Mtoto huyo
Aisee embu pandisha kidogo iyo camera...
Haha unataka kuona nini
Hapa kuongea kigugumizi....subiri nisogee karibu....
Usiniguse!!!!!
Usiniguse!!!!!
Suala la urembo kwa sisi wanawake linjumuisha mambo mengi sana kuanzia mavazi na hereni, vishaufu bangili vidani na makochokocho mengine.
Siku za karibuni kumeibuka mtindo wa wanawake kuvaa vikuku yaani cheni za miguuni. jambo hilo limekuwa likipigiwa kelele na baadhi ya watu wenye mrengo tofauti wakihusisha jambo hilo na tabia zisizofaa.
Lakini cha kushangaza nimewahi kuona baadhi ya wabunge wanawake na viongozi wa kike serikalini tena wenye mamlaka makubwa wakiwa wamevaa vikuku tena wengine walipata hata fursa ya kupiga picha na mkuu wetu na vikuku vyao.
Ninachofahamu mimi, bungeni ni mahali ambapo mavazi yanazingatiwa sana, na ninaamini wengi wetu tumewahi kushuhudia baadhi wabunge wakitolewa nje kwa sababu ya mavazi yao kuonekana kwenda kinyume na matakwa ya bunge, lakini pamoja na jamii huku nje kuwahukumu wanawake wanaovaa vikuku kama watu waliopotoka kimaadili, lakini kwenye eneo hilo la bunge inaonekana jambo hilo limepewa Baraka.
Sasa kwa kuwa suala la urembo kwa wanawake linaenda na wakati, hivi sasa tumerudi Kiafrika Zaidi, na sasa urembo wa shanga umechukua nafasi. licha ya shanga kutumika kama chachandu ya kunogesha mapenzi kwa kuvaliwa kiunoni na wanawake, lakini kwa miaka mingi urembo wa shanga umekuwa ukitumiwa na waafrika wake kwa waume katika kujipamba.
Mfano mzuri ni kwa Wamasai ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakijipamba kwa shanga wake kwa waume na wamekuwa wakipendeza haswa.
Sasa miye hivi karibuni nimeamua kujipamba Kiafrika Zaidi kwa kutupia urembo wa shanga mwilini kiunoni hadi mguuni.
Sasa sijui wenzangu mtanionaje?
CC:
miss chagga, miss neddy, miss strong, Karucee, MankaM, DEMBA, Munkari, tinna cute, Tina, Paloma, sister, Ennie, Arabela, Preta, farkhina, Asprin, Mentor, watu8, charminglady, mwekundu, Fixed Point, Ruttashobolwa utafiti, Tyta, Kaunga, Neylu
Kumbe mmekaribiana eeeeh.....lol
Mi siimoo!!!Hahaha utajua uko uko
Weee wacha kutuchungulia!!!
Kwani hiyo picha ya mguu wenye shanga unadhani ni ya nani