Ahsante na Heri ya mwaka mpya kwako pia mkuu
nivea,
shumbimadelu,
Mkuu, Jinsia yako ni ipi?
UTI-yaani Urinary Tract Infection: Hutokea pale njia /au sehemu ya njia ya mkojo inaposhambuliwa na kusababisha muwasho, +/-kuharibu njia ya mkojo.Njia hii huanzia katika figo hadi mirija itoayo taka mwili(mkojo) nje iitwayo urethra.
Kuna aina tatu za UTI yaani;
1. Urethritis(kuwashwa kwa mirija itokayo katika kibofu hadi nje ya mwili)
2. Cystitis (Kibofu +/- mirija tajwa)
3. Pyelonephritis (Figo na njia tajwa)
Chronic Cystistis hasa tunaongelea kupata ugonjwa katika njia ya mkojo(UTI) ambapo tatizo huwa linajirudia angalau mara mbili ndani ya miezi sita, ukiwa umetibiwa au kubaki kwa muda mrefu-kuanzia/zaidi ya wiki mbili(recurrent or persistent).
Vijidudu(bacteria) huweza kushambulia katika njia ya mkojo,
Tatizo hili hupatikana kwa njia ya
-Kutumia vyoo vya jumuia(hasa vya kukaa)
-Njia zisizo salama za kufanya mapenzi.
-Baadhi ya watu huwa katika shida hii mf. Wajawazito, Wagonjwa wa Kisukari n.k.
- Watu wasiotumia maji kwa wingi.
Dalili:
Kujisikia maumivu ya tumbo (kama 'yanachoma')
-Kusikia maumivu wakati wa kukojoa(yanachoma)
-Homa
-Damu katika mkojo n.k
Kwa kuongea na daktari pamoja na kufanya vipimo, aina ya U.T. I hugundulika.
Matibabu hutegemea aina ya UTI mgonjwa aliyonayo.
Njia nzuri ya kujikinga:
-Tumia maji ya kunywa mengi/kwa wingi.
-Epuka mapenzi yasiyo salama.
-Kuwa msafi, epuka kutumia vyoo usivyojua usafi wake.
Iwapo mtu ana dalili hizo na pia kwa wajawazito na wagonjwa wa kisukari ni vyema kufika hospitali/kituo cha afya kwa ushauri na matibabu husika.