miss chagga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 57,811
- 49,053
Utafikiri wamevaa helmet kichwaniMimi mwanamke anayevaa wigi hata awe mzuri vipi sitongozi
Wananuka kama mzoga
Wanja najaribu jaribu, kucha hapana nlivoumizwa siku ile sirudii, afu ilikua kutoa ushamba tu nna kucha ndefu za mikono na miguu hata sina haja ya kubandikahahahha nimecheka hapo namba nne! binafsi wanja mweusi unahitaj wito! me pia wanja mweusi najhs kchekesho tupu! wanja blown ni mtamu ujue tu kuushape! mie niliipa 20000/=kufundishwa kujishape wanja km wa lulu lol! anza mdg mdg wanja unaongeza urembo mnoo!
kope mie nilibandika sik ya harus zile fupi nikawa romantic hatar! toka hapo sijawah fikiria kubandika kope! mie yale maref ya kina irine uwoya huwa nashindwa jaman kuelewa!
mie kucha nabandika mara moja moja!nikiwa na moody!
pambana na hali yako tu mamy! lol!
Kuna vingine sijawahi kujaribu, vingine nimejaribu vikanizidi uwezo....
1: kupaka wanja kwenye nyusi
Huu urembo ulinishinda tangu enzi za mwalimu, kila nikijaribu naona nakua Kama nyau hasa hasa wanja mweusi, basi nikijaribu kupaka nafuta naendelea na mambo mengine, mara chache nimejaribu wanja wa brown napaka kwa mbaaali naona unakuja kuja mdogo mdogo ntaweza.
2: kuvaa wig/kushonea weaving
Hapa nimeinua mikono, wig nilivaa mwaka flani wakati naanza kusokota dread siwezi kwenda kazini vile, nikanunua wig kwanza dukani tu naambiwa linauzwa elf 25 nikashtuka nlijua buku ten, nikanunua nikavaa mmh najiona nakua kama kanjibai, linawasha, lina joto nlipata shida, nywele zilivorefuka sijarudia tena huu urembo siuwezi kabisa.
3: kubandika kucha
Nilijaribu siku moja kutoa ushamba, naona shost angu kila siku anabandika anapendeza, akanipeleka namie nikabandika mmh siku hiyo hata kutandika kitanda nilishindwa, kuchomeka shuka kwenye godoro ikawa tabu, siku chache nikazoea, siku ya kuzibandua sasa yani zinang'olewa utadhani nimetekwa nlikua na kazi ya kupiga kelele kama kimbwa, sirudii tena sitarudia kabisa.
4: kubandika kope
Hii kujaribu tu siwezi make, nikiwaona kina mwajuma ndalandefu wanavokua huwa nacheka, kope zinasimama utadhani mtu kavaa kofia, yana wenyewe haya
5: kupaka cream/kujichubua
Hii kazi ya kujipa mateso hii, uso mweupe miguu myeusi, kuna siku nliwekewa maji ya cream bila kujua ushamba huu, nimeulizwa tu niweke maji nkajibu eeh weka nlijua labda glycerin, duh siku mbili tu nkaanza kuwa kama tumbili....
Wewe huwezi nini?
Nb: naombeni mniambie mafuta ya nywele natural, naona nywele zinakatika
basi mkuu ukienda tukuyu utaishi single maisha yako yote utakayokuwa pale..Mimi mwanamke anayevaa wigi hata awe mzuri vipi sitongozi
Wananuka kama mzoga
Sio Wote wavaao hayo "mawigi" huwa yananuka.
Yapo ambayo ni masafi Sana, ingawa hata Mimi binafsi sifurahii nikutanapo na anayevaa kwangu hunipunguzia ladha Fulani.
Ndio nilichokupendea hicho.Wigs, kope za kubandika, weaving, kujikoboa...vyote vimenishinda. Nimebakiza kutinda nyusi mara moja kwa miezi na mafuta yangu ya Nazi MINARA..nimemaliza.
Huko ndiyo style yao?basi mkuu ukienda tukuyu utaishi single maisha yako yote utakayokuwa pale..
Mimi sipendi mwanamke mwenye kuvaa minguo mingi. unakuta mtu kavaa kyupi, skin taiti kisha suruali ya jinzi juu, sasa ukute na tojo la saridalamu, mpaka maku ina kanu vibaya.
basi mkuu ukienda tukuyu utaishi single maisha yako yote utakayokuwa pale..
Uchafu, Majasho, kuvaliwa muda mrefu bila kubadilishwa hizo zaweza kuwa miongoni mwa sababu.mie nadhan kunuka wig ni uchafu sijui niseme majasho!au yale ya bei ya chin nadhan!
mimi pia nazipenda...Sijawahi kuchora wala sina tattoo, japo nazipenda
wanyakyusa bana sijui wana matatizo gani,wanawake ni wazuri tu ila hawaki kuwa natural....kujichubua sasa khaa!
afu wana sauti kali mno,hawajui kubembeleza kike eti..