huyu hajapendeza
watu oo tusiponunua za bandia hatupendezi,huyu nae si mtanzania ama watu ni wabaya tu ama hawajiamini na nywele zao angalia na hii pia ya flavian matata
jamani kweli kwa nywele za asili hampendezi? ona na huyu
nani anasema huyu hajapendeza na afro yake?
utawasikia wanawake wanalalamika yaani mimi nisuke twende kilioni,kwani lazima usuke twende kilioni,si nywele zenu na staili ni ubunifu wenu. huyu kapendeza mbona.
hata huyu nae hajapendeza?ama watu ndio wabaya?
huyu ni mwanaume gani atasema hajampendeza ama hamtaki? ama tatizo watu ni wabaya tu na hawajiamini?
good look.
eti na huyu hajapendeza kwa sababu hajanunua nywele za bandia?ama tatizo wanawake wanaosema hivyo ni wabaya ama hawajiamni?
hata leo nikiambia oa naenda kwa mzee kumwambia aandae ng'ombe pamoja na kwamba hana nywele za bandia
matata huyu hajapendeza?
WANAWAKE EBU NIAMBIENI,NYINYI MNAOGA KILA SIKU ALAFU NYWELE ZINAACHWA WIKI NZIMA HAZIGUSI MAJI NA HATA WIKI MBILI KISA NI ZA BANDIA ZITAHARIBIKA, HAMUONI KAMA NI TATIZO NA NI UCHAFU NDO MAANA WENGI HAWAISHI KUSEMA NYWELE ZINANIWASHA,ZINAUMA, ZITAACHAJE KUWASHA WAKATI HAZIOGI WIKI NZIMA?NA HATA WAKATI MWINGINE ZINANUKA WEWE UNADUNDA TU ETI HAZIJAFUMUKA.
HEBU JARIBUNI NA KUBUNI STAILI ZA KIAFRIKA KWA NYWELE ZA KIAFRIKA.
eti mtu anatumia 50,000 kusuka kila wiki,wanaume mtatuua,si bora ufuge nywele zako kama hawa wadada na gharama ya kuzitunza inakuwa ndogo na zingine ile familia,kwa mwezi laki mbili inahitajika kwa ajili ya nywele,mbona balaa.