Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
UTI= Urinary Tract Infection ni ugonjwa unaoambatana na mfumo mzima wa njia ya mkojo kutokea kwenye mafigo, mirija ya mkojo (ureter), kibofu, tunda (prostate gland ) na njia ya kupitia mkojo kwenye uume (urethra)
Hivyo sababu huambatana na chanzo cha tatizo katika mojawapo ya sehemu husika, Mfano:
1. Ugonjwa wa sukari hufanya kiwango cha sukari kuwa kikubwa kwenye damu kwa vile mafigo kazi yake ni kuchuja damu hivyo ni kusema sukari huingia kwa wingi kiasi cha kusababisha vidudu bakteria kuzaliana kwa wingi kwenye mafigo au kibofu cha mkojo.
2. Madawa /sumu huchubua utando wa njia ya mkojo na kusababisha bacteria kuzaliana
3. Matatizo ya vijiwe kwenye figo/ mirija ya mkojo, kibofu, hufanya msongomano wa mkojo na Vijidudu huzaliana.
4. Maradhi ya Tunda Prostate gland huvimba na kufunga njia ya mkojo matokeo yake kuuzuia na kuuweka mkojo mda mrefu kwenye kibofu mpaka bacteria kuzaliana.
5. Tendo la ndoa, sexual intercouse unapata vijidudu moja kwa moja kutoka kwa mwanamke mwenye uambukizo
6. Kujichua, tendo hili mara nyingi watu hutumia mafuta au sabuni ambazo huwa zina kemikali zinazopenya kwenye mrija wa mkojo huwasha na kusababisha vidonda ambayo bacteria hukua na kazaliana,
7. Usafi, aidha kwa kujikamua sana baada kukojoa, kutawaza maji machafu kutokuwa na hali ya unadhifu, huko chini kuna vijidudu ambavyo huishi baina ya njia ya haja kubwa na makorodani kutokana na hali ya ujoto humea vizuri na hupata nafasi ya kukuingia kwenye mirija kama utakuwa huna tabia ya kuwapunguza kwa usafi.
Natumai nimejaribu kukutajia sababu kuu muhimu katika mazingira ya kawaida huenda zikakusaidia kukata kiu yako.
Asante
Maambukizi kwenye njia ya mkojo
Information Description
Wanawake na wanaume wanaweza kupata maambukizo kwenye njia ya mkojo, lakini zaidi kwa wanawake kwa sababu ni rahisi bakteria kuingia kwenye njia ya mkojo. Dalili za maambukizo ni:
Kutaka kukojoa mara kwa mara
Kusikia maumivu makali wakati wa kukojoa
Mkojo kuchanganyikana na damu.
Maambukizi haya yanaweza kuepukwa kwa kujiweka safi hasa kwa kusafisha eneo la via vya uzazi kila siku na kuhakikisha unanawa baada ya kwenda haja kubwa. Wakati wote unasafisha kutoka mbele kuelekea nyuma. Ukisafisha
kutoka nyuma kwenda mbele unaweza kusambaza bakteria kutoka kwenye haja kubwa kwenda kwenye tundu la
mkojo. Hatua nyingine za kuchukua ili kuepuka maambukizo haya ni kunywa maji mengi; kukojoa mkojo mara kwa mara (usijaribu kubana mkojo kwa muda mrefu) na hasa baada ya ujamiiana, na kuvaa chupi za pamba na nguo pana zinazoweka sehemu za siri kavu.
Iwapo unafikiri unayo maambukizo kwenye mrija wa kupitisha mkojo, kunywa maji mengi na nenda
kamwone mhudumu wa afya kwa ajili ya matibabu. Usijamiiane mpaka dalili zote ziwe zimetoweka.
Siwezi kutowa Dawa kabla ya kumaliza somo lenyewe mkuu The secretary Si nimekuambia nitaendelea somo lenyewe ni kubwa sana.hapo poa nasubiri tiba mbadala
Siwezi kutowa Dawa kabla ya kumaliza somo lenyewe mkuu The secretary Si nimekuambia nitaendelea somo lenyewe ni kubwa sana.
Mimi sio Daktari UPOPOSomo zuri ,je wewe ni Dactari?