Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HILI ni lishaufu thatha.Nini madhumini na matumizi ya vitu vifuatavyo wavaapo wakina dada na akina mama katika jamii yetu?
1: Kipini cha puani a.k.a (Kishaufu) iwe kushoto au kulia
2: Kikuku iwe mguu wa kushoto au kulia au yote kwa pammoja
3: Na mwisho ni Shanga za kiunoni.
Je, waonaje? Vyapoteza maana halisi kwa wanaovaaa hole hole hole au?
Maoni yako tafadhali changia..
======================================
MAJIBU YALIYOPATIKANA
======================================
Nimeona nilete mada hii ili kuwekana sawa katika ishu ambayo inaongelewa pasipo kuwa na ufahamu wa kina. Katika mapambo yanayotumika sana ulimwenguni na tena na watu wa marika tofauti ni pamoja na vikuku na vishaufu.
=> Kuhusu vikuku miguuni
![]()
Kwa makabila ya kiafrika vikuku huvaliwa kuanzia na watoto wachanga, wasichana, wanawake wa makamo na hata vikongwe.
Vikuku hivyo vyaweza kuwa vya shanga, ngozi, au hata madini kama dhahabu, fedha na hata shaba. Vyaweza kuvaliwa mguu mmoja au hata miguu yote.
![]()
=> Kuhusu uvaaji wa Vishaufu/kipini puani
![]()
Tukirudi kwa vishaufu, urembo huu ambao huvaliwa puani aghalabu hupatikana kwa makabila ya pwani lakini kwa miaka ya karibuni umeenea hata kwa makabila mengine hasa kwa wasichana.
=> Kuhusu uvaaji wa shanga kiunoni
Hitimisho:
Kwanini basi naleta hii ishu tuijadili ni kwamba, hapa JF nimesoma baadhi ya wachangiaji wakihusisha hasa vikuku na mienendo isiyofaa na kuleta dhana kuwa wenye kutumia mapambo hayo basi wana ajenda nyingine.
Binafsi napenda kusema kuwa urembo wowote waweza kutafsiriwa vyovyote - kwa ubaya au uzuri ila mwisho wa siku mtumiaji/mvaaji tu ndiyo mwenye kujua maana.
Wenzangu sijui mnasemaje?