Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,887
- 7,673
Sina access na jukwaa la JF Doctor lakini kwakuwa ni jukwaa la hoja mchanganyiko naomba wenye utaalam na uzoefu watatue na watuelimishe katika hili.
Ugonjwa wa UTI hupunguza kweli nguvu za kiume?
Hutapata ushauri mzuri humu zaidi ya kwenda tena kwa Dr. amchukue vipimo na kuona nini hasa tatizo. Pole sana mkuu,endelea kumpenda na kumjali mkeo namna hiyo.
Wanajf naombeni msaada juu ya hili. Mke wangu anasumbuliwa na kuumwa tumbo na mgongo mara kwa mara. Mara ya kwanza tulienda hospitali wakasema ana U.T.I,akapewa dawa baada ya kumaliza ile dose alikaa kama miezi miwili bila hayo matatizo then akaanza tena kulalamika. Tukaenda hospital nyingine akapewa dawa na kushauriwa aache kutumia vidonge vya uzazi wa mpango(akasitisha matumizi yake),tangu mwezi 9, mwaka jana mpaka juzi 14/01/2012 ameanza tena kulalamika tumbo na mgongo. Kabla na nikiwa nafikiria nini cha kufanya naombeni mawazo yenu kwa uzoefu, ufahamu na ushauri wa kitaalamu juu ya hili.
U.T.I ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa mkojo wa binadamu{urinary system}ugonjwa huu unasababishwa mara nyingi na aina moja ya bacteria anayeitwa ESCHELICHIA COLI,ugonjwa huu unaweza ukawapata wanawake na wanaume .Kutokana na swali lako ugonjwa wa U.T.I kwa mwanaume unasababishwa na njia nyingi kama vile ushoga[homosexual},kunywa maji yasiyo salama,kushea nguo za ndani{chupi},kushea choo kichafu na watu mbalimbali,kuanika nguo za ndani nje .n.k.
Na dalili za huu ugonjwa ni homa kali[fever},kukojoa mkojo mzito na wenye harufu kali[clouds urine},pia unaweza ukapata maumivu chini ya kitovu[abdominal pain} na maumivu wakati wa kukojoa.Ila si lazima ukiumwa huu ugonjwa uwe na dalili zote hizi nilizozitaja unaweza ukapata dalili mojawapo kati ya hizi.
Mwanaume anayeumwa U.T.I akifanya mapenzi na mwanamke anaweza akamwambukiza au kutomwambukiza inategemea na jinsi walivyofanya hayo mapenzi.matibabu ya U.T.I ni unapewa antibiotics kama vile ceftriaxone,rimfapicin gentamycin n.k.
Young_Master,
Hapo kwenye bluu, panaenda kinyume na shule yangu ya Microbiology. Unaweza ukanifafanulia? inawezekana shule yangu ipo outdated....