Huu uzi umenikumbusha mdada mmoja mmbongo kwenye party hivi karibuni. Alikuwa amevaa shanga kama hizi (picha ya kwenye post # 1) miguu yote na mikononi pia gauni lake lilimkaa vizuri sana pia alikuwa na kilemba cha kukata na shoka. Huu wimbo kila ukipigwa alikuwa akiinuka kwenda kuucheza na alikuwa akiucheza vizuri sana. Waalikwa wengine walipomshtukia kwamba anaucheza wimbo huu vizuri sana basi ulikuwa unaombwa kila mara ili wamuone tu huyo mrembo akifanya vitu vyake, na njemba wengine walikuwa wakienda kumuomba wacheze naye.