Urais ni kazi ngumu sana ambayo siyo kila mtu anaiweza

Urais ni kazi ngumu sana ambayo siyo kila mtu anaiweza

Waoooo ephen wanguu waridi wa ❤️ wangu.karibu sanaa ephen.nilikuwa mpweke utafikiri mtoto anayenyonya aliyeachwa na kutelekezwa na mama yake.moyo wangu ulikuwa umesinyaa kwa huzuni utafikiri maua yaliyokosa maji.nilikukumbuka sana jukwaani hapa ephen.ni wewe unipaye furaha,tabasamu na kicheko moyoni mwagu . Ni wewe uliye chemchemi ya ya furaha ya moyo wangu.ephen karibu sana.ni kweli tunatofautiana Mitizamo kiitikadi lakini ipo siku utamuunga mkono mama yetu mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan, huku ukibubujikwa na machozi ya majuto ya kwanini ulichelewa kujuwa kuwa Mama huyu mwenye moyo wa upendo, ukarimu, unyenyekevu na uzalendo ni mpango wa Mungu Mwenyewe katika kuwainua watanzania na amejitoa na kujitolea kuwatumikia watanzania.ephen natamani niendelee kuandika lakini naomba niishie hapa maana Najuwa hupendi maandiko marefu.
Dahhhh🤣🤣🤣🤣🤣
 
Siku za mwisho kila goti litapigwa mbele za Mungu , kila ulimi utakiri kuwa Tundu Antipas Lissu ndiye rais aliye kwenye mpango wa Mungu na kila mkono utampigia kura Tundu Antipas Lissu kuwa rais wa Tanzania 2025 .
 
Siku za mwisho kila goti litapigwa mbele za Mungu , kila ulimi utakiri kuwa Tundu Antipas Lissu ndiye rais aliye kwenye mpango wa Mungu na kila mkono utampigia kura Tundu Antipas Lissu kuwa rais wa Tanzania 2025 .
Sahihi kabisa
 
Andiko langu lipo wazi na limenyooka kabisa.maana mimi huwa siandiki na kuacha mashimo mashimo nyuma. Ni Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mwenye uwezo wa kuliongoza Taifa letu mpaka 2030.
Hata maandiko ya mchungaji Msigwa kuhusu Mbowe yalikuwa ya Kumsifia kama Yako kumbe ilikuwa " zilongwa mbali Zitendwa mbali" 😂😂😂😂
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kama kuna kazi ngumu na nzito na yenye majaribu mazito na mitihani ya kila aina na yenye kukuweka roho juu juu na presha muda wote basi kazi hiyo ni ya Urais. ni kazi nzito ,ni msalaba Mzito ambao mtu hujitwisha Mabegani mwake Ni kazi inayokufanya ukose usingizi,kukosa hamu ya kula chakula,kupumzika,kutulia na familia yako,uhuru wako binafsi na mambo mengine mengi.

Unaweza ukawa waziri mzuri au mkurugenzi mzuri wa taasisi au kampuni lakini usiweze kuongoza nchi hata kwa wiki moja tu kabla ya kujikuta ukitoa matamko yenye Utata,yenye kuleta taharuki na sintofahamu. Kwa sababu urais ni kazi inayohitaji busara,hekima, unyenyekevu,subira,stamina ya kifua, uvumilivu,moyo wa kusamehe, ujasiri, misimamo na kutokukubali kuyumbishwa.

Urais unahitaji kuwa na jicho la tatu hasa katika kupokea na kufanyia kazi ushauri .maana unapaswa kupokea kila taarifa,kila habari,kila tetesi juu ya jambo fulani au mtu fulani au taasisi fulani ili ufanye maamuzi au kutoa neno au tamko lakini Mwisho wa siku wewe ndiye unatakiwa kwa kutumia akili zako ulizopewa na Mungu wako kuchuja na kupima jambo hilo katika usahihi wake usioacha makosa.

Ugumu na uzito wa kazi hii ya Urais ndio maana unaweza kuona mwingine anakonda kila siku au kuzeeka kila siku kwa sababu ya mawazo mazito na majukumu mazito ya kazi hii. Kumbuka unakuwa unaongoza watu ambao kila mmoja ana akili yake na mawazo yake.unaongoza hadi watu ambao hata ufanye jambo gani zuri wao watakupinga na kukukosoa tu.wao kila kitu ufanyacho ni kibaya kwao na hakifai na kinafaa kupingwa .

Kumbuka Urais hata mwananchi wa kijijini huko Mbozi Mkoani Songwe akinyanyaswa na Mgambo au Mtendaji kata anakutupia lawama wewe Rais ambaye upo ikulu Dar au Chamwino Dodoma na kusema kuwa hata kupigia kura uchaguzi ujao.Mgonjwa akijibiwa vibaya na muuguzi au nesi hospitalini au zahanati huko Namanyere au Laela sumbawanga utaona laana na lawama zote anakutupia wewe Rais ambaye upo Dar ukisaidia wajane na yatima chakula .kwa hiyo unaweza ukaona ugumu wa kazi hii ambapo unabeba lawama za kila aina hata kwa mambo ambayo hujafanya wewe wala kuagiza.

Urais ni mgumu na unaohitaji roho ngumu na ya ujasiri na misimamo ya hali ya juu sana katika kufanya Maamuzi ,hususani ya uteuzi,utenguzi na uhamisho wa watendaji na watumishi pamoja na wasaidizi wako. Maana kuna wakati mwingine unaweza hadi kupandikizwa hofu au uoga kuwa fulani usimteue wala kumpa nafasi yoyote ile serikalini kwa kuwa siyo mtu mzuri au hakuungi mkono au hakupendi au huwa anakusema vibaya au ni kundi au mtu wa fulani.kumbe wanaokuwa wanasema haya wanakuwa tu wanahofu ya mtu huyo kuchukua au kuhatarisha nafasi zao kutokana na uchapakazi , uzalendo,uadilifu wa mtu huyo.

Au wengine wanaweza kusema mtu fulani usimtoe katika nafasi fulani kwa sababu ni mtu muhimu sana na ana siri nyingi sana au amesaidia sana wewe kuwa hapo au ni mtu wa muhimu sana katika ushindi wako au huyu ndio kiboko ya wapinzani wako.wanaokuwa wanasema haya wanasema hivi kwa kuwa wana maslahi yao binafsi na kulinda mirija ya unyonyaji waliyotengeneza kupitia mtu huyo na hivyo kuhofia kuwa akiondoka inakuwa ni mwisho na kukatwa kwa mirija yao. Kwa hiyo hapa inahitaji ujasiri wa Rais mwenyewe katika kufanya maamuzi kijasiri bila kujali maneno yanasemwa vipi.ni kuishinda hofu na uoga na kujuwa kuwa hana ubia katika Urais wake na ana mamlaka yote kikatiba na kisheria na kwamba wabia wake ni wananchi pekee na siyo kikundi fulani cha watu.

Urais unahitaji utulivu wa hali ya juu sana katika kufanya maamuzi na kutoa matamko. Kwa sababu kauli za Rais zina Athari kubwa sana katika jamii kitaifa na kimataifa. Hivyo Rais hapaswi kuongozwa na hasira,jazba,chuki,visasi,Udini,ukabila, undugu na kujuana katika kufanya maamuzi.Ndio maana nasema siyo kila waziri mzuri anaweza kumudu nafasi ya Urais. Ikulu ni mahali pazito sana ndugu zangu. Ni mahali ambapo wakati mwingine usipokaa sawa unaweza jikuta watu wako wa karibu unaowaamini wakawa msitari wa mbele kukuhujumu,kukuchafua ,kukuchonganisha na umma kwa kificho kwa kutumia watu wa pembeni au wapinzani.

Mwisho niseme kuwa Rais Samia ANATOSHA kwa Urais na anastahili kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa kuwa anakidhi vigezo anavyopaswa kuwa navyo Rais. Kazi hii ya Urais ina watu wake walioandaliwa na Mungu Mwenyewe na siyo wewe kuutafuta kwa jasho na Damu. Wengine kikomo chao ni kwenye uwaziri tu na kuendelea kupewa maelekezo kutoka juu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Headless chicken Lucas Mwashambwa is here again! Kama poyoyo zinaweza nani atashindwa? Ni kama kazi zingine tu!
 
Siku za mwisho kila goti litapigwa mbele za Mungu , kila ulimi utakiri kuwa Tundu Antipas Lissu ndiye rais aliye kwenye mpango wa Mungu na kila mkono utampigia kura Tundu Antipas Lissu kuwa rais wa Tanzania 2025 .
Huyo Lissu hawezi hata kujiongoza. Muulize hela alizochangiwa kununua gari amepeleka wapi?
 
Ungesoma uelewe na siyo kukimbia kutoa maoni yako bila kuelewa mada.Mama anaweza vyema sana na ndio maana hapo mwisho nimeeleza kuwa anatosha na anastahili kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili
Urais ni kazi sababu kuficha mikataba mibovu kwa zama hizi za kuhoji ni kazi ngumu

Kuficha ufisadi na matumizi mabovu ni kazi ngumu

Kusema watu wanafanya drama wakati wanatekwa ni kazi ngumu

Kuwafuga watu kama Nape ,January na Mwigulu ni kazi ngumu sana,

Kuiba kura TLS Mwabukusi asishinde ni kazi ngumu

Ongezea nyingine umalizie na kazi ngumu sana
 
Ugonjwa huingia kwa haraka na huondoka taratibu. Lucas umeanza kupona taratibu Sasa hatimaye umekiri kwamba huyo bi mkubwa hafai ! Akili zitarudi tu endelea na dozi.
Hapana hajakiri kuwa mama hafai bali lengo lake ni kutoa tahadhari kwa Rais wa TLS Mwabukusi.
 
Kazi ya urais ni rahisi sana ukiwa upande wa haki.Na kazi ngumu na ya kijinga ni kuwa chawa wa mtu na kuanzisha vi thread uchwara vya kumsifu mtu
 
Uraisi ni kazi kubwa ndiyo,lakini mama amejitahidi sana hadi kuifanya tanzania iwe hapo miradi mikubwa yote ya baba aliyoiacha mama ameindeleza na kuimaliza isitoshe ni mwanamke tu.

mama samia mitano tena.
 
Back
Top Bottom