Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

kufanya tendo la ndoa kipindi mwenzi wako ametoka kumaliza dozi ya UTI na bila kutumia kinga kunaweza kusababisha kuambukizwa..
 
wee si na jana umeuliza?

Nenda kaombe ushauri 'live' kwa dokta, tena uende na mpenzio asije kuwa na gono akawa anakudanganya ana UTI
 
Wanajamvi poleni na week end. Nahitaji kufahamisha dawa nzuri ya uti kwa mtoto wa miaka 5. Natanguliza shukrani
 
Tafuta dawa inayo itwa cephelexin syp.
 
Habari zenu wanajamii.

Hii ni mara yangu ya kwanza kuja jukwaani.

Naomba mnisaidie jinsi ya kutibu chronic systitis mtanisamehe kama nimekosea kuandika.

Tatizo hili lilinipata baada ya kuumwa ugonjwa wa kaswende syphils ambayo ilinikaa mwilini kwa muda mrefu bila kujua nikidhani ni fungus maana shule niliyokuwa nasoma ilikuwa ni sehemu yenye joto. Nilikuwa natumia madawa ya fungus mpaka pale nlpoenda hospital ya mkoa ndio nikapimwa na kuonekana nina kaswende.

Niliitibu na kufanikiwa kupona bt ilikaa mwilini kwa muda wa miaka mitatu bila kujua. Sasa nilipokuwa chuoni nilikuwa nasikia kuna v2 vnachoma choma sehemu za siri. Nikapima std's hakukuwa na ugonjwa lkn nikawa naumwa.

Dkt wa hospital ya chuo aliniambia ni u.t.i so ninywe maji meng na alnipa dawa vitamin b.

Tatizo hl likawa linajrudia kila wakati nikienda hospital wananiambia ninywe maji meng 2 kumbe tatizo likawa chronic. Nikawa nikitumia dawa bado naumwa. Ikanibd niende kupga utra sound ikaonekana nina cystitis pia kibofu changu cha mkojo kimekuwa deformed. Nikachomwa sindano za powerself, wakanipa flagile na dawa nyngne inaitwa flucomox cjui km pia ntakuwa nmesahau pia kabla ya hapo nilienda hospital nyngne wakaniambia nina uti so wakanichoma sindano nyingne za mishipa kitu km gentamisine au km ckusahau na dawa za augementine bt tatzo bado.

Je nifanyaje? Je una madhara gani mwilini mwangu hususani ktk suala zima la uzazi?

Naomba mnishauri ndg zangu.
 
WEWE NII JINSIA GANI NDUGU YANGU Riwa COME THIS WAY KAKA MKUU hippocratessocrates HERI YA MWAKA MPYA WAKUU ZANGU MSAIDIENI
 
Last edited by a moderator:
Ahsante na Heri ya mwaka mpya kwako pia mkuu nivea,

shumbimadelu,

Mkuu, Jinsia yako ni ipi?

UTI-yaani Urinary Tract Infection: Hutokea pale njia /au sehemu ya njia ya mkojo inaposhambuliwa na kusababisha muwasho, +/-kuharibu njia ya mkojo.Njia hii huanzia katika figo hadi mirija itoayo taka mwili(mkojo) nje iitwayo urethra.

Kuna aina tatu za UTI yaani;
1. Urethritis(kuwashwa kwa mirija itokayo katika kibofu hadi nje ya mwili)
2. Cystitis (Kibofu +/- mirija tajwa)
3. Pyelonephritis (Figo na njia tajwa)


Chronic Cystistis hasa tunaongelea kupata ugonjwa katika njia ya mkojo(UTI) ambapo tatizo huwa linajirudia angalau mara mbili ndani ya miezi sita, ukiwa umetibiwa au kubaki kwa muda mrefu-kuanzia/zaidi ya wiki mbili(recurrent or persistent).

Vijidudu(bacteria) huweza kushambulia katika njia ya mkojo,

Tatizo hili hupatikana kwa njia ya
-Kutumia vyoo vya jumuia(hasa vya kukaa)
-Njia zisizo salama za kufanya mapenzi.
-Baadhi ya watu huwa katika shida hii mf. Wajawazito, Wagonjwa wa Kisukari n.k.
- Watu wasiotumia maji kwa wingi.

Dalili:
Kujisikia maumivu ya tumbo (kama 'yanachoma')
-Kusikia maumivu wakati wa kukojoa(yanachoma)
-Homa
-Damu katika mkojo n.k


Kwa kuongea na daktari pamoja na kufanya vipimo, aina ya U.T. I hugundulika.

Matibabu hutegemea aina ya UTI mgonjwa aliyonayo.

Njia nzuri ya kujikinga:
-Tumia maji ya kunywa mengi/kwa wingi.
-Epuka mapenzi yasiyo salama.
-Kuwa msafi, epuka kutumia vyoo usivyojua usafi wake.

Iwapo mtu ana dalili hizo na pia kwa wajawazito na wagonjwa wa kisukari ni vyema kufika hospitali/kituo cha afya kwa ushauri na matibabu husika.
 
Last edited by a moderator:
Wasiwasi wangu ni kuwa kwa jinsi nilivyofuatilia hitory ulivyoelezea,kwa dawa hizo ulizotumia ulitakiwa kuwa umeishapona,ila sina hakika kama ulikuwa ukizitumia kwa usahihi;hasa kumaliza dozi(sahihi).Kwa kweli kwa tatizo lako na dawa nyingi zinazotumika siku hizi hospitali unatakiwa kutumia kwa zaidi ya siku saba (14 days kwa matokeo mazuri zaidi),kama utaendelea kutumia kwa siku tano (au sindano moja moja)kama ambavyo naona mara nyingi zikitolewa,natarajia kukuona tena hapa kwa mara nyingine.

Anyway,jaribu kurudi tena hospitali ukaongee vizuri na daktari,mweleze mkasa mzima jinsi ilivyokuwa mpaka sasa.
 
wana JF, nina ujauzito wa wiki 24 lakini uti imekuwa ikijirudia mara kwa mara, na kila nikienda hospitali doctor aninipa antibiotics, namuonea huruma huyu kijacho wangu mwenzenu, nimefuatilia yote doctor ananiambia kuhusu kutawaza kutoka mbele kwenda nyuma, kutotumia sabuni wakati wa kunawa sehemu za siri na kunywa maji mengi lakini bado, kwa sasa natumia cranberry juice sina uhakika kama nitafanikiwa au la, msaada tafadhali
 
Tumia Azithromycin, Capsules USP 500g, kidonge 1 kila siku kwa siku 5. Hakikisha unatumia na huyo anaye ku-do kwa tiba ya uhakika.
 
Pole mdada. Angalia pia usafi wa choo chenu ikishindikana jaribu kumuona dokta kapona ana clinic kila siku pale Tumaini Hospital!
 
Tumia Azithromycin, Capsules USP 500g, kidonge 1 kila siku kwa siku 5. Hakikisha unatumia na huyo anaye ku-do kwa tiba ya uhakika.

Kwa majina ya dawa kama haya inawezekana kweli kubadili lugha ya kufundishia iwe kiswahili kama waheshimiwa wanavyopigia upatu?
 
Yes Dr Kapona atakusaidia, ila hayupo Tumaini tena, siku hizi ana clinic/hosptl yake kule Chanika.

Pole mdada. Angalia pia usafi wa choo chenu ikishindikana jaribu kumuona dokta kapona ana clinic kila siku pale Tumaini Hospital!
 
Yes Dr Kapona atakusaidia, ila hayupo Tumaini tena, siku hizi ana clinic/hosptl yake kule Chanika.

Asante kwa taarifa Nasema, long time since I last went at tumaini to consult him, kumbe ameacha clinic ya tumaini! Najua alikuwa na hiyo hospital yake lakini alikuwa anahudumia zaidi j/mosi. Thanks once again.
 
Last edited by a moderator:
Nimepima mkojo leo naambia kuna few pus cell. Dokta kasema ni UTI. Bado sijachukua dawa maana wao wakikuandikia inabidi ununue kwao.Ni dawa gani ambayo ni nzuri..
 
UNAWEZA KUDHIBITI U.T.I MWENYEWE..!

U.T.I ni ugonjwa sugu unaosumbua sana watu wengi hivi sasa, wakubwa kwa wadogo. U.T.I(Urinary tract Infection) ni ugonjwa unaoathiri njia ya mkojo na huweza kusababisha maumivu makali na unapojiimarisha mwilini kwa muda mrefu

huathiri figo pia. Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na mtu kusikia haja ya kukojoa kila wakati na kusisimka wakati wa kujisaidia, kusikia maumivu, kutoa mkojo mchafu na hata kutoa haja ndogo iliyochanganyika na damu.

Wataalamu wetu wa masuala ya tiba wanatueleza kuwa tatizo hili hujitokeza pale mlango wa njia ya haja ndogo inaposhambuliwa na bakteria ambao husambaa na wasipotibiwa mapema huenea hadi kwenye figo na athari zake ni mbaya.

UNAWEZA KUDHIBITI U.T.I KWA TIBA MBADALA


Kwa kawaida kila ungonjwa una tiba mbadala, siyo lazima kwenda hospitali. Unaweza kuudhibiti au kuponya ugonjwa huu kwa kunywa maji mengi (Ya Uvuguvgu) pamoja na juisi itokanayo na matunda halisi, iwapo utawahi kabla tatizo halijawa sugu.

Kwa maana nyingine, unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kuwa na mazoea ya kunywa maji
(Ya Uvuguvgu) ya kutosha kila siku. Ukinywa maji (Ya Uvuguvgu)ya kutosha yatakufanya uende haja ndogo kila mara na kwa njia hiyo wale bakteria watakuwa wakitoka

na hatimaye kuisha kabisa. Aidha, njia nyingine ya kuudhibitibi ugonjwa huu ni kunywa maji mengi
(Ya Uvuguvgu) au kwenda haja ndogo mara baada ya kufanya tendo la ndoa, kitendo hiki husaidia kuwaondoa mapema bakteria wote ulioambukizwa wakati wa kujamiiana na mwenzio.

Katika hali ya kawaida, ugonjwa wa UTI hutoweka ndani ya siku tatu mara baada ya kuanza kutumia tiba asili ya kunywa maji mengi
(Ya Uvuguvgu)na juisi ya matunda halisi, iwapo ugonjwa utaendelea kuwepo baada ya siku hizo, hiyo itakuwa na maana ugonjwa wako umeshakomaa na hivyo hauwezi kutibika kwa tiba hii ya nyumbani.

Katika hali kama hii, utakuwa huna njia nyingine isipokuwa kwenda hospitalini na kuonana na daktari ambaye atakufanyia uchunguzi na kukupatia dozi sahihi ambayo utatakiwa kuizingatia bila kukosa. Uamuzi huu ni muhimu hasa

kama unasikia maumivu makali ambayo yanaweza kuwa yanasababishwa na kuathirika kwa figo. Kwa kawaida tiba ya kidaktari kwa ugonjwa huu huhusisha matumizi ya dawa kali za ‘
antibiotics’, ambazo watu wengi wanazikimbia kutokana na athari zake za baadae (side effects). Lakini ni muhimu kufuata ushauri wa dokta na kumaliza dozi ili kuepuka uwezekano wa kurejea kwa ugonjwa, tena kwa kasi kubwa.

KUZUIA
Ili kujiepusha na ugonjwa huu, suala la usafi na kuwa na tabia ya kunywa maji ya kutosha ni jambo muhimu sana. Hakikisha unajisafisha vizuri mara baada ya kwenda haja na kubadilisha mara kwa mara nguo yako ya ndani, hasa kwa akina mama.

Vile vile usikae na haja ndogo kwa muda mrefu, nenda kajisaidie mara nyingi kadri unavyosikia kufanya hivyo. Kitu cha mwisho cha kuzingatia kwa mgonjwa wa UTI ni kupunguza unywaji wa pombe na vinywaji vingine vyenye sukari, kwa sababu sukari ni chakula cha bakteria hivyo kwa kuendelea kunywa kinywaji chenye sukari kutaifanya hali kuendelea kuwa mbaya. Ugonjwa huu ni rahisi kuepuka kwa mtu anayependa kunywa maji ya kutosha na kunywa juisi halisi kila siku.

DAYATI MUHIMU KUDHIBITI UTI

Katika kuudhibiti ugonjwa huu, pendelea kula vyakula ama vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha vitamini C ambayo utakipata kwenye matunda ya aina mbalimbali yakiwemo machungwa, mboga za majani n.k. Jiepushe na ulaji wa

vyakula vya ‘kupaki’ kama vile ‘chizi’, chokoleti na bidhaa nyingine zilizotengenezwa kutokana na maziwa. Pia jiepushe na ulaji wa vyakula vyenye viungo vingi kama pilau, epuka vyinywaji vyenye ‘caffeine’, kilevi na sigara na mwisho achana na vinywaji kama soda na vinavyofanana na soda.@
The secretary

How To Treat UTI With Home Natural Remedy


 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom