Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Mkuu tiba ya kikorea inapatikana wapi yani nimechoka hadi mood ya kukutana nae inaisha

Sent using Jamii Forums mobile app

Achana na haya mambo ! Mkapime mkojo wote kisha anzeni dawa kwa pamoja ! pia inawezekana kabisa kwa unavosema inatoka harufu kwenye mkojo sio kweli ; harufu inatoka mara nyingi iwapo kuna infection kwenye njia ya uzazi , hapo lazima mkapime pia magonjwa ya zinaa (STI's) lakini pia , ungemshauri kama mwenza wako anatumia dawa asijihusishe na tendo la ndoa hata kama nje ya nyumba yaani mtu mwengine.

Kwa wewe mwanadada ni muhimu kunywa maji mengi sana wakati unatumia dawa za UTI, hii inasaidia kusafisha kibofu cha mkojo.
 
1.amepima mwezi mmoja ulipita
2.alipewa amoxilin clavam na sindano moja powerceff
3.nimepima weak moja ulipita
4.nimetumia ciproflaxin
5.tulipima tulivyokaribia kufunga ndoa
5.kwa mimi ni mkojo wenye harufu tofauti na siku nyingine hivyo nikisikia hiyo harufu tu najua
5.yeye kuumwa hadi kwenda hospitali toka nimemfahamu ni mara moja aliumwa kichwa na kusikia baridi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtibuni na mchepuko wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndani ya huo mwezi imejirudia mara moja nikatumia ciproflaxin kwa siku 5 jipili nimekutana nae jana nimeanza tena sikia harufu ya mkojo ila siumwi na yeye haumwi na tusipokutana hata mwezi hiyo shida hainipati though nikukutana nae tu lazima nipate


Sent using Jamii Forums mobile app
Kunyweni sana madafu

[emoji252] [emoji479]
 
Huu uzi unavutia zile dawa zetu za mtishamba zipate soko na watakuja kizinadi sanaa.

Pole kwa kuumwa.
 
Mkuu tiba ya kikorea inapatikana wapi yani nimechoka hadi mood ya kukutana nae inaisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda Riverside, (Dar es salaam) fika pale kwenye kituo cha boda boda , ulizia Sun Dispensary... au hospitali ya Wakorea. Ni mwendo wa dk 5 kwa muguu, hakika hutajuta, binafsi hali ilikua tete ila sasa niko safi kabisa, ukifanikiwa lete mrejesho ili iweze kuwaponya na wengine wanaosumbuliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa tutapima vyote nimechoka kwa kweli.harufu naisikia kwenye mkojo yani unakuwa na harufu tofauti na siku nyingine na nisipokutana nae hata mwezi siisiki hiyo harufu kwe mkojo yani unakuwa clean na bila harufu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wakuu .nimeolewa miezi michache iliyopita kila nikikutana kimwili na mume wangu napata uti yeye alishaumwa akapewa dawa na sindano lakin kila tukikutana napata uti tena naombeni msaada wenu wangu


Sent using Jamii Forums mobile app
Maradhi ya UTI sugu hayawezi kutibika kw asindano zaHospitali utatumia mpaka utachoka nitafute mimi nikupe dawa zangu za asili upone kwa siku 14 tu. Ukinihitaji nitafutew kwa wakati wako.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili Herbalist mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Herbalist MziziMkavu
 
jamani wan JF naombeni msaada kwa hili! nina kaka yangu anasumbuliwa sana na UTI kama kuna mtu anafahamu dawa nzuri anielezee! ameshakunywa sana antibiotics (cipro,cephalexin,celexin etc) lakini wapi inatoka kwa muda then inarudi!

napendelea sana tiba asilia mwenye ujuzi amwage data
 
The problem is not a medicine you take but is how you live--your home,thus why you get UTI infection frequently
 
ELIMU YA AFYA KUHUSU U.T.I!! NA KAMA HALI HALISI NDIYO HII BASI KUNA UWEZEKANO WANAOPATA MAJIBU SAHIHI YA UTI NI ASILIMIA NDOGO SANA!![emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]

MAJIBU ya UTI hayatoki ndani ya muda mfupi

By Kalunde Jamal, Mwananchikjamal@mwananchi.co.tz

Hali yako kiafya siyo nzuri na unahisi una malaria kutokana na kuwa na dalili zote za ugonjwa huo.

Unaamua kwenda zahanati kupata vipimo vya afya, unakutana na foleni ya wagonjwa, hivyo unafuata utaratibu wa kwenda kumuona daktari kisha unachukuliwa vipimo na kupelekwa maabara.

Ndani ya saa moja, ukiwa umekaa kwenye benchi huku umeshika tama, anakuja muuguzi kukuita ili uende kuchukua majibu yako kwa daktari ambayo yanaonyesha una maambukizi ya njia ya mkojo (UTI).

Hakika ugonjwa huu umekuwa ‘maarufu’ siku hizi kwa kuwa wengi wanaokwenda katika baadhi za hospitali, zahanati au vituo cha afya kupata tiba huambiwa wana UTI.

Huenda hiyo ndiyo sababu ya kushamiri kwa biashara ya kuuza dawa za ugonjwa huo kwenye baadhi ya zahanati na vituo vya afya.

Utafiti uliochapishwa miaka kadhaa iliyopita na Asina Pacific Journal of Tropical Medicine, umeonyesha kuwa zahanati na vituo vya afya binafsi hulenga kuuza dawa kama chanzo cha mapato badala ya kuangalia afya ya mteja(mgonjwa).

Kwa mujibu wa utafiti huo, vituo vya afya na zahanati binafsi huongeza malipo kwa mgonjwa kwa kumuandikia sindano za ugonjwa huo.

Wagonjwa wasemaje?

Wagonjwa saba kati ya 10 waliohojiwa na gazeti hili kwenye vituo vya afya viwili na zahanati sita waliopimwa afya kutokana na kusumbuliwa na homa, waliambiwa vipimo vyao vimeonyesha wana UTI.

“Hee huu ugonjwa umening’ang’ania kila nikijisikia vibaya nikipima nakutwa na UTI na dawa ninazopewa ni hizi hizi Ciprofloxacin,”anasema Zulfa Zayd ambaye ni miongoni mwa wagonjwa waliohojiwa na gazeti hili. Nilihama zahanati na huku nako nimekutana na yale yale, kilichobadilika ni aina ya dawa huku nimepewa Ciplo, nimechoka jamani.”

Agness Shao aliyekuwa akipima afya kwenye zahanati iliyopo maeneo ya Kinondoni anasema anajua ugonjwa wake ni huo.

“Nikijisikia vibaya nakwenda kupima kwa ajili ya kujiridhisha, lakini najua kabisa huu ndiyo ugonjwa wangu kwa sababu tunatumia choo kimoja watu wengi,” anasema Shao.

Wataalamu wa afya wazungumza

Mganga mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi anasema waliopewa mamlaka ya kulinda afya za wananchi wanaonekana kulisahau jukumu lao na kwa kufanya hivyo wanahatarisha maisha ya wananchi.

“Tumekuwa tukisema mara nyingi hatua za kupima maradhi hayo, kwanza unaupima mkojo na unaweza kupata mabadiliko ya mkojo kwa kupima kipimo cha kwanza ukahisi ni UTI, ilihali kitaalamu ni lazima kujiridhisha kabla ya kutoa uamuzi wa majibu kwa mgonjwa,”anasema Profesa Kambi.

Anaongeza kuwa mkojo unapopimwa unaweza kuonyesha kuwa kuna bakteria, ili kujiridhisha kama ni wa ugonjwa huo lazima wale bakteria waoteshwe hatua hiyo kitaalamu inaitwa (culturing bacteria).

“Ili upate majibu sahihi kipimo hiki huchukua saa 48 kwa uchache hadi 72, tofauti na hapo majibu hayo si sawa. Tunakemea kila siku kumpa mtu dawa za ugonjwa asiokuwa nao... ni kumtia usugu, kwa sababu ukifanya na kipimo cha kuotesha bakteria kinakupa na mwelekeo wa dawa gani atumie, kwa kuhisi hisi lazima utampa isiyokuwa sahihi,” anasema Profesa Kambi.

Daktari Godfrey Materu wa Kituo cha Afya cha Arafa kilichopo maeneo ya Temeke Dar es Salaam, anasema kuna wagonjwa wanakwenda kupima wakiwa na majibu yao kichwani.

“Kuna wakati tunalazimika kutoa elimu, kwa sababu wagonjwa huja na majibu ya magonjwa yao kichwani, wanapoambiwa hawana homa wanakasirika na kwenda kupima mahali kwingine.

“Kuna wakati nilinusurika kufukuzwa kazi kwenye zahanati fulani baada ya kumueleza mgonjwa aliyekuwa anapata homa kuwa hana malaria, UTI wala Typhoid badala yake ana uchovu akanywe maji na apumzike muda mrefu, ”anasema Dk Materu.

Anafafanua kuwa mgonjwa alikuwa anamfahamu mwenye zahanati ndipo alikwenda kumwambia kuwa hakupimwa ipasavyo.

“Aliambiwa (na mwenye zahanati) aje siku inayofuata na asilipe; apimwe na daktari mwingine. (alipopimwa) alikutwa na UTI nyingi na malaria wadudu watano na kununua dawa pale pale na aliondoka kwa furaha,”anasema.

Kutokana na vipimo hivyo kutofautina na vyake, bosi wake alimfokea na kumuona kama mtu anayetaka kumfukuzia wateja.

“Sipingani na hilo, lakini nashauri wagonjwa wawaamini wataalamu wa afya, badala ya kuja na majibu ya homa zao kwa madai wanajijua,” anashauri Dk Materu.

Utaratibu wa vipimo vya UTI

Mkuu wa mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha KCMC, Profesa Alfred Mteta anasema ili kujua kama mtu ana UTI au la, mkojo wake unatakiwa kupita kwenye vipimo saba.

Anasema vipimo hivyo vikibainisha kuwapo kwa bakteria ndiyo wataoteshwa kupata uhakika kama ni maradhi hayo au la, na itafanyika kwa saa *48 au 72.*

“Kinachofanyika sasa ni biashara badala ya huduma, hawa wenye hizi zahanati wanalenga zaidi kuuza dawa.

“Wanasahau kuwa kazi yao ni kulinda afya za watu na siyo kuwaumiza, kumpa mtu dawa kwa ugonjwa asiokuwa nao ni kuufanya mwili uwe sugu na usikubali matibabu,”anasema.

Profesa Mteta anasema UTI inaanza na dalili kwa mgonjwa ikiwamo kuhisi maumivu au moto kwenye njia ya mkojo na kukojoa mara kwa mara.

“Baada ya dalili hizo mgonjwa akisikilizwa na kupimwa na daktari, hufanyiwa pia vipimo vya maabara. Kipimo cha kwanza na cha muhimu sana ni urinalysis ambacho pamoja na mambo mengine mkojo wa mgonjwa huzungushwa kwenye mashine maalumu (centrifuge) halafu huangaliwa kwenye darubini!,” anasema Profesa Mteta.

Akielezea zaidi anasema lengo ni kuangalia kama kweli kuna ushahidi wa UTI hasa uwapo wa white cells na red cells (Seli nyeupe na nyekundu) nyingi.

“Vilevile huangalia uwapo wa bakteria katika mkojo pamoja na aina nyingine za seli na vijidudu,” anasema.

Akizungumzia hatua ya pili, anasema ni kuufanyia ule mkojo ‘culture’ yaani kuotesha na kutambua aina ya vidudu vilivyo kwenye mkojo.

“Hii ya culture huendana na sensitivity test yaani vile vidudu vilivyoota hujaribiwa kwenye maabara ni dawa gani itafaa kuvitibu. Hatua zote hizi _zinachukua saa 48 hadi 72! Lakini_ zinampa daktari uhakika wa uwapo wa UTI na matibabu gani yatolewe yaani antibiotic gani na kwa dose gani na muda gani.

“Huo ndiyo utaratibu ambao sasa unavunjwa na baadhi ya watu wasio na weledi kwenye taaluma ya afya ambao huchukua njia ya mkato na kubambikiza wateja UTI ili kuwauzia dawa tu,” anasema Profesa Mteta. Pia, anasema wagonjwa wanaweza kuathirika na antibiotics hizo na vilevile dawa holela husababisha usugu wa vijidudu kwa antibiotics.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom