Habari zenu wapendwa,
Nina tatizo la UTI ambalo limeanza kujitokeza tokea mwanzoni mwa mwaka huu nikawa nakunywa tu dawa linapungua, kufikia mwezi wa saba nikazidiwa na kupimwa kwa Daktari nikaambia nina UTI 50,000 kitu ambacho Dk alisema ni kiwango kikubwa sana kuwahi kutokea ikabidi nipumzishwe kwa huduma ya karibu. Nilipata dawa ya vidonge jina sikumbuki ila kasha lake lima mualizeti hivi na pia nikachomwa sindano za Gentamisene.
Baada ya wiki moja kupita nilipima tena nikawa bado nina UTI 70 ambapo nilienda tu duka la dawa na kununua dawa moja inatajwa tajwa kama ni nzuri kwa UTI nimemaliza kama siku tano zimepita leo nimejihisi miwasho sehemu za siri sikusita kwenda kupimwa katika moja ya dispensay ya karibu nikakutwa tena ninayo UTI 500.
Sasa hapa sielewi kwani huu ugonjwa huwa hausikii dawa au kuna dawa nyingineambayo kali zaidi kumaliza tatizo hili? maana linonekana ni sugu sasa kwangu na nimelichoka kabisa, Naomba msaada wenu wadau wangu maana najua kwenye wengi haliharibiki neno.
Karibu