Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Nilisha umwaga huu ugonjwa ila niliwah mapema hospital na nashukuru nilipata matibabu
 
Asilimia kubwa ya Watanzania hawaujui vizuri ugonjwa wa UTI.Kumekwepo na maelezo kutoka kwa watu mbali mbali na wakati mwingine hata kwa wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa huu lakini bado watu wengi wanakanganyika na ukweli halisi.Leo nitajaribu kutoa maelezo walau kwa kina ili jamii iujue ugonjwa huu kinagaubaga.

Kwanza kabisa kirefu cha cha herufi UTI ni URINARY TRACT INFECTION ikimaanisha maambukizi kwenye njia ya mkojo.Msomaji anapaswa kujua njia ya mkojo ni ipi, inaanzia wapi na inaishia wapi.Kwa ujumla njia ya mkojo inaanzia kwenye mrija wa mkojo kwa mwanaume na mwanamke.Mrija huu unajulikana kama URETHRA na ukishapata maambukizi ugonjwa sehemu hii unaitwa URETHRITIS.

Njia ya mkojo inayofuata baada ya urethra ni BLADDER yaani kibofu.Kibofu kikipata maambukizi ugonjwa unajulikana kama CYCITITIS.Baada ya kibofu inafuata mirija miwili inayokwenda kwenye figo mbili.Mirija hii inaitwa URRETERS na ikishaambukizwa inajulikana kama URRETITIS.Na mwisho wa njia ya mkojo ni figo mbili yaani KIDNEYS na hizi figo zikishaambukizwa ugonjwa unajulikana kama NEPHRITIS.

Sasa basi ni lazima tujue ni vimelea wa aina gani wanaoleta ugonjwa wa UTI.Hapa nitajaribu kuonisha na kupanga vimelea katika makundi maalum.Vimelea vinavyojulikana ni kama ifutavyo:

1.BACTERIA eg Streptococci, Staphylococci, E.Coli, H.Influenza, Proteus sp.Pseudomonas etc.

2.VIRUSES eg Clamydia tracomatis

3.FUNGI eg Candida albicans

4.TRICHOMONIASIS 5.SCHISTOSOMIASIS (kichocho)

6. PARASITES 7.GONORRHEA (kisonono).

Watoto wadogo mara nyingi wanapata UTI kutokana na kutobadilisha nepi kwa wakati na hivyo unyevu wa mikojo na mavi huvuta vimelea na kuleta maambukizi.

Kwa watu wazima hasa wale wanaofanya ngono zembe wanapata magonjwa ya zinaaa kwa urahisi na hivyo wanakuwa tayari wana UTI.
Kuna fikra kubwa imejengeka miongoni mwa jamii kuwa UTI inaletwa kwa urahisi kwenye vyoo vya kuchangia.Dhana hii kwangu naweza kusema si sahihi hata kidogo kwa sababu wanaume wanakojoa kwa kuagiza mkojo kwa mbali kama risasi kwenye tundu la choo, sasa hao vimelea wanafuata mkondo wa mkojo kama unavyofanya umeme? Au wanaruka na kuja kuingia kwenye tundu la mkojo? Jibu ni hapana.

Kwa wanawake wao wanajisaidia kwa kuchuchamaa, wakimaliza hawatoezi au hawasoteshi nyeti zao kwenye sinki au shimo la choo na wala vimelea vya magonjwa vilivyomo chooni haviambukizi kamwe kwa ya mvuke.

Dalili za UTI zinaonekana kulingana na aina ya maambukizi.Lakini dalili kuu kwa watoto na watu wazima zinafanana nazo ni maumivu wakati wa kukojoa na pengine kutoka uchafu au usaha kwenye njia ya mkojo.
Kichocho dalili zake ni kukojoa damu na maumivu.

Complications za UTI nazo ziko nyingi na zinategemeana na aina ya maambukizi.Matibabu nayo yako mengi na tofauti kulingana na aina ya maambukizi.
 
uzi mzuri mkuu. ila klamidia sio virusi na sizani kama kuna virusi husababisha UTI. pia ni vema kutofautisha STDs na UTI japo vinashabihiana sana.
 
Baadhi ya STDs kama kisonono, fungi, non gonococcol urethritis(NGU), clamydia tracomatis and virus vinaleta UTI.STDS zingine kama Ukimwi, upele (scabies), lymphagranuloma inguinale venerium, chancroides, chancre na kaswende haziwezi kuleta UTI.Kwa hiyo sio kushabihiana bali ni kweli zinaleta UTI.
 
Kwa nyongeza virus wanaoweza kuleta UTI japo kwa uchache ni Herpes simplex virus na Adenovirus.
 
Habari wana javi! Ni KE, ninasumbuliwa na kuwashwa nyetin nkienda kupima napewa dawa za kupachika, nimetumia candistat sana pamoja na gynozol lakini sipon natokwa na majimaji yanaelekea kuwa kama kamasi rangi ya kijanjan.

Kwa upande Wa UTI kila nkipima mkojo naambiwa ni mchafu nimetumia cipro sana pamoja na kuchoma powersafe nkimaliza dose sioni mabadiliko nkikojoa mkojo unauma kwa mbali baada ya kumaliza, kuna kipindi huwa hali inatulia tena inaanza.

Najitahidi sana usafi Wa chini na kunywa maji mengi lkn wapi. Kwa anayefahamu Tiba zaidi ya hizo naomba anisaidie, Asante!
 
Soma Hapa

 
UTI chronic sometimes ni magonjwa ya zinaa, umeshapima magonjwa ya zinaa kupitia damu? napia Kama unae mume au mpenzi wote mtibiwe, mara nyingi mtu mwenye UTI akinywa antibiotic inaisha lakini wewe umeshakunywa antibiotic nyingi huponi means sio ya kawaida, jiongeze usingangane tuu ni UTI, dawa inayotibu UTI na fungus chronic ninayo ila hiyo UTI yako sijuhi maana hadi powersef imegoma?
 

Una ukimwi wewe..huwezi kupona
 
kuna dawa inatolewa na kampuni inayoitwa BF SUMA hiyo dawa inaitwa FEMICARE ni nzuri sana kwa tatizo lako hilo, itafute na uitumie nakuhakikishia itakuwa mwisho wa tatizo lako. utapopona uturudishie mrejesho
 
Pole Sana my dia,inabidi ukamuone specialist w wanawake acha kwenda hospital z kawaida,kwakuongezea wanawale wengi hawajui jins y kusafisha nyuchi ,wanaweka vidole ndan kwa adai wanasafisha kumbe wanaharibu,ukishapona jitahid kubadili mfumo mzima w kusafisha kwa bibi,usisondeke kidole utatoa bacteria wazuri wanaokulinda...google jinsi y kusafisha huko,halafu kunywa maji mengi Sana,mazoez usiache,Kula healthy food ili uipe nguvu immunity yako iweze kuoambana na magonjwa....pia kacheki STD's...
 

Hayo maji maji ya kijani yana harufu mbaya?
Je ukifanya mapenzi unaumia?
Je tumbo la chini linauma?
Unaweza kukuta unamaambukizi sugu ya kwenye viungo vya ndani vya uzazi.
Nenda hospitali ya kueleweka kwa uchunguzi wa kina.

Kama una recurrent vaginal candidiasis jaribu kuangalia yafuatayo.....
1.Pima HIV
2. Pima kisukari
3. Angalia aina ya nguo za ndani uvaazo , ni vizuri zikawa za Pamba tupu , uwe unavaa zikiwa kavu kabisa na ukifua uanike juani ...n:b ni vizuri ukawa nazo nyingi.
4. Pia angalia unavyoiosha papuchi yako kwa ndani , excessive douching na kutumia sabuni sana unaharibu normal flora ya vagina. Haifai kuosha sana papuchi kwa ndani.
Pole sana.
 
wewe uliesema anaukimwi (hiv) nimekustai sana,kama ushauri wa kujenga hukuwa nao ungekaa kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…