Tanzania ina physcists wa kiwango gani , world class au ! basi ili mradi tu , umeshaona hata paper moja kwenye journal ya kimataifa kuhusu masuala ya nuclear iliyondikwa na mtanzania ? .
hatufanyi hata basic research kwenye masuala hayo unafikiri knowledge itatoka wapi ?
Ninapo ongelea world class physicists nina maana kana , Dirac , Einstein, Max Born , stephen hawking , chandrashekar na wengine.
Hata ukiangalia hawa wataalamu wetu wamepata Phd zao wapi ? ,ni vyuo fulani second rate , siyo cambridge ,oxford ,Gronigen ,harvard au hata Uc berkley .
lazima mtambue mtaalamu mzuri anategemea sana professor wake alikuwa nani hilo ni muhimu sana nitakupa mfano .
Homi Jehangir Bhabha,
FRS (October 30, 1909 January 24, 1966) huyu ndio mtaalamu wa kwanza wa technolojia ya nuclear ya india na alikuwa mwanafunzi wa
Dirac miaka ya 30's.
Dai Chuanzeng huyu alikuwa mwanafizikia aliyejifunza masuala ya nguvu za atomiki chini ya
professor chadwick mvumbuzi wa neutron pale cambridge university , mchina huyu alivyorudi kwao akaenda kuanzisha utafiti wa masuala hayo mpaka china ikaja kuwa nuclear power.
kwa hiyo haya mambo yanakwenda kwa mipango mizuri ya muda mrefu ukiangalia kutoka wakati huo miaka ya thelathini mpaka china inapata kuwa na nguvu za atomiki ni zaidi ya miaka thelathini.
kwa hiyo ni kwa kiwango gani tunasomesha wataalamu wetu kwenye vyuo vizuri vyenye world renowned scientist na kwa kiwango gani tunawajali wataalamu hawa ili wasiingie kwenye siasa ili kufuata pesa za mizengwe ndio factor itatuwezesha kwenda mbele. na sio blabla.
nenda pale udsm utakuta hata hawa maprofesa tulionao hatuwajali wamekata tamaa na maisha. unafikiri ni nani atakuwa na uwezo kufanya utafiti wa kiwango cha juu kama ana matatizo binafsi .
Fundi Mchundo:
Nakushangaa sana unaposema pwani watumie hiki, vijijini watumie kile. Je ni nani atakusaidia katika mambo hayo? Je ni kila siku tununue hivyo vitu bila ya kuwa na wataalamu wenye kuelewa hivyo vitu?
Ukikubaliana na mimi kuwa tunahitaji watu wa kuelewa siri ya teknologia hizi, basi NYUKI hatakuwa mbali sana nasi.
Katika hoja yako moja umezungumza masuala ya computer nilipoeleza mambo ya DVD. Samahani ukunielewa. DVD ina kama sehemu mbili muhimu, sehemu ya kwanza ni ya mathematics (Data compression) na sehemu ya pili ni media (laser disk) ambayo inaweza kustore data. Sehemu ya kwanza ya mathematics ilishagunduliwa zamani lakini ilisubiri laser technology. Hivyo sikuzungumzia masuala ya computer repair kwani ayefaidika zaidi kwenye biashara ya computer ni mwenye intellectual property, kutengeneza chip au mwenye ku-develop software.
Kama vile mathematics part ya DVD ilisubiri kwa muda mrefu maendeleo katika masuala ya laser technology, amini usiamni watu wanalifanyia kazi usiku na mchana usalama wa NYUKI.