M, C C M, C C M, Sikilizeni kilio cha Wananchi.

Wananchi tunateseka na Shida huku mtaani.
Je hamuoni siku hizi wananchi hawafanyi mambo ya maendeleo kwakuwa hawana uwezo.

Mfano, ukizunguka hapa jijini Daresalaamu,
Shughuri za Ujenzi wa Nyumba za kuishi hakuna.
Badala take siku hizi watu wanaziuza nyumba zao tena kwa bei che kabisa.
Nendeni Chamazi mkajionee karibu kila nyumba inauzwa, mafundi ujenzi hawana kazi tena kwa sasa.
Hapo tunajumlisha mafundi uashi, rangi, bomba, kuezeka, sakafu, marumaru nk.
Jambo hili linathibitisha kushuka kwa uwezo wa kunua wa wananchi, ( purchasing power )

C C M, ni lazima muingilie kati kwa jambo hili.
Wananchi wamekuaminini na kukuchagueni kwa miaka mingi ili muwanasue na huu mkwamo wao.

Ukweli ndio huu,
Unapo kataa kumpandishia mfanyakazi mshahara kwa miaka mingi, unampunguzia mwananchi uwezo wa kiuchumi kwa kiasi kikubwa na sio mfanyakazi tu.

Kumbuka mfanyakazi akijenga nyumba mafundi wata inua kipato chao.
Akishona nguo, au kulipa ada ya mtoto, anawaongezea kipato hao wateja wake.
Nakadharika.

Hivi ikitokea mmepata Raisi anayetesa RAIA wake namna hii bado mtampa awamu ya pili kugombea kiti cha uraisi ?

Kama anasera ya kufunga mkanda ili ajenge miundombinu, basi ilibidi kwanza aweke mjadala wa wazi ili kila MTU tu aridhie kuufunga huo mkanda Bali pia ajiandae na huo mkanda wake.

Na sio tu kumlazimisha mwananchi bila ridhaa yake huku tukishuhudia baadhi ya wananchi wakijitapa tena hadharani kuwa wanaishi maisha ya raha mustarehe kwa sasa.

Kama hamumpendekezi Membe, basi mpeni kijiti, Januari Makamba au Masele. Mbona mna watu wengi waadirifu na wema kwa raia.

Tatizo LA upinzani naona kwa kipindi chote hiki bado hawajajipanga katika ngazi ya mgombea uraisi.
Mkituuliza wananchi kwa sasa wala hatujui Upinzani umemwandaa nani kugombea kiti cha Uraisi.

C C M, C C M, C C M, Chama Cha Mapinduzi, Sikieni kilio Cha Wananchi Wenu.

Naipenda Nchi Yangu Tanzania na Sina pa Kukimbilia, Hakika Ningekimbilia.
 
Tunaenda na Magu mpaka 2022 ( Miaka 7 awamu ya kwanza) then anatuchukua awamu ya pili mpaka 2029 akimaliza hana cha kuongeza muda then ndio tunaanza kujadili wengine wa kumrithi
HAKIKA.
 
Twataka MTU mwenye exposure Na vision aijuaye dunia.Ukataka kufanikiwa kuwa Na maendeleo ni lzm uliwe,China ,USA zote zinaliwa thus Wana maendeleo, tusipoliwa tutazidi kuwa masikini milele
 
Mimi nasimama na magufuli 2020 magufuli tu atosha kazi na bata
 
Sio busara na ni kinyume cha taratibu za chama kuanza kumpigia kampeni Membe kwa sasa.
 
Kwa nini kama mnajua mgombea wenu anafanya vizuri na anaungwa mkono na watu wengi mnahaha kujaribu kuzuai wengine wasigombee naye???? Kuna mambo hayaga utata katika maisha. Ukiona kuna woga ujue kuna shida mahali.
 
Acha uongo mbona mi siuwazi
Hata mimi nautaka urais kupitia CCM. Tena nautaka 2020 na si muda mwingine. Huwezi kunizuia kugombea kwa sababu ya mazoea tu. Waje akina Membe tuchukue fomu wote tupimwe na wanachama wetu nani anakubalika kupeperusha bendera ya chama chetu. Tusikubali kutishwa na watu waoga (Waoga wa namna hii kwa kiingereza wanaitwa "coward").
 
Mkuu vitu vingine unapaswa utafakari sana. Hivi unadhani kwamba Raisi Magufuli kama Mwenyekiti wa CCM atajiweka kwenye mazingira ya CCM kuteua mgombea wa CCM mbadala wake? HUyu Magufuli ninayemfahamu au mwingine? Au hujaona tayari ameshajiwekea mazingira kwamba hilo lisiwezekane hata kidogo?
Kwani Membe akiona hawezi kugombea 2020 kupitia CCM si ajiunge na chama kingine chochote ndani ya Tz atimize ndoto yake? Vyama vyote hapa Tz viko chini ya mlezi moja.
 
Back
Top Bottom