Urembo wa Picco na Henna

Urembo wa Picco na Henna

Urembo huu ni moja kati ya mitindo yenye kupendeza na kuvutia
Ni mtindo maarufu sana kwenye maeneo ya pwani hususani ni Tanga, Unguja, Pemba Dar es salaam na Mombasa, na hata kwenye maeneo mengine pia fashion hii ila nadhani wote tutakubaliana ya kuwa kwa hakika ukanda wa pwani ndio kiboko yao.

Mtindo huu hutumika pia kwa mabibi harusi na hata wahudhuriaji maharusini na kwenye sherehe zozote zile au kwa ajili ya kujipamba tu.
Ikiwa utapata mchoraji mzuri basi kwa hakika utavutia

Ruksa na wewe kutupia picha zako mbali mbali zinazoonyesha mtindo huu wa Picco kama nawe ni mpenzi wa mtindo huu
View attachment 421552
nina mipicha mingi mizuri ya piko tatizo hili LI SIMU HALI UPLOAD PICHA
 
Kwa sisi wenye rangi adhimu ya kiafrika huo urembo unatuhusu? coz naona picha ni za watu wenye rangi za mitume tu, nahisi mm nikipaka itabid wananchi watumie microscope kuona hyo michoro.
Jamani usiseme hivo wanawake sote wazuri vyovyote ulivo iwe mweupe mweusi ukipaka hio hina na piko lazima utabadilika utazidi kupendeza
 
Jamani usiseme hivo wanawake sote wazuri vyovyote ulivo iwe mweupe mweusi ukipaka hio hina na piko lazima utabadilika utazidi kupendeza
Ni kweli kila rangi ina uzuri wake
 
Binafsi mwanamke ambae anapaka pico na hina ananivutia sana.

Tatizo langu moja tu nina wivu sitaki watu wengine wamuone jinsi alivyopendeza na pia akienda kuchorwa kwa mashoga zake sina imani nao naona kama watamshawishi halafu nitaibiwa.

Kwenye kucha apake hinna sio zile rangirangi..usoni apake wanja sio mapoda poda na rangi rangi za macho
Kama mimi tu aisee
 
hina.jpeg
mie tayari
 
Back
Top Bottom