Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Pole mwaya, jitahidi kufuata masharti ya daktari.
Inawezekana mwenzio naye ana maambukizi kwa hiyo ukijitibu mwenyewe ni kazi ya bure.
 
Kigogo siyo hivyo bhana, kwani ni nani kakuambia ukimwi unauwa miaka hii,
utakufa Kigogo na mapresha na masukari wa ukimwi wapo wanadunda tu,
mtake radhi mdada wa watu.
Hakuna majibu hayo sio sahihi..wewe lazima una ukimwi maana hizo dalili ni za kimwi
 
Last edited by a moderator:
nenda kachome sindano za detromaizng, umalize doz, kama upo kwenye mahusiano sitisha huduma na utumie doz, baada ya hapo kapime iyo UTI,
 
Nina rafiki yangu. Karibu mwaka sasa anasumbuka na ugonjwa ambao alielezwa ni uti.

DAlili:
1. Maumivu makali sehemu za siri, tumbo na mgongo. Mkojo unauma sana na ni wa njano/mwekundu.

MATibabu :
2. Ametibiwa hospitali 3 tofauti wakamwambia ni UTI baada ya vipimo. Alikwenda kwenye dispensary moja miezi michache iliyopita wao wakamwambia ni fungus.

Matokeo:
3. Tangu aanze kutumia dawa kama alivyoelekezwa ugonjwa umekuwa ukitulia na kurudi. Hivi Jana hali imerudi kama mwanzo.

Ombi:
4. Ushauri unahitajika juu ya wapi hasa tiba sahihi inaweza kupatikana. Asanteni wakuu
 
Mgonjwa ana jinsia gani?umri gani?anatumia catheter?
Anahitaji long term prophylaxis treatment na either nitrofurantion au trimetoprim/sulfamethazole..Hizo infection zinazojirudia ni kwasababu ya resistence inayojitokeza baada ya kujaribu antibiotics tofauti.Bacteria wanatengeza survival mechanisims na hio inaweza kusababishwa na kutokukamilisha antibiotic cures n.k.....
 
Nina rafiki yangu. Karibu mwaka sasa anasumbuka na ugonjwa ambao alielezwa ni uti.

DAlili:
1. Maumivu makali sehemu za siri, tumbo na mgongo. Mkojo unauma sana na ni wa njano/mwekundu.

MATibabu :
2. Ametibiwa hospitali 3 tofauti wakamwambia ni UTI baada ya vipimo. Alikwenda kwenye dispensary moja miezi michache iliyopita wao wakamwambia ni fungus.

Matokeo:
3. Tangu aanze kutumia dawa kama alivyoelekezwa ugonjwa umekuwa ukitulia na kurudi. Hivi Jana hali imerudi kama mwanzo.

Ombi:
4. Ushauri unahitajika juu ya wapi hasa tiba sahihi inaweza kupatikana. Asanteni wakuu

MAAMBUKIZI YA NJIA YA MKOJO (URINARY TRACT INFECTIONS (UTI)

attachment.php

Neno U.T.I si geni masikioni mwa wengi, kwani ni wengi leo utawasikia "naumwa U.T.I". Japo si wote hulitumia kisahihi. Wengine wana tatizo ambalo ni tofauti na U.T.I, lakini anaweza akaenda hata duka la dawa na kuomba apatiwe dawa za U.T.I. Leo nimeona tubadilishane elimu juu ya hili tatizo, angalau kila mmoja awe na uelewa U.T.I ni nini hasa, inasababisha na nini, na ni jinsi gani anaweza kujikinga.

U.T.Is, ni kifupisho cha Urinary Tract Infections, ambayo kwa lugha yetu ni maambukizi ya njia ya mkojo. Kama linavyojieleza, kwamba maambukizi ni lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo ndipo tunaita ni U.T.I, na si pengine popote. Una uchafu unatoka ukeni, hiyo ni kitu kingine tofauti nk. Tunapozungumzia njia ya mkojo, ni kutoka eneo la nje hadi kwenye kibofu, na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.

Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo(ikihusisha na figo pia), inaitwa Lower Urinary Tract Infect. Na ikihusisha eneo la juu ya kibofu, inaitwa Upper Urinary Tract Infection.

Tatizo hili huwapata wote, wanaume na wanawake. Lakini huwapata zaidi wanawake kutokana na tofauti za kimaumbile. Hii ni kwa sababu kuu mbili, i)njia ya haja ndogo ya mwanamke iko jirani zaidi na njia ya haja kubwa ambapo vijidudu vingi visababishao U.T.I ndipo vinapoishi, ii) mrija wa mkojo (urethra) wa mwanamke ni mfupi ukilinganisha na wa mwanaume, hivyo kufanya iwe rahisi kwa maambukizi kufika kwenye kibofu kwa mwanamke kuliko kwa mwanaume.
Visababishi

Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bacteria ambao makazi yao ya kawaida utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa, mfano Escherichia coli na wengineo. Pia, linaweza likasababisha na ‘fungus' na visababishi vingine, japo ni mara chache sana.

Vihatarishi na Njia ya Maambukizi

a)Kwa wanawake

• Kujamiiana –hii huweza kuamisha bacteria walio kwenye uume moja kwa moja, ama watokanao na maambukizi ya ukeni kuingia moja kwa moja njia ya mkojo
• Kuchezea ama kuchezewa na mikono michafu maeneo ya uke kunaweza kusababisha maambukizi
• Njia mbaya ya kujisafisha baada ya haja kubwa au ndogo inaweza kuhamisha bacteria walio ktk njia ya haja kubwa na kuingia njia ya mkojo
• Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambao huua bacteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bacteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi
Vifuatavyo pia vinaweza vikachangia
• Ujauzito –mara nyingi hushusha kinga ya mwili ya mjamzito
• Upungufu wa homon ya ya kike Oestrogen husababisha bacteria wasababishao U.T.I kuzaliana kirahisi

b)Kwa wanaume

• Matatizo ya tezi ya kiume(prostate) mabapo husababisha mrija wa mkojo kuziba, ama kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bacteria kujenga makazi
• Kutotahiriwa, ambapo nyama ya mbele inaweza kuhifadhi bacteria wasababishao U.T.I
• Kujamiiana kinyume cha maumbile huingiza kirahisi bacteria walio njia ya haja kubwa kwenye njia ya mkojo
• Kujamiiana bila kinga na mwanamke ambaye ana maambukizi ukeni
• Kuwa na VVU ambapo hupunguza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi

c)Kwa wote
• Kutokunywa maji na vinyaji kwa wingi –kunywa maji mengi husababisha mkojo kuzalishwa kwa wingi, na kukojoa mara kwa mara na hivyo kusafisha njia ya mkojo
• Kuwekewa mirija inayosaidia kutoa mkojo nje inaweza pia kukaribisha maambukizi
• Matatizo ya figo na mengine kwenye njia ya mkojo yanayoweza kuziba njia ya mkojo
• Kisukari ambapo hudhoosha kinga ya mwili na pia kuharibu mfumo wa figo wa uchujaji

Dalili za U.T.I
a) Kwa eneo la chini la njia ya mkojo
i. Hali ya kujisikia kutaka kukojoa muda wote
ii. Maumivu, au hali ya kujisikia kuchoma choma wakati wa kukojoa
iii. Kukojoa mara kwa mara na mara zote mkojo ni mdogo
iv. Mkojo unaweza kuonekana una ukungu, na mara nyingine unatoa harufu kali
v. Maumivu ya nyonga kwa wanawake
vi. Maumivu ya rektamu(rectum) kwa wanaume
vii. Na mara nyingine damu kwenye mkojo

b) Kwa eneo la juu la njia ya mkojo
i. Maumivu ya tumbo(hasa eneo la juu kwa pembeni –chini ya mbavu)
ii. Homa kali
iii. Kutetemeka na kujihisi baridi
iv. Kichefuchefu na /au kutapika

Vipimo na matibabu

Mara nyingi kipimo cha mkojo kinaweza kuonyesha tatizo.
Matibabu ni antibiotic baada ya daktari kubaini tatizo

Madhala yatokanayo na U.T.I isipopata tiba sahihi

• Inaweza ikasababisha maambukizi makubwa ya figo(pyenephritis) ambayo yanaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa figo na hivyo kutishia maisha

• Kwa wajawazito inaweza kuhatarisha maisha ya wote mama, na motto aliye tumboni

• Bakteria wanaweza kuingia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhala mengine

• Inaweza kusababisha shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi mbovu wa figo

Tiba mbadala nyumbani kabla ya kumwona daktari
Unaweza kutibu, ama kupunguza tatizo nyumbani kabla ya kumwona daktari pale uonapo dalili ya awali ya U.T.I, ambayo ni maumivu na kuchomachoma wakaji wa kukojoa. Fanya yafuatayo

i. Kunywa maji mengi hasa saa 24 za kwanza baada ya kuona dalili. Hii itasaidia kuzalisha mkojo kwa wingi na kusafisha njia ya mkojo
ii. Kojoa mara kwa mara na hakikisha ni hadi mkojo unaisha ili kibofu kiwe tupu
iii. Kwa maumivu ya mlango wa mkojo, oga na kuosha kwa maji ya moto, kutapunguza maumivu

Njia za Kujikinga na U.T.I

Kunywa maji na vinywaji kwa wingi kila siku. Hii itakusaidia ukojoe mara kwa mara na kutoruhusu bacteria kujenga makazi kwenye njia ya mkojo
Kojoa kila ujisikiapo mkojo na usiubane kwa muda mrefu

Kwa wanawake

Nenda ukakojoe mara tu umalizapo tendo la kujamiiana. Hii itasaidia kutoruhusu bacteria kuingia na kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.

Badili pedi mara kwa mara uwapo hedhini

Epuka kujisafisha ukeni na maji yarukayo kwa kasi, pia epuka kupilizia marashi ukeni, ama kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu. Hizo huua bacteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bacteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi
Ujisafishapo baada ya kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bacteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo

Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauliana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni kuwasaidia kujikinga na maambukizi

Kwa wanaume
Kuhakikisha maeneo ya ncha ya uume ni masafi mara zote, hasa ikiwa hujatahiriwa kuepusha kujihifadhi na kuzaliana kwa vijidudu visababishao maradhi.
Kondom wakati wa kujamiiana nayo ni kinga nzuri

Asanteni kwa kutenga muda wenu kupata elimu hii

Mgonjwa Mpeleke Hospitali akatibiwe asipo pona nitafute mimi Dawa ya kutibu Maradhi ya UTI ninayo kunipata mimi bonyeza hapa
.
Mawasiliano
 
Attachments

  • UrinaryTractInfection.jpg
    UrinaryTractInfection.jpg
    40.7 KB · Views: 1,777
Nina rafiki yangu. Karibu mwaka sasa anasumbuka na ugonjwa ambao alielezwa ni uti.

DAlili:
1. Maumivu makali sehemu za siri, tumbo na mgongo. Mkojo unauma sana na ni wa njano/mwekundu.

MATibabu :
2. Ametibiwa hospitali 3 tofauti wakamwambia ni UTI baada ya vipimo. Alikwenda kwenye dispensary moja miezi michache iliyopita wao wakamwambia ni fungus.

Matokeo:
3. Tangu aanze kutumia dawa kama alivyoelekezwa ugonjwa umekuwa ukitulia na kurudi. Hivi Jana hali imerudi kama mwanzo.

Ombi:
4. Ushauri unahitajika juu ya wapi hasa tiba sahihi inaweza kupatikana. Asanteni wakuu

Umeeleza vema.. lakini hujasema dawa gani ametumia mpaka sasa na kwa utaratibu upi..?
 
Muhimu sana kutazama mazingira unayoishi, pengine maambukizi yanatoka kwa partner wako unaeishi nae, au choo / bafu unachotumia kama cha kazini au nyumbani.

Kama hali inaendelea na upo tayari kutumia dawa za kiasili wasiliana nami ntakupataia kwa bei nafuu. Mimi si mganga wa kienyeji isipokuwa kuna dawa za asili nizijuazo, mojawapo ni hiyo ya UTI.

Pitia hapa kwa namba za simu na mawasiliano mengine: https://www.jamiiforums.com/matanga...ural-unaolainisha-ngozi-sasa-unapatikana.html
 
Habari waungwana, ninapenda kuuliza kua ugonjwa wa U.T.I. unaweza kumpelekea mtu kupungua nguvu za kiume? Na kama ni hivyo nifanye nini kutatua tatizo hilo?

Asanteni sana, ushauri wenu ni muhimu sana kwangu.
 
Pole! Mimi nikusaidie upande wa ushauri tu maana mimi si dr. Umeenda hospital. Nenda kapime ujue ni UTI kweli? Kama ndio utumie dawa ulizoandikiwa na uzitimie kwa uaminifu.
Kama tatizo linaendelea nenda hospital wakufanyie culture ili ujue ni aina gani ya mdudu wa UTI uliyenaye na anatibiwa na dawa ipi. Ukishajua hayo UTI kwao utapona vizuri. Lakini pia ukishapona kaa mbali na vitu vinavyokusababishia UTI mfano anika nguo za ndani direct juani zikauke vizuri. Kama una mwenza hakikisha wote mnapata tiba. Ishi mazingira masafi wakati wote.
 
Habar waungwana, ninapenda kuuliza kua ugonjwa wa u.t.i uanweza kumpelekea mtu kupungua nguvu za kiume?
na kama ni hivyo nifanye nn kutatua tatizo hilo?

ahsanten sn, ushauri wenu n muhim sn kwangu.

MAAMBUKIZI YA NJIA YA MKOJO (URINARY TRACT INFECTIONS -UTIs)

Neno U.T.I si geni masikioni mwa wengi, kwani ni wengi leo utawasikia "naumwa U.T.I". Japo si wote hulitumia kisahihi. Wengine wana tatizo ambalo ni tofauti na U.T.I, lakini anaweza akaenda hata duka la dawa na kuomba apatiwe dawa za U.T.I. Leo nimeona tubadilishane elimu juu ya hili tatizo, angalau kila mmoja awe na uelewa U.T.I ni nini hasa, inasababisha na nini, na ni jinsi gani anaweza kujikinga.

U.T.Is, ni kifupisho cha Urinary Tract Infections, ambayo kwa lugha yetu ni maambukizi ya njia ya mkojo. Kama linavyojieleza, kwamba maambukizi ni lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo ndipo tunaita ni U.T.I, na si pengine popote. Una uchafu unatoka ukeni, hiyo ni kitu kingine tofauti nk. Tunapozungumzia njia ya mkojo, ni kutoka eneo la nje hadi kwenye kibofu, na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.

Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo(ikihusisha na figo pia), inaitwa Lower Urinary Tract Infect. Na ikihusisha eneo la juu ya kibofu, inaitwa Upper Urinary Tract Infection.

Tatizo hili huwapata wote, wanaume na wanawake. Lakini huwapata zaidi wanawake kutokana na tofauti za kimaumbile. Hii ni kwa sababu kuu mbili, i)njia ya haja ndogo ya mwanamke iko jirani zaidi na njia ya haja kubwa ambapo vijidudu vingi visababishao U.T.I ndipo vinapoishi, ii) mrija wa mkojo (urethra) wa mwanamke ni mfupi ukilinganisha na wa mwanaume, hivyo kufanya iwe rahisi kwa maambukizi kufika kwenye kibofu kwa mwanamke kuliko kwa mwanaume.
Visababishi

Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bacteria ambao makazi yao ya kawaida utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa, mfano Escherichia coli na wengineo. Pia, linaweza likasababisha na ‘fungus' na visababishi vingine, japo ni mara chache sana.

Vihatarishi na Njia ya Maambukizi

a)Kwa wanawake
• Kujamiiana –hii huweza kuamisha bacteria walio kwenye uume moja kwa moja, ama watokanao na maambukizi ya ukeni kuingia moja kwa moja njia ya mkojo
• Kuchezea ama kuchezewa na mikono michafu maeneo ya uke kunaweza kusababisha maambukizi
• Njia mbaya ya kujisafisha baada ya haja kubwa au ndogo inaweza kuhamisha bacteria walio ktk njia ya haja kubwa na kuingia njia ya mkojo
• Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambao huua bacteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bacteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi
Vifuatavyo pia vinaweza vikachangia
• Ujauzito –mara nyingi hushusha kinga ya mwili ya mjamzito
• Upungufu wa homon ya ya kike Oestrogen husababisha bacteria wasababishao U.T.I kuzaliana kirahisi

b)Kwa wanaume
• Matatizo ya tezi ya kiume(prostate) mabapo husababisha mrija wa mkojo kuziba, ama kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bacteria kujenga makazi
• Kutotahiriwa, ambapo nyama ya mbele inaweza kuhifadhi bacteria wasababishao U.T.I
• Kujamiiana kinyume cha maumbile huingiza kirahisi bacteria walio njia ya haja kubwa kwenye njia ya mkojo
• Kujamiiana bila kinga na mwanamke ambaye ana maambukizi ukeni
• Kuwa na VVU ambapo hupunguza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi

c)Kwa wote
• Kutokunywa maji na vinyaji kwa wingi –kunywa maji mengi husababisha mkojo kuzalishwa kwa wingi, na kukojoa mara kwa mara na hivyo kusafisha njia ya mkojo
• Kuwekewa mirija inayosaidia kutoa mkojo nje inaweza pia kukaribisha maambukizi
• Matatizo ya figo na mengine kwenye njia ya mkojo yanayoweza kuziba njia ya mkojo
• Kisukari ambapo hudhoosha kinga ya mwili na pia kuharibu mfumo wa figo wa uchujaji

Dalili za U.T.I
a) Kwa eneo la chini la njia ya mkojo
i. Hali ya kujisikia kutaka kukojoa muda wote
ii. Maumivu, au hali ya kujisikia kuchoma choma wakati wa kukojoa
iii. Kukojoa mara kwa mara na mara zote mkojo ni mdogo
iv. Mkojo unaweza kuonekana una ukungu, na mara nyingine unatoa harufu kali
v. Maumivu ya nyonga kwa wanawake
vi. Maumivu ya rektamu(rectum) kwa wanaume
vii. Na mara nyingine damu kwenye mkojo

b) Kwa eneo la juu la njia ya mkojo
i. Maumivu ya tumbo(hasa eneo la juu kwa pembeni –chini ya mbavu)
ii. Homa kali
iii. Kutetemeka na kujihisi baridi
iv. Kichefuchefu na /au kutapika

Vipimo na matibabu

Mara nyingi kipimo cha mkojo kinaweza kuonyesha tatizo.
Matibabu ni antibiotic baada ya daktari kubaini tatizo

Madhala yatokanayo na U.T.I isipopata tiba sahihi
• Inaweza ikasababisha maambukizi makubwa ya figo(pyenephritis) ambayo yanaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa figo na hivyo kutishia maisha
• Kwa wajawazito inaweza kuhatarisha maisha ya wote mama, na motto aliye tumboni
• Bakteria wanaweza kuingia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhala mengine
• Inaweza kusababisha shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi mbovu wa figo

Tiba mbadala nyumbani kabla ya kumwona daktari
Unaweza kutibu, ama kupunguza tatizo nyumbani kabla ya kumwona daktari pale uonapo dalili ya awali ya U.T.I, ambayo ni maumivu na kuchomachoma wakaji wa kukojoa. Fanya yafuatayo
i. Kunywa maji mengi hasa saa 24 za kwanza baada ya kuona dalili. Hii itasaidia kuzalisha mkojo kwa wingi na kusafisha njia ya mkojo
ii. Kojoa mara kwa mara na hakikisha ni hadi mkojo unaisha ili kibofu kiwe tupu
iii. Kwa maumivu ya mlango wa mkojo, oga na kuosha kwa maji ya moto, kutapunguza maumivu

Njia za Kujikinga na U.T.I
Kunywa maji na vinywaji kwa wingi kila siku. Hii itakusaidia ukojoe mara kwa mara na kutoruhusu bacteria kujenga makazi kwenye njia ya mkojo
Kojoa kila ujisikiapo mkojo na usiubane kwa muda mrefu

Kwa wanawake

Nenda ukakojoe mara tu umalizapo tendo la kujamiiana. Hii itasaidia kutoruhusu bacteria kuingia na kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.
Badili pedi mara kwa mara uwapo hedhini

Epuka kujisafisha ukeni na maji yarukayo kwa kasi, pia epuka kupilizia marashi ukeni, ama kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu. Hizo huua bacteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bacteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi
Ujisafishapo baada ya kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bacteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo

Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauliana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni kuwasaidia kujikinga na maambukizi

Kwa wanaume

Kuhakikisha maeneo ya ncha ya uume ni masafi mara zote, hasa ikiwa hujatahiriwa kuepusha kujihifadhi na kuzaliana kwa vijidudu visababishao maradhi.
Kondom wakati wa kujamiiana nayo ni kinga nzuri

Asanteni kwa kutenga muda wenu kupata elimu hii

Ukikosa Dawa ya kujitibia Maradhi ya UTI nitafute mimi Dawa ninayo nitakupa na utapona kwa gharama zako ukiweza kunitafuta bonyeza hapa.
Mawasiliano
 
Muhimu sana kutazama mazingira unayoishi, pengine maambukizi yanatoka kwa partner wako unaeishi nae, au choo / bafu unachotumia kama cha kazini au nyumbani.

Kama hali inaendelea na upo tayari kutumia dawa za kiasili wasiliana nami ntakupataia kwa bei nafuu. Mimi si mganga wa kienyeji isipokuwa kuna dawa za asili nizijuazo, mojawapo ni hiyo ya UTI.

Pitia hapa kwa namba za simu na mawasiliano mengine: https://www.jamiiforums.com/matanga...ural-unaolainisha-ngozi-sasa-unapatikana.html

Wewe unaonekana una kiburi sana.kwanini ukipigiwa cm hupokei na umetoa namba mwenyewe? Mbabaishaji
 
Back
Top Bottom