C C M, C C M, C C M, Sikilizeni kilio cha Wananchi.
Wananchi tunateseka na Shida huku mtaani.
Je hamuoni siku hizi wananchi hawafanyi mambo ya maendeleo kwakuwa hawana uwezo.
Mfano, ukizunguka hapa jijini Daresalaamu,
Shughuri za Ujenzi wa Nyumba za kuishi hakuna.
Badala take siku hizi watu wanaziuza nyumba zao tena kwa bei che kabisa.
Nendeni Chamazi mkajionee karibu kila nyumba inauzwa, mafundi ujenzi hawana kazi tena kwa sasa.
Hapo tunajumlisha mafundi uashi, rangi, bomba, kuezeka, sakafu, marumaru nk.
Jambo hili linathibitisha kushuka kwa uwezo wa kunua wa wananchi, ( purchasing power )
C C M, ni lazima muingilie kati kwa jambo hili.
Wananchi wamekuaminini na kukuchagueni kwa miaka mingi ili muwanasue na huu mkwamo wao.
Ukweli ndio huu,
Unapo kataa kumpandishia mfanyakazi mshahara kwa miaka mingi, unampunguzia mwananchi uwezo wa kiuchumi kwa kiasi kikubwa na sio mfanyakazi tu.
Kumbuka mfanyakazi akijenga nyumba mafundi wata inua kipato chao.
Akishona nguo, au kulipa ada ya mtoto, anawaongezea kipato hao wateja wake.
Nakadharika.
Hivi ikitokea mmepata Raisi anayetesa RAIA wake namna hii bado mtampa awamu ya pili kugombea kiti cha uraisi ?
Kama anasera ya kufunga mkanda ili ajenge miundombinu, basi ilibidi kwanza aweke mjadala wa wazi ili kila MTU tu aridhie kuufunga huo mkanda Bali pia ajiandae na huo mkanda wake.
Na sio tu kumlazimisha mwananchi bila ridhaa yake huku tukishuhudia baadhi ya wananchi wakijitapa tena hadharani kuwa wanaishi maisha ya raha mustarehe kwa sasa.
Kama hamumpendekezi Membe, basi mpeni kijiti, Januari Makamba au Masele. Mbona mna watu wengi waadirifu na wema kwa raia.
Tatizo LA upinzani naona kwa kipindi chote hiki bado hawajajipanga katika ngazi ya mgombea uraisi.
Mkituuliza wananchi kwa sasa wala hatujui Upinzani umemwandaa nani kugombea kiti cha Uraisi.
C C M, C C M, C C M, Chama Cha Mapinduzi, Sikieni kilio Cha Wananchi Wenu.
Naipenda Nchi Yangu Tanzania na Sina pa Kukimbilia, Hakika Ningekimbilia.