Tunayo mambo mengi tu ya muungano lakini suala la Uraisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar siyo mojawapo.
Hivi sasa chama cha Mapinduzi kiko busy kutafuta mgombea uraisi wa Zanzibar, katika vitu ambavyo ni makosa ni kuwahusisha Watanganyika katika mchakato wa kumtafuta mtu ambaye atakuwa raisi wa Wazanzibari.
Hivi karibuni kutafanyika mchakato wa uteuzi wa mgombea uraisi wa Zanzibar ndani ya CCM, pamoja na kwamba mchakato utaanzia Zanzibar lakini bado Watanganyika waliomo kwenye kamati kuu na baadae mkutano mkuu wa CCM Taifa utahusika sana katika kuwapata wagombea wa nafasi ua Uraisi huko Zanzibar...