Kwanza niseme mleta maada ambaye amejipambanua kama mgonjwa ana kitu kisaikolojia tunaita self-consciousness(kujishitukia),coz anajua hadi maana ya ugonjwa husika but ameshindwa kujizuia kupata tena au kupata tiba,kifupi kwa miaka ya hivi karibuni watu wengi sana wamekua na tabia ya kusingizia U.T.I yale magonjwa mengi yanayohusiana na sexual transmitted,ikiwemo gonorea,coz its obvious leo hii ukitaja una ugonjwa wa zinaa ni aibu,tofauti na magonjwa kama U.T.I yana tamkika kirahisi mbele ya jamii,coz watu huamini ni mchafuko wa mkojo,kumbe sometimes unaweza ukawa umevagaa gonjwa la zinaa then unajitibu kisaikolojia kuwani U.T.I,now natoa mchango wangu:Kama walivyoeleza wadau wengine kua ni mchafuko wa mkojo,kwa wanaume sio mara nyingi kuupata lakini tatizo lipo sana kwa wanawake,chooni ni sehemu ambako bakteria hawa wanaweza kupatikana,lakini sio lazima choo ndio iwe source ya mtu kupata hayo maambukizi huko,coz sometimes hata kujaamiana kunaweza kusababisha hatari ya kuwapata bakteria hao toka kwa mtu ambae anao,na mara nyingi wanapatikana kwenye njia ya haja kubwa, so risk kubwa sometimes kwa wale mnaopenda kufanya kinyume na maumbile,cha msingi ni kuimarisha usafi wa choo,ukiwa haja kubwa wakati wa kujisafisha(kutawaza),jisafishe ukitokea mbele kwenda nyuma na sio nyuma kwenda mbele coz bakteria hao wanapatikana sehemu ya haja kubwa sana,na kuepuka ngono zembe,kumbuka wadudu hao wakiwa sugu sana huenea mpaka kwenye figo,so figo inaweza kupata madhara,dalili zake ni kupata haja ndogo mara kwa mara lakini kiasi cha mkojo kinakua kidogo sana,coz wale wadudu wanaathiri sensor za mkojo kwenye kibofu so sensor zinaasume kibofu kimejaa ndio maana mara kwa mara mtu hujisikia kwenda kukojoa,sometimes mkojo huambatana na maumivu ya kuchoma n.k