Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Suala si kupatiwa dawa ,ishu ni kujua hyo source ya UTI,ukute leo unapatiwa dawa bda ya wiki unarudi hospital kama kawaida,Fanya vipimo upate uhakika kuna tendency UTI inaweza ikawa secondary cause so fanya vipimo kama ultrasound,urine culture and sensitivity then primary disease itibiwe na proper dose na combination ya broad spectrum antibiotics

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Habari za jumapili wapendwa,naomba kuuliza nini dawa nzuri ya UTI,mana nilipima hosp na wakaniambia ni UTI wakanipa anti biotics,Cplo na dox,sasa tatizo limerudi tena,je kuna dawa mbadala?hata kama ni ya kienyeji jamani mana hali yangu si nzuri

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Nenda kwenye hospital kubwa zaidi achana na mambo ya dawa za kienyeji ambazo nyingi ni za kubahatisha wakati unaendelea kuumia
 
Matibabu ya UTI-hutegemea na severity(Mild,severe,acute or chronicity) ukishajua ni UTI ipi unatakiwa utumie appropriate dose...na pia uzingatie upande wa pili wa matibabu ambayo ni kujitahidi kuepuka zile sababu zilizo kufanya upate UTI-mfano kutumia vyoo vichafu hasa vya kukaa, kukaa na mkojo mda mrefu bila kuotoa(kukojoa) na kutokua na mazoea ya kunywa maji ya kutosha(kunywa maji ya kutosha inasaidia).......kama UTI inakua inakurudia mara kwa mara (recurrent UTI)ni vzr kufanya CULTURE and SENSTIVITY test ya mkojo...ila kupata antibiotic inalenga wadudu waliopo moja kwa moja...
 
samahami naomba kuuliza. Je u.t.i ikikomaa sana au ikiwa inajirudia rudia inasababisha matatizo kwenye kizazi?? Na je njia ya mkojo na kizazi vinahusiana??? Kwamba wadudu wa u.t.i wanaeza shambulia kizazi??? Samahan naomba mnisaidie kunipa jibu jamani i need to know please.
 
Asanteni sana kwa ushauri wenu,basi nitaenda hosp kupima

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Maambukuzi ya njia ya mkojo (urinary tract infections) au kwa kifupi UTI kama ilivyozoeleka kwa wengi. Kwa kiasi kikubwa, labda na hata wewe msomaji pengine ni zaidi ya mara moja umewahi kusikia mtu mzima au mtoto akiambiwa anasumbuliwa na UTI.

Kwa mtoto, mara nyingi si tabu sana na hakuna maswali mengi lakini kwa mtu mzima kidogo muhusika mwenywe yaani mgonjwa na watu wa karibu naye wanakuwa na maswali mengi kuliko majibu. Mfano watu

watahoji, Je UTI inasababishwwa na nini? Je mhusika kaipataje hiyo UTI? Je kujamiiana inaleta UTI? Na je inaweza kumuambukiza mwenza? Je nini matibabu yake? Je nini madhara yake ya muda mfupi na mrefu?.

Kwa hakika haya ni baadhi tu ya maswali yatupasayo kuwa na majibu juu ya tatizo la UTI.

Basi leo naomba nichukue fursa na muda wenu kidogo tuzungumzie japo kwa ufupi tatizo la UTI, tukilenga kutoa majibu kwa baadhi ya maswali hapo juu bila kusahau suala zima la kinga na matibabu ya UTI.

UTI ni nini ?

Maambukizi katika sehemu yeyote ya njia ya mkojo husababisha maradhi na matatizo ya aina mbalimbali. Mara nyingi tunapozungumzia UTI, huwa tunalenga maambukizi yanayosababishwa na vimelea (bakteria) au chochote kile kinachoweza kusababisha UTI huingia katika njia ya mkojo kutokea aidha nje ya mwili au hata ndani ya mwili kwa njia ya damu au vinginevyo.


UTI huweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia au umri. Hata hivyo, yapo makundi ambayo kutokana na sababu za kibiologia na kinga ya mwili kushuka au kuwa ndogo huathiriwa zaidi na tatizo hilo. Makundi hayo ni pamoja na watoto, wazee na wanawake.


Watoto ni waathirika wakubwa wa UTI na yaweza kusababisha maambukizi kusambaa hadi kwenye damu na mwiili mzima na hatimaye kusababisha kifo. Maumbile ya watoto na utegemezi walio nao wakati wa kujisaidia

inaweza kuwa ni sababu hatarishi kwa wao kupata tatizo hili. Vile vile kinga yao ya mwili bado huwa bado haijakomaa kuweza kuhilili uvamizi wa vijidudu mbalimbali kwenye miili yao.


Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hasa ya mfumo wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bacteria. Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi sana ukiliganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bakteria kupata urahisi wa kuingia ndani.


Ukubwa wa tatizo

UTI ni tatizo kubwa katika jamii na jinsia. Hata hivyo hakuna data au taarifa kamili juu ya ukubwa wa tatizo hili katika maeneno mengi Duniani hasa katika nchi zinazoendelea zilizo na miundombinu duni na changa ya afya. Utunzaji wa kumbukumbu ni tatizo linachongia pia ukosekanaji wa taarifa.


Kwa kiasi kikubwa tatizo la UTI huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume, zaidi ya mara mbili kwa kukadiria. Karibu kila mwanamke katika maisha yake anaweza wa kupata UTI japo mara. Pia uwezekano upo kwa tatizo kujirudia mara kwa mara.

Sababu za UTI

UTI yaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Mathalani ni vimelea (bakteria) japo pia na jamii nyingine ya vijidudu vinaweza kusababisha UTI. Bakteria aina ya Escherichia coli kwa kiasi kikubwa ndio

inayosababisha UTI japo pia bakteria wengine wapo. Vijidudu hivi vyaweza kuingia katika njia ya mkojo kutokea nje ya mwili au hata kwa kupitia damu ya mhusika.


Kwa wanawake, fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya mvuto kwa bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi, hasa UTI.


Kwa wanaume mara nyingi kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, huwa siyo waathirika wakubwa wa UTI.


Vihatarishi

Sababu hatarishi (risk factors) za UTI zipo nyingi, kulingana na umri, jinsia na mazingira ya mhusika. Mfano sababu hatarishi za mtoto mchanga kupata UTI si sawa na mtu mzima jinsia ya kike. Maumbile na mfumo wa

kibiologia ya mwanamke humweka katika nafasi hatarishi zaidi ya kupata UTI. Vile vile ngono, tena ya mara kwa mara ni moja ya sababu zinazoweza kuchangia mtu kupata UTI.


Kwa kupitia ngono, bakteria waliopo katika sehemu za siri za mhusika vinaweza kupata nafasi ya kupenya na kuingia katika mfumo wa njia ya mkojo kwa urahisi zaidi.


Sababu nyingine ni upungufu wa kinga mwilini kwa sababu yeyote, ikiwamo ujauzito kwa wanawake na ugonjwa wa kisukari (diabetes). Lakini pia, sababu nyingine kadha wa kadha zinazosababisha upungufu wa kinga mwilini.


Dalili za UTI je?

Dalili za UTI kwa kiasi kikubwa hutokana na umri na jinisia ya mhusika, lakini zaidi kisababishi (cause) ya UTI. Dalili zinaweza kuwa kusikia maumivu wakati wa kukojoa, homa na maumivu katika viungo vya mkojo, kuhisi kuhitaji kukojoa mara kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa.


Nyingine ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu na au mgongo kwa chini. Mkojo wenyewe unaweza onekana wenye damu au usaha.


Kwa watoto dalili pekee kubwa ni homa. Hii inaweza kuambatana na kushindwa kula vizuri, kulia lia sana na hata kutapika.


Matibabu ya UTI

Matibabu ya UTI kwa kiasi kikubwa unapatikana bila shida na usumbufu mkubwa maadam tatizo lijulikane mapema na kwa usahihi. Utaratibu mzima wa matibabu hutegemea majibu ya maabara, kisababisho cha UTI na umri pia wa mhusika


Pamoja na hayo, UTI ni ugonjwa unaozuilika. Kwa ujumla suala zima la kuzingatia kanuni za afya bora hasa ya mwili na mazingira ni suluhisho tosha kwa tatizo la UTI.


Unywaji wa maji mengi ili kupata mkojo mwingi ili pengine uweze kusafisha njia ya mkojo nayo pia inashauriwa. Inashauriwa pia kukojoa mara tu baada ya tendo la kujamiiana. Kwa watoto ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi ya pampers hasa kubadilisha kwa wakati.

Dawa ya Maradhi ya UTI:

Kwa Mtu Mgonjwa wa Maradhi yoyote inatakikana awe anakunywa maji Uvuguvugu anapo Amka Asubuhi kabla ya kupiga mswaki Unywe Glasi 2 za Maji ya Uvuguvugu na baada ya kupiga Mswaki Unywe glasi 1 na kabla ya kunywa chai unywe Glasi moja ya maji ya Uvuguvugu kila siku Ufanye hivyo kwa wakati wa asubuhi.

Na Wakati wa Mchana Dakika 15 au dakika 30 kabla ya kula chakula cha Mchana unywe maji ya Uvuguvugu Glasi 1.

Na Wakati wa chakula cha Usiku unatakiwa unywe Maji ya Uvuguvugu Glasi 2 kabla ya kula chakula cha usiku.

na unywe Maji ya Uvuguvugu Glasi 1 kabla ya kwenda kulala usiku. Jumla utakuwa umekunywa glasi 8 kwa siku huu ndio

utaritibu wa kutibu kila maradhi hapo juu uwe unakunywa kila siku mpaka upone hayo maradhi yako na huenda
ikachukuwa muda wa miezi 3 ukifulululiza kunywa hayo maji ya Uvuguvugu utakuwa umekwisha pona maradhi yako.@Mafrank
 
Asante sana kwa majibu mazuri Mzizi mkavu. kwaiyo hapo u.t.i.haiusiani na kizazi?? Xo haiaffect kizazi.
 
Habari za jumapili wapendwa,naomba kuuliza nini dawa nzuri ya UTI,mana nilipima hosp na wakaniambia ni UTI wakanipa anti biotics,Cplo na dox,sasa tatizo limerudi tena,je kuna dawa mbadala?hata kama ni ya kienyeji jamani mana hali yangu si nzuri

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Mkuu kama ulitumia doz ya hizo dawa kwa usahihi na bado tatizo likarudi, kuna uwezekano wa mambo mengi kama:
1. Umeendelea kupata maambukizo au umerudia kupata maambukizi. Kumbuka hizo ni tiba, sio kinga na kumbuka maambukizi ya UTI yanaweza kuhamasishwa na "tabia" fulani fulani

2. Inawezekana una tatizo jingine zaidi ya UTI

3. sababu zinginezo.

Sikushauri uanze ktumia dawa zingine, hadi upate ushauri wa daktari...
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maalifa.hao nifangas wako mwilini nenda phamas kanunue dawa ya Fruncozone.
 
Dr hawaijui utahangaika sana.hailusiw kwa mjamzto au 6momth za kunyonyesha.
 
kuna mdada hana furaha kabisa mda wote anamawazo kama mtu ambae anaelekea kujinyonga. miguu inamvimba na inauma sometimes. baada ya kumhoji sana akaniambia anaumwa na wanawake wenzie wanamwambia kuwa atakuwa na U.T.I naomba kujuzwa dalili za ugonjwa huu
 
Mbona sioni uwiano Kati ya hio UTI na Kuwa suicidal!huyo mtu nadhani ana matatizo kwenye kichwa(schizofrenia) au psycose wanaita wataalamu aende hospitali akapewe antipsyotics.
 
Nina tatizo hili la UTI kujirudia mara kwa mara naombeni msaada wa matibabu kwa kina kwani nimetibiwa huu mwaka unaisha lakini kila nikipima tena inaonekana ipo japokuwa dalili zake hupungua.

Kwa mara ya kwanza nilikua nakojoa mara kwa mara, maumiv wakat wa kukojoa, maumivu chini ya kitovu, homa lakini kadri muda unavozidi kwenda dalili hizo zimepotea ila ugonjwa haujaisha.

Nini tatizo wajameni, ukizingatia kipindi hichi ni mjamzito; je, ugonjwa huu utaniletea matatizo kwa mtoto atakayezaliwa?
 
Unapotibiwa mwenzako/ wenzako nao wanatibiwa? Isije kuwa unatibiwa halafu unarudia ulikopata hiyo UTI.
 
Back
Top Bottom