Urinary Tract Infections ( UTIs) Imekuwa Janga

Urinary Tract Infections ( UTIs) Imekuwa Janga

Kunywa maji kwa wingi hakikisha kila unapoenda kukojoa mkojo wako unakua mweupe....utakunywa madawa mengi ya hosptal na itakua inajirudia!!Dawa ni kunywa maji mengi sanaaaa hasa Asubuhi kabla ya kupata breakfast
 
Vyoo vya public vinachangia sana kusambaza ugonjwa huu kwa wanawake. Kunywa maji mengi husaidia sana lakini kama bi dada nao ugonjwa huu na njemba wake ambao hupeana yale mambo matamu basi njemba naye inabidi atibiwe ili kuumaliza ugonjwa vinginevyo utakuwa unajirudia kila mara.
Nashangaa mtu anaingia ofsini mara anakimbilia kupuu halafu anachafua hewa mpaka wenzake wanatoka njee. Hasa wanywaji wa Safari bia na pombe ya mnazi. Shame thing,!!!
 
Teenagers wasiku hizi wana pata San UTI kwakuwa wana Fanya ngono nyuma na mbele na ndo maana bacteria wa nyuma wana hamia na mbele(ngini kinyume na maumbile)husababisha UTI
 
Kunywa maji kwa wingi hakikisha kila unapoenda kukojoa mkojo wako unakua mweupe....utakunywa madawa mengi ya hosptal na itakua inajirudia!!Dawa ni kunywa maji mengi sanaaaa hasa Asubuhi kabla ya kupata breakfast
Yaonesha maji mengi kweli ni tiba . ...... je hayo maji mengi ndo tiba kabisa ama itakubidi upate na "kikombe cha babu wa samunge"
 
Teenagers wasiku hizi wana pata San UTI kwakuwa wana Fanya ngono nyuma na mbele na ndo maana bacteria wa nyuma wana hamia na mbele(ngini kinyume na maumbile)husababisha UTI
Utafiti huo umetupiwa hapa .... "ngono double" .... Twaweza mpooooooooooooooooo[emoji1] [emoji1]
 
Vyoo vya kisasa vya kuflash ni sababu ya ongezeko la tatizo la UTI hasa kwa wanawake. Zamani enzi za vyoo vya shimo UTI ilikuwa haijulikani kwani ilitokea kwa nadra sana. Lakini leo tatizo hili ni la kawaida sana. Elimu inahitajika ili kutunza usafi wa vyoo vya marumaru na kutunza sehemu za mwili ambazo zinapata maabukizi.
Umeniongezea "ubuyu" mkuu ... na umesaidia kupunguza udadisi nilokuwa nao juu ya kwa nini maambukiz yamekuwa mengi nowadays kuliko zamani
 
Watoto wa kike na wanawake kwa ujumla ndio wanaonekana hasa kuwa wahanga wa UTI kwa sababu ya maumbile ya sehemu za siri hasa wakati wa kujisaidia haja ndogo.
Katika shule za bording (goverment) na vyoo vya maeneo ya public huwa ni vichafu sana, hivyo kupelekea maambukizi ya gonjwa hili.
Kinachotakiwa kufanyika ili kupunguza maambukizi haya kwa wasichana na wanawake kwa ujumla kama ifuatavyo:
1. Kabla ya kujisaidia haja kubwa au ndogo hakikisha unasafisha choo kwa dawa za chooni au sabuni ya dettol itakayosaidia kuua vijidudu vilivyokuwepo tayari kwenye sinki la choo.
2. Unapomaliza kujisaidia, wakati wa kuchamba unatakiwa kuwa makini, anza kujisafisha ukeni baada ya hapo ndiyo usafishe na sehemu ya haja kubwa. Wengi wao hujiongeza maambukizi wenyewe kwani vijidudu vya UTI hukaa katika haja kubwa, kwa hiyo unapochamba kuanzia sehemu ya haja kubwa na kumalizia sehemu ya haja ndogo unakuwa umewahamisha wadudu hao kutoka kwenye kinyesi na kuwaruhusu waingie kwenye njia ya mkojo.
3. Pia unashauriwa kunywa maji safi na salama kwa wingi kwani kusaidia kuondoa tatizo hili kama halijawa kubwa.
Asanteni.
[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] hakika nimehabarika ..... hongera ..... akina dada pitieni hapa mhabarike pia. ..
 
Kunywa maji mengi itapotea yenyewe
ikishagundulika kuwa una UTI ni lazima utibiwe kitaalamu sana maana kuna uti changa na uti sugu... uti changa inatibika kirahisi kwa kutumia antibiotic za kawaida ila kwa UTI sugu ni lazima itibiwe kwa utaalamu sana maana madhala yake yaweza hata kusababishia matatizo ya uzazi mfano kuwa tasa ama mgumba kabisa.... kunywa maji mengi siyo dawa bali ni njia ya ziada ya kupunguza maambukizi ya UTI maana unaweza kunywa maji mengi halafu ukajikuta unaona uvivu kwenda haja ndogo na hapo ukishakaa na mkojo kwa muda mrefu ni hatari sana kwa kuwa utakuwa unachochea zaidi UTI kuanza jichimbia ndani ya kibofu cha mkojo... mana mkojo ni uchafu wa mwilini ambao ukikaa muda mrefu kwenye kibofu cha mkojo vimelea huwa vinatabia ya kuanza kujizalisha na kupelekea ugonjwa huu hatari sana.... ukiona unadalili za UTI usithubutu kujitibu bali nenda hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi!! ahsante
 
Tulishafeli siku nyingi mtihani wa usafi maliwatoni labda turudi tukasome tena sayansikimu
 
ugonjwa huu wa njia ya mkojo UTI ni ugonjwa ambao unatoka na mambo mengi sana mfano kama nguo zako za ndani (chupi) ni chafu basi ni rahisi sana kuupata huu ugonjwa ..kama hiyo haitoshi huu ugonjwa unapatikana sana vyooni yaani vyoo vya jumuiya ambapo ni rahisi ana kuambukizwa hasa akina dada, mama pia hata jinsia ya kiume nayo ni rahisi sana kuambukizwa huu ugonjwa endapo choo kinachotumika hakisafishwi vizuri na unashauriwa kabla hujakitumia choo ni lazima umwage maji mengi ili uwe salama kukitumia choo hicho.... lakini kaeni mkijua huu ugonjwa historia yake ni ndefu kidogo.... damu inapojichuja mwilini moja kwa moja kilichochujwa huelekezwa kwenda kwenye kibofu cha mkojo na mbaya zaidi ukijisikia kubanwa na haja ndogo na nawewe ukaubana au kukaa na mkojo muda mrefu basi kaa ukijua kuwa kwenye kibofu cha mkojo ule uchafu unaanza kutengeneza wadudu ambao utakupelekea wewe kukosa raha kabisa maana utaanza jisikia homa.. unapokojoa utajisikia maumivu wakati wa kukojoa au kuwashwa sehemu za siri hapo ukishaona hivyo chukua hatua ya haraka ya kuenda hospitali na siyo kwenda kwa waganga wa kienyeji, au ukachukua hatua ya kujitibu mwenyewe utajikuta unafanya biashara ya kichaaa... maana siyo antibiotic zote zinaweza kutibu UTI kwa asilimia 100%. nini ufanye ili usipate UTI? kwanza ni lazima uwe msafi hasa nguo za ndani pia usichangie nguo za ndani na mtu yeyote hata za mpenzi wako, usichangie na mtu taulo maana nayo hiyo ni hatari kwa afya yako, usikae na mkojo kwa muda mrefu, kunywa maji ya kutosha maana hiyo itasaidia kusafisha kibofu chako cha mkojo na unapojisikia kubanwa na haja ndogo chukua hatua ya kwenda kukojoa haraka na hakikisha unakojoa mkojo woote, tumia kondomu, unapougua UTI ukishajua basi mshauri hata mpenzi wako muende mkatibiwe pamoja ili kumaliza tatizo, usafi wa hali ya juu hasa hasa chooni, ipende afya yako kwa kuwa msafi na kufua nguo zako mara kwa mara!!!! ahsanteni kwa kunisikiliza
 
Back
Top Bottom