Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Nilisha umwaga huu ugonjwa ila niliwah mapema hospital na nashukuru nilipata matibabu
 
Asilimia kubwa ya Watanzania hawaujui vizuri ugonjwa wa UTI.Kumekwepo na maelezo kutoka kwa watu mbali mbali na wakati mwingine hata kwa wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa huu lakini bado watu wengi wanakanganyika na ukweli halisi.Leo nitajaribu kutoa maelezo walau kwa kina ili jamii iujue ugonjwa huu kinagaubaga.

Kwanza kabisa kirefu cha cha herufi UTI ni URINARY TRACT INFECTION ikimaanisha maambukizi kwenye njia ya mkojo.Msomaji anapaswa kujua njia ya mkojo ni ipi, inaanzia wapi na inaishia wapi.Kwa ujumla njia ya mkojo inaanzia kwenye mrija wa mkojo kwa mwanaume na mwanamke.Mrija huu unajulikana kama URETHRA na ukishapata maambukizi ugonjwa sehemu hii unaitwa URETHRITIS.

Njia ya mkojo inayofuata baada ya urethra ni BLADDER yaani kibofu.Kibofu kikipata maambukizi ugonjwa unajulikana kama CYCITITIS.Baada ya kibofu inafuata mirija miwili inayokwenda kwenye figo mbili.Mirija hii inaitwa URRETERS na ikishaambukizwa inajulikana kama URRETITIS.Na mwisho wa njia ya mkojo ni figo mbili yaani KIDNEYS na hizi figo zikishaambukizwa ugonjwa unajulikana kama NEPHRITIS.

Sasa basi ni lazima tujue ni vimelea wa aina gani wanaoleta ugonjwa wa UTI.Hapa nitajaribu kuonisha na kupanga vimelea katika makundi maalum.Vimelea vinavyojulikana ni kama ifutavyo:

1.BACTERIA eg Streptococci, Staphylococci, E.Coli, H.Influenza, Proteus sp.Pseudomonas etc.

2.VIRUSES eg Clamydia tracomatis

3.FUNGI eg Candida albicans

4.TRICHOMONIASIS 5.SCHISTOSOMIASIS (kichocho)

6. PARASITES 7.GONORRHEA (kisonono).

Watoto wadogo mara nyingi wanapata UTI kutokana na kutobadilisha nepi kwa wakati na hivyo unyevu wa mikojo na mavi huvuta vimelea na kuleta maambukizi.

Kwa watu wazima hasa wale wanaofanya ngono zembe wanapata magonjwa ya zinaaa kwa urahisi na hivyo wanakuwa tayari wana UTI.
Kuna fikra kubwa imejengeka miongoni mwa jamii kuwa UTI inaletwa kwa urahisi kwenye vyoo vya kuchangia.Dhana hii kwangu naweza kusema si sahihi hata kidogo kwa sababu wanaume wanakojoa kwa kuagiza mkojo kwa mbali kama risasi kwenye tundu la choo, sasa hao vimelea wanafuata mkondo wa mkojo kama unavyofanya umeme? Au wanaruka na kuja kuingia kwenye tundu la mkojo? Jibu ni hapana.

Kwa wanawake wao wanajisaidia kwa kuchuchamaa, wakimaliza hawatoezi au hawasoteshi nyeti zao kwenye sinki au shimo la choo na wala vimelea vya magonjwa vilivyomo chooni haviambukizi kamwe kwa ya mvuke.

Dalili za UTI zinaonekana kulingana na aina ya maambukizi.Lakini dalili kuu kwa watoto na watu wazima zinafanana nazo ni maumivu wakati wa kukojoa na pengine kutoka uchafu au usaha kwenye njia ya mkojo.
Kichocho dalili zake ni kukojoa damu na maumivu.

Complications za UTI nazo ziko nyingi na zinategemeana na aina ya maambukizi.Matibabu nayo yako mengi na tofauti kulingana na aina ya maambukizi.
 
uzi mzuri mkuu. ila klamidia sio virusi na sizani kama kuna virusi husababisha UTI. pia ni vema kutofautisha STDs na UTI japo vinashabihiana sana.
 
Baadhi ya STDs kama kisonono, fungi, non gonococcol urethritis(NGU), clamydia tracomatis and virus vinaleta UTI.STDS zingine kama Ukimwi, upele (scabies), lymphagranuloma inguinale venerium, chancroides, chancre na kaswende haziwezi kuleta UTI.Kwa hiyo sio kushabihiana bali ni kweli zinaleta UTI.
 
Kwa nyongeza virus wanaoweza kuleta UTI japo kwa uchache ni Herpes simplex virus na Adenovirus.
 
Habari wana javi! Ni KE, ninasumbuliwa na kuwashwa nyetin nkienda kupima napewa dawa za kupachika, nimetumia candistat sana pamoja na gynozol lakini sipon natokwa na majimaji yanaelekea kuwa kama kamasi rangi ya kijanjan.

Kwa upande Wa UTI kila nkipima mkojo naambiwa ni mchafu nimetumia cipro sana pamoja na kuchoma powersafe nkimaliza dose sioni mabadiliko nkikojoa mkojo unauma kwa mbali baada ya kumaliza, kuna kipindi huwa hali inatulia tena inaanza.

Najitahidi sana usafi Wa chini na kunywa maji mengi lkn wapi. Kwa anayefahamu Tiba zaidi ya hizo naomba anisaidie, Asante!
 
Soma Hapa

U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza: 'Urinary tract infections', ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo. Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na ugonjwa huu. Zaidi ya wanawake milioni 8 wanauguwa ugonjwa huu kila mwaka nchini Marekani peke yake.

Kama ulishawahi kupatwa na U.T.I basi hutazisahau dalili zake ambazo mara nyingi huanza kwa hitaji la ghafla la kutaka kwenda kupata haja ndogo na unapofika bafuni mara baada ya kutoa kiasi kidogo cha mkojo utaanza kusikia maumivu kwenye kibofu cha mkojo na hata kwenye urethra. Katika dalili kubwa zaidi utaishia kujisikia homa, baridi kali, maumivu nyuma ya mgongo na hata damu kutoka pamoja na mkojo.

Habari njema ni kuwa kuna dawa mbadala za nyumbani unazoweza kuzitumia na ukajikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu. Endelea kusoma.

Kinachosababisha U.T.I:

  • Kisukari
  • Maumivu ya mishipa
  • Ajari katika uti wa mgongo
  • Ushoga (kwa wanaume)
  • Usafi duni
  • Upungufu wa maji mwilini
  • Kushikilia mkojo muda mrefu
  • Kurithi
  • Kuongezeka ukubwa kwa kibofu cha mkojo au mawe kwenye figo.

Baadhi ya dalili za kawaida na zisizo za kawaida za U.T.I

  • Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa
  • Maumivu kwenye kibofu cha mkojo
  • Mikojo kukutoka pasipo kutaka
  • Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa
  • Kukojoa damu
  • Harufu nzito au mbaya ya mkojo
  • Homa
  • Kusikia baridi
  • Kutokujisikia vizuri
  • Kujisikia uchovu

Dawa mbadala 7 zinazotibu U.T.I


1. Baking Soda
Baking Soda

U.T.I ambayo imedumu zaidi ya siku mbili inahitaji kuripotiwa kwa daktari. U.T.I isiyotibiwa mapema inaweza kuepelekea matatizo zaidi kwenye figo na kuleta matatizo mengine makubwa zaidi.

Ili kuzuia U.T.I isijiimarishe zaidi jaribu kuongeza kijiko kimoja cha chai cha baking soda kwenye glasi ya maji na unywe na hivyo kusaidia kupunguza makali au kuendela kwa maambukizi ya U.T.I. Baking soda itapunguza hali ya uasidi katika mkojo wako na kupelekea nafuu haraka.

Baking soda ni ile kinamama wanatumia wakati wanapika maandazi. Siri iliyopo hapa ni huko kupunguza asidi kwenye mkojo na mwilini kwa ujumla na hivyo kuongeza hali ya ualikalini mwilini.


2. Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries):



Zabibu nyeusi



Zabibu nyekundu



Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries) ambazo zote zinatoka katika mti wa aina moja na zina sifa sawa ya kudhibiti bakteria. Katika utafiti mmoja, juisi ya zabibu nyeusi iligundulika kuwa na uwezo wa kudhibiti U.T.I. Pendelea kutumia juisi ya matunda haya glasi 2 mpaka 4 kwa siku mara kwa mara ili kujikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu.


-3. Nanasi
Nanasi



Kula Nanasi mara kwa mara ni mbinu nzuri kabisa katika kudhibiti maambukizi katika njia ya mkojo. Kwenye nanasi kuna kimeng'enya mhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama 'Bromelain'. Katika utafiti mmoja, watu wenye U.T.I waliopewa hii bromelain sambamba na antibiotic zao walifanikiwa kuondokewa na maambukizi ya U.T.I. Kula vipande vitatu mpaka vitano vya nanasi kila siku kutakuweka mbali na ugonjwa huu.

4. Maji

maji




Kama unasumbuliwa na U.T.I au inakutokea unapatwa na ugonjwa huu mara kwa mara, basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku walau glasi 8 mpaka 10 kwa siku, maji yenye joto la kawaida yaani yale ambayo hayajawekwa kwenye friji.

Mara nyingi mtu mwenye U.T.I huwa ana upungufu wa maji mwilini na ikiwa utauchunguza mkojo wake utaona ni wa rangi ya njano. Kunywa maji ya kutosha kila siku na kama matokeo yake bakteria wote wanaokupelekea upatwe na U.T.I watalazimishwa kutoka nje ya mwili kupitia mkojo utakaoupata kutokana na kukojoa mara kwa mara kama matokeo ya kunywa maji mengi

Na utaona baada ya siku 4 mpaka 7 hata rangi ya mkojo inabadilika na kuwa mweupe kabisa. Kujifunza zaidi kuhusu tiba kwa kutumia maji bonyeza


5. Vitamini C

Vitamini C husaidia kuzuia uzarishwaji wa bakteria wabaya mwilini



Baadhi ya madaktari wanashauri mtu atumie mpaka mg 5,000 za vitamin C kwa siku kwa mgonjwa anayesumbuliwa na maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo.

Vitamini C hukifanya kibofu cha mkojo kubaki na afya kutokana na asidi yake safi kwenye mkojo kitendo ambacho ni mhimu katika kuwazuia bakteria wabaya kufanya makazi kwenye kibofu cha mkojo. Ukiacha machungwa, Vitamini C inapatikana pia kwa wingi katika juisi ya ubuyu na kwenye mlonge. Hakikisha unapata kiasi cha kutosha cha Vitamini C kila siku ili kujikinga na hata kujitibu na U.T.I.


6. Kitunguu swaumu:

Kitunguu swaumu



Kitunguu swaumu ni mojawapo ya tiba mbadala ya nguvu katika kutibu maambukizi kwenye njia ya mkojo. Ni dawa nzuri dhidi ya bacteria na virusi na hivyo moja kwa moja kuwa mhimu katika kutibu U.T.I ya jumla na hata ile ya kibofu cha mkojo.

Kwakuwa moja ya kazi ya kitunguu swaumu ni kusafisha mkojo basi ni dhahiri inafaa sana katika kutibu U.T.I. Namna ya kukitumia; Chukuwa kitunguu swaumu kimoja na ukigawe mara 2, menya nusu yake (punje 10 au 15), menya punje moja baada ya nyingine na kisha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala na mapema uamkapo asubuhi kwa siku 7.


7. Limau/ndimu:

Limau/Ndimu

Changanya kijiko kikubwa kimoja cha juisi ya limau au ndimu kwenye maji robo lita ya uvuguvugu kidogo na unywe kutwa mara tatu. Mchanganyiko huu wa limau na maji ya uvuguvugu utakuondolea maumivu yatokanayo na U.T.I na hata kuzuia kutokwa na damu kama matokeo ya maambukizi ya U.T.I hasa kwenye kibofu cha mkojo.


Vitu vya kufanya kujikinga usipatwe na U.T.I

  • Ongeza unywaji maji kila siku au juisi za matunda, juisi uliyotengeneza mwenyewe nyumbani.
  • Epuka vinywaji baridi, pombe, chai ya rangi na kahawa.
  • Penda kuwa msafi.
  • Mara zote jitawaze kutoka mbele kurudi nyuma na uepuke kuchangia na wengine vifaa vya bafuni.
  • Pata haja ndogo mara baada ya tendo la ndoa.
  • Usiushikilie mkojo muda mrefu, mara usikiapo kutaka kupata haja ndogo mara moja nenda
  • Vaa nguo za ndani zilizotengenezwa kutokana na pamba.
  • Epuka kaffeina.
  • Epuka tendo la ndoa kinyume na maumbile.
Dawa mbadala hizi 7 zinaweza kukusaidia kujikinga usipatwe na U.T.I au kujitibu ingawa bado inashauriwa kwenda kumuona daktari iwapo maumivu au dalili zinadumu kwa muda mrefu.

Zingine kama hii:


Pata ujumbe kwenye simu yako! Pokea ujumbe mfupi mmoja bure kwenye simu yako kila siku kuhusu afya. Namba yako kamwe hatapewa mtu mwingine yeyote.
Jaza fomu ifuatayo, kisha bonyeza kitufe cha Jiunge:

Chanzo: fadhilipaulo.com
 
UTI chronic sometimes ni magonjwa ya zinaa, umeshapima magonjwa ya zinaa kupitia damu? napia Kama unae mume au mpenzi wote mtibiwe, mara nyingi mtu mwenye UTI akinywa antibiotic inaisha lakini wewe umeshakunywa antibiotic nyingi huponi means sio ya kawaida, jiongeze usingangane tuu ni UTI, dawa inayotibu UTI na fungus chronic ninayo ila hiyo UTI yako sijuhi maana hadi powersef imegoma?
 
Habari wana javi! Ni KE, ninasumbuliwa na kuwashwa nyetin nkienda kupima napewa dawa za kupachika, nimetumia candistat sana pamoja na gynozol lakini sipon natokwa na majimaji yanaelekea kuwa kama kamasi rangi ya kijanjan. Kwa upande Wa UTI kila nkipima mkojo naambiwa ni mchafu nimetumia cipro sana pamoja na kuchoma powersafe nkimaliza dose sioni mabadiliko nkikojoa mkojo unauma kwa mbali baada ya kumaliza, kuna kipindi huwa hali inatulia tena inaanza. Najitahidi sana usafi Wa chini na kunywa maji mengi lkn wapi. Kwa anayefahamu Tiba zaidi ya hizo naomba anisaidie, Asante!

Una ukimwi wewe..huwezi kupona
 
kuna dawa inatolewa na kampuni inayoitwa BF SUMA hiyo dawa inaitwa FEMICARE ni nzuri sana kwa tatizo lako hilo, itafute na uitumie nakuhakikishia itakuwa mwisho wa tatizo lako. utapopona uturudishie mrejesho
 
Pole Sana my dia,inabidi ukamuone specialist w wanawake acha kwenda hospital z kawaida,kwakuongezea wanawale wengi hawajui jins y kusafisha nyuchi ,wanaweka vidole ndan kwa adai wanasafisha kumbe wanaharibu,ukishapona jitahid kubadili mfumo mzima w kusafisha kwa bibi,usisondeke kidole utatoa bacteria wazuri wanaokulinda...google jinsi y kusafisha huko,halafu kunywa maji mengi Sana,mazoez usiache,Kula healthy food ili uipe nguvu immunity yako iweze kuoambana na magonjwa....pia kacheki STD's...
 
Habari wana javi! Ni KE, ninasumbuliwa na kuwashwa nyetin nkienda kupima napewa dawa za kupachika, nimetumia candistat sana pamoja na gynozol lakini sipon natokwa na majimaji yanaelekea kuwa kama kamasi rangi ya kijanjan. Kwa upande Wa UTI kila nkipima mkojo naambiwa ni mchafu nimetumia cipro sana pamoja na kuchoma powersafe nkimaliza dose sioni mabadiliko nkikojoa mkojo unauma kwa mbali baada ya kumaliza, kuna kipindi huwa hali inatulia tena inaanza. Najitahidi sana usafi Wa chini na kunywa maji mengi lkn wapi. Kwa anayefahamu Tiba zaidi ya hizo naomba anisaidie, Asante!

Hayo maji maji ya kijani yana harufu mbaya?
Je ukifanya mapenzi unaumia?
Je tumbo la chini linauma?
Unaweza kukuta unamaambukizi sugu ya kwenye viungo vya ndani vya uzazi.
Nenda hospitali ya kueleweka kwa uchunguzi wa kina.

Kama una recurrent vaginal candidiasis jaribu kuangalia yafuatayo.....
1.Pima HIV
2. Pima kisukari
3. Angalia aina ya nguo za ndani uvaazo , ni vizuri zikawa za Pamba tupu , uwe unavaa zikiwa kavu kabisa na ukifua uanike juani ...n:b ni vizuri ukawa nazo nyingi.
4. Pia angalia unavyoiosha papuchi yako kwa ndani , excessive douching na kutumia sabuni sana unaharibu normal flora ya vagina. Haifai kuosha sana papuchi kwa ndani.
Pole sana.
 
wewe uliesema anaukimwi (hiv) nimekustai sana,kama ushauri wa kujenga hukuwa nao ungekaa kimya.
 
Back
Top Bottom