DOKEZO URGENT: Binti wa miaka 16 ameozeshwa kwa lazima kama mke wa pili, huko Laela, Sumbawanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hongera sana mheshimiwa, inatia moyo kuona bado kuna viongozi wawajibikaji. Pongezi nyingi sana kwako
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dkt. Gwajima D hujambo?

Nauliza swali. Naamini kwako nitapata jibu sahihi nami niweze kuwasilisha kwa mhusika.

Kuna binti, mwanafunzi wa kidato cha 3. Ana miaka 20 bila shaka. Mwaka huu, mwezi Februari alipimwa na kukutwa na ujauzito. Akapewa likizo akashughulike na ujauzito wake kisha atakapojifungua arudi kuendelea. Hii ni kulingana na sera ya elimu ya mwaka 21 au 22.

Sasa, binti kafika nyumbani na anataka kuolewa. Je, sheria inasemaje? Akiolewa, muoaji hatopata matatizo mbeleni?

Je, utaratibu wenu wa ufuatiliaji wa wanafunzi wote wanaokatisha masomo kwa sababu ya ujauzito upo imara kiasi gani? Ama huwa ni hiari, mwanafunzi akishika ujauzito na kusimama masomo, kurudi ni maono yake binafsi na wazazi wake?

Natanguliza shukrani.
 
Mheshimiwa gwajima rai yangu ni kwamba dawati la kijinsia kuwa nani ya kituo Cha polisi inaleta ukakasi. Watu wengi wanaogopa kuingia humo hasa watoto ukizingatia polisi walivyo na maigizo ya kutisha wananchi. Dawati la kijinsia litaftiwe kona nyingine
 
Kuna hoja hapa maana ule ukauzu wa polisi na mikwara yao unaogopesha watu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran, kesho lazima mkuu wa wilaya ataenda kuwakamata akishirikiana na vyombo vya dola
Inatakiwa busara itumike. Mazingira ya huko vijijini hakuna elimu na uelewa hivyo maisha kama haya ndiyo kawaida yao. Hawajui hata kama wanavunja sheria. Hivyo naishauri serikali isi-over react kwa kufunga watu miaka 30. Japo kutojua sheria siyo utetezi lakini itakuwa siyo vizuri kufunga watu miaka 30 kwa mazingira ya aina hiyo.
 
Hujielewi ,kama wao

Serikali ipeleke mswada wa mabadiliko ya Sheria ya ndoa Kwa umri 14yrs ,kimsingi bint amekizi vigezo vya kuolewa miaka 17

Labda awe mwanafunzi
Kichwani umebeba uono,
Kwahio hii inahalalisha kuolewa kwa lazima?
 
Mkuu laela ni wilaya ?
Duuuh! mkuu,angalia content,yaani unaanza kudili na jambo la Laela kama ni wilaya au mji mdogo?Aisee...
Hongera sana Dr.Gwajima,umerespond kwa haraka sana,hakika wewe ni kiongozi.Natamani baadhi ya viongozi waige mfano wako.Mengi huandikwa humu,lakini huwa hatuoni response kama uliyoonyesha kutoka kwa viongozi mbalimbali wa sekta mbalimbali.Kwa hili,nakusifu sana.Yaani umerespond nadhani kwa haraka,kuliko hata mbunge wa jimbo la Sumbawanga vijijini,ndugu Deus Clement Sangu,ambaye hapo Laela ndiyo nyumbani kwao.Mimi binafsi,siwezi kumlaumu, yawezekana katingwa na mambo mengi,na hajapata wasaa wa kuingia humu jamvini.
Kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yako,Dr.Gwajima.I wish,uje uwe hata waziri mkuu wa hii nchi,baada ya Majaliwa.
 
Ni upuuzi mkubwa kusema kupeleka msaada

Je,wangapi ambao hawakuweza fanya hivyo na wameolewa kwalazima ,waziri pelekeni mswada huo haraka Ili uwakomboe hao mabint au mnaiogopa bakwata
 
Ahsanteni sana Wadau wa JF kwa taarifa hii. Huu ndiyo ushirikiano wa jamii tunaohitaji. Tunashughulikia. Ahsanteni kwa mawasiliano ya namba ya simu.
Nimetiwa moyo sana kuona hii, Asante mheshimiwa Waziri
 
Kuna ndoa za utotoni na kuna ndoa za kulazimishwa. Hii kwa mujibu wa mtoa mada ni ya kulazimishwa. Usifanye juhudi zote za waziri kuwa hazina maana.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Kuna ndoa za utotoni na kuna ndoa za kulazimishwa. Hii kwa mujibu wa mtoa mada ni ya kulazimishwa. Usifanye juhudi zote za waziri kuwa hazina maana.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Naomba kuuliza! Hivi Ndoa za kulazimishwa huwa zinaangukia kwenye makosa gani!? Je ni Civil au Jinai!!??
 
Big up sana Dr. Gwajima for such an amazing response to this urgent call. you're a super leader!
 
S
Kuna ndoa za utotoni na kuna ndoa za kulazimishwa. Hii kwa mujibu wa mtoa mada ni ya kulazimishwa. Usifanye juhudi zote za waziri kuwa hazina maana.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
heria ya ndoa inasema wazazi wakiridhia na si mtoto akiridhia.Sheria ndio haifai muaoaji hana kosa hapo,kama serikali haitaki ndoa za utotoni ibadilishe sheria.Mtoto wa miaka 14 anaridhia nini kwenye suala kubwa kama ndoa? kama kupiga kura tu mtoto huyo haruhusiwi,kunywa pombe haruhusiwi ,kuendesha gari haruhusiwi eti ndoa ndoa ndio aridhie, huu ni wendawazimu.Serikali isitufanye wote hatuna akili kama kuna makundi ya dini inayaogopa kwenye hili suala la ndoa za utotoni ni heri iache hao watoto waendelee kuolewa
 
Mawaziri, Makatibu wakuu , maji nk...... Kila mwenye fom6 yupo jf.


Yamkini hata rikiboy aliyeweka Uzi wa kulana kimasihara ni naibu waziri, wachangiaji wakiwa wakurugenzi wa wizarani na makanali
😁😁😁
 
Inasikitisha..hivi mtu unaoaje binti wa miaka 16..hiyo so grooming?


Sad fact ni kwamba majority ya comments humu ndani wanaona ni sahihi huyo Binti kulazimishwa ndoa na kuolewa mke wa pili kwa umri huo!


Ubinaadam hakuna, Utu umepotea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…