Urgent: Utaratibu wa kupokea mishahara dirishani urudishwe haraka

Urgent: Utaratibu wa kupokea mishahara dirishani urudishwe haraka

Ni hivyo tuu, huu utaratibu urudishwe haraka. Sababu iko wazi, makato mapya ya kutoa na kuweka pesa bank hayavumiliki hata kidogo na yanamnyonya mfanyakazi directly sababu hajapewa option(s), yaani automatically anafosiwa kukatwa sababu hakuna njia ya kuuchukua huo mshahara bila kukatwa.

Haiwezekani hako ka salary nikalipie Income Tax, jumlisha makato lukuki na kubaki na ka take home kadunchuuu. Halafu ninapoenda kukachukua hako ka take home bado tena nilipe "Government Levy". Kwa nini nilipie kuchuchukua hako ka take home wakati nimeshalipa "Income Tax?".

Turudi old school tuu, mishahara itumwe kwa wahasibu wa halmashauri husika, kama ni taasisi basi zitumwe kwenye ofisi husika, kisha mtumishi ataamua yeye anapeleka bank ama anakaa nazo.
Ata ukirufishwa izo tozo zitapelekwa kwenye hayo madirisha
 
images76543.jpeg
 
Uzalendo ni kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa lako, yaani serikali ndiyo imekulipa huo mshahara ila ikitaka ikate tena kidogo tu unalialia!

Hii ni sawa na Mungu anayekubariki na kila kitu ila roho yako inauma kumpa chochote kitu.
Basi Wasiajiri watu wa kulipwa mshahara, ili hela ibaki huko huko.
kuliko kumdanganya mtu unamlipa 60,000 alafu kwenye hiyo unamkata 15,000 kabla haumjamlipa, na baada ya kumlipa, unataka akupe tena Tsh 10,000 hii si dhulma?
 
Back
Top Bottom