Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada

Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada

Tumezowea kuona baadhi ya jamii kama wamasai wakivaa shanga miguuni au vikuku kwa wanawake na bila kuwa na tafsiri mbaya katika jamii.

Ila zinapovaliwa na waswahili tunakuwa na maana tofauti. Kama ni Mwanamke basi anaonekana ni muhuni.Mwenye uelewa wa dhana hii katika jamaii em share hapa.
 
1. Ana mwanaume zaidi ya mmoja
2. Ni mshirika wa Ibada za Shirki

Last but not listed: kuna mstari mwembamba kati ya shanga zile wanazovaa na mambo ya kucheza mechi za Kinyume champion League.

Asanteni.
 
Nini madhumini na matumizi ya vitu vifuatavyo wavaapo wakina dada na akina mama katika jamii yetu?

1: Kipini cha puani a.k.a (Kishaufu) iwe kushoto au kulia
2: Kikuku iwe mguu wa kushoto au kulia au yote kwa pammoja
3: Na mwisho ni Shanga za kiunoni.

Je, waonaje? Vyapoteza maana halisi kwa wanaovaaa hole hole hole au?

Maoni yako tafadhali changia..


======================================
MAJIBU YALIYOPATIKANA
======================================

Nimeona nilete mada hii ili kuwekana sawa katika ishu ambayo inaongelewa pasipo kuwa na ufahamu wa kina. Katika mapambo yanayotumika sana ulimwenguni na tena na watu wa marika tofauti ni pamoja na vikuku na vishaufu.

=> Kuhusu vikuku miguuni

DSC07523.JPG


Kwa makabila ya kiafrika vikuku huvaliwa kuanzia na watoto wachanga, wasichana, wanawake wa makamo na hata vikongwe.

Vikuku hivyo vyaweza kuwa vya shanga, ngozi, au hata madini kama dhahabu, fedha na hata shaba. Vyaweza kuvaliwa mguu mmoja au hata miguu yote.


vikuku.jpg






=> Kuhusu uvaaji wa Vishaufu/kipini puani
attachment.php

Tukirudi kwa vishaufu, urembo huu ambao huvaliwa puani aghalabu hupatikana kwa makabila ya pwani lakini kwa miaka ya karibuni umeenea hata kwa makabila mengine hasa kwa wasichana.

=> Kuhusu uvaaji wa shanga kiunoni



Hitimisho
:
Kwanini basi naleta hii ishu tuijadili ni kwamba, hapa JF nimesoma baadhi ya wachangiaji wakihusisha hasa vikuku na mienendo isiyofaa na kuleta dhana kuwa wenye kutumia mapambo hayo basi wana ajenda nyingine.

Binafsi napenda kusema kuwa urembo wowote waweza kutafsiriwa vyovyote - kwa ubaya au uzuri ila mwisho wa siku mtumiaji/mvaaji tu ndiyo mwenye kujua maana.

Wenzangu sijui mnasemaje?
HILI ni lishaufu thatha.
 
Back
Top Bottom