Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Pia soma ~ Zahanati ya Kata ya Itundu, Wilaya ya Urambo - Tabora, Mganga Mfawidhi anaenda kazini anapojisikia
Zahanati hutoa huduma katika ngazi ya Kijiji na siyo Kata kama inavyoelezwa katika taarifa hiyo. Huduma katika zahanati hutolewa kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa tisa na nusu alasiri. Aidha Timu ya uchunguzi imebaini kuwa picha inayosambaa inaonekana imepigwa baada ya saa tisa na nusu alasiri, sambamba na hilo Timu ya uchunguzi ilizungumza na wananchi wa eneo husika pamoja na wateja waliokuwa wakiendelea kupatiwa huduma katika zahanati hiyo, ambapo wote walikanusha uwepo wa madai hayo.
Aidha Zahanati ya Kijiji cha Itundu ina watumishi zaidi ya mmoja, hivyo utoaji wa huduma hauhusiani na uwepo wa Mganga Mfawidhi pekee. Na, inapolazimu Mganga Mfawidhi kutokuwepo kazini, hali hiyo hutokea kwa nadra na mara nyingi ni kwa sababu za kikazi zinazohusu usimamizi na utekelezaji wa majukumu ya zahanati katika ngazi ya Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo inatoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa hiyo. Aidha inasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuwasilisha malalamiko, maoni na mapendekezo yao kupitia mifumo rasmi ya Serikali iliyowekwa kwa ajili ya kupokea na kushughulikia changamoto za wananchi. pia inaende-lea kusisitiza utoaji wa huduma bora, salama na zenye kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma na hait-ovumilia vitendo vyovyote vinavyokwenda kinyume na viwango vya utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo