Maendeleo ya vitu hayana maana kama hayabadilishi maisha ya watu kwa muda mfupi na muda mrefu.
Urais sio uwaziri wa miundo mbinu ndugu. Ni maendeleo ya watu, ni ustawi wa jamii, ni ukuaji wa kipato cha mwananchi wa kawaida, ni uwezo wa kununua na kulipia mahitaji muhimu na ya lazima, ni furaha katika jamii, ni ukuaji na maendeleo ya huduma za jamii, ni utawala bora, ni uhuru na demokrasia, ni uwezo wa kugharimia mavazi, chakula, na malazi.
Urais sio kutembea na kundi la walinzi na magari na ndege za kivita. Urais ni alama ya upendo, amani, umoja na mshikamano. Ni alama ya mfariji mkuu, ni kimbilio la walioonewa, ni kilimbilio la wanyonge, ni alama ya ucha Mungu, ni kuhani mkuu katika nchi, ni mtetezi wa wajane na watoto yatima, ni baba kwa wasio na baba, ni mpatanishi, ni mwamuzi, ni mfariji.
Urais sio uungu, ni ubinadamu, ni unyenyekevu, ni utu wema, ni upole, ni kiasi, ni usamaria, ni uponyaji, ni usikivu, ni uhodari, ni ucha Mungu.
Urais sio miundo mbinu.
Urais ni taasisi pana.
Maendeleo hayana chama