Wakuu poleni na majukumu kama kichwa cha mada kinavyo jieleza,nina miezi 3 sasa nasumbuliwa na UTI isiyopona nilianza kujisikia kuwashwa kwenye njia ya mkojo Dec.2017 nikaenda hospitali baada ya vipimo ikaonekana nina UTI Dr akaniandikia dawa amoxilin nikatumia kwa ufasaha.
Mwaka huu 2018 mwezi wa kwanza nikaanza tena kuhisi maumivu kwenye njia ya mkojo na safari hii mpaka kwenye korodani nikarudi tena hospitali Agakhan wakachukua vipimo vya mkojo na damu majibu yalipotoka ikaonekana sina magonjwa mengine ya zinaa bali UTI Dr akanipa cefalexin capsule na zenyewe nikatumia vyema hali ya maumivu ikapotea kwa muda.
Mwezi huu wa pili nikaanza kuhisi maumivu sehemu za ubavuni karibu na nyonga,maumivu ya korodani na njia ya mkojo nikaamua kwenda hospitali ya rufaa baada ya kutoa maelezo Dr akaniandikia kipimo cha utra-sound,x-ray,na culture sensitivity majibu yalipotoka ikaonekana kwenye mkojo hakuna mdudu aliyeota,utra sound ikaonyesha kuna bacteria kwenye kibofu cha mkojo.
Nikaandikiwa Ciprofloxacin kwa siku 30,kabla sijatoka nikamueleza Dr.kuwa nina sumbuliwa na gastritis kwa muda mrefu na cipro ni moja kati ya dawa zinazonisumbua sana nikitumia Dr akanijibu hakuna mbadala cipro ni dawa nzuri tu,ila kanywe ukishindwa basi.
Sasa nimejitahidi nimekunywa kwa siku nane,tumbo likaanza kuuma sana hata kula ni kwa shida,nimeamua kuacha.
Naomba ushauri nitumie dawa gani?hakuna sindano mbadala wa cipro vidonge?