Urithi wa ndoa za Kikristo una mapungufu, wazazi hawapewi chochote

Urithi wa ndoa za Kikristo una mapungufu, wazazi hawapewi chochote

Kwanini Ukristo haujali wazazi kwenye urithi ?

Inauma kuona kwamba mwanaume anaweza kufariki akiwaacha wazazi wake. yeye ndie alikuwa akiwatunza wazazi wake waliozeeka. Lakini kifo kinapobisha hodi, kinachoacha siyo tu huzuni, bali pia pengo kubwa la haki.

Kwenye mgawanyo wa urithi, wazazi wake hawaambulii chochote. ZERO. Ni kama hawakuwahi kumlea, kumpa elimu, au kumsindikiza katika safari ya maisha.

Mali zote zinarithiwa na mke na watoto lakini kiuhalisia mali zote zinakuwa ni za mke kwasababu watoto bado ni wadogo hawajitambui, Mke huyo ataolewa tena na mwanaume mwingine, mali alizorithi zitakuwa ni za ndugu zake na mme wake mpya.

Wazazi wanaambulia SIFURI / ZERO, labda iwe ni kwa huruma tu au kuna usia uliachwa.
Daaaah. Umaskini mbaya sana. Wewe umerithisha nini kwa watoto wako kama mzazi? Mzazi ndo anapaswa arithishe watoto. Mali ya mzazi ni ya watoto. Usikae kuanza kutamani mali ya mwanao wewe mchawi.
 
Kuna urithi wa kikristo?? Mimi najua hivi vitu vipo chini ya sheria ya nchi sio dini
Ni kweli

Kwenye mirathi wakristo asilimia kubwa wako vizuri

Mirathi huwa haisumbui kama ilivyo kwenye uislamu

Kwenye uislamu mwenye akifa ni patashika nguo kuchanika
 
Hao wanawake wengi ni sababu ya mume kufariki halafu ampe mzazi wa mume mali, acha hizo
 
Uislamu pekee ndo dini inotenda haki kwa watu wa rika zote

Urithi kwenye Uislamu kila mtu mwenye haki yake atapata mpaka jirani sio wazee tu
Hizo zote ni tamaa tu ndizo zinawafanya walilie mali ya marehemu!
 
Mafundisho ya Kikristo yanatuelekeza kwamba sisi tutaondoka nyumbani tutaambatana na wake zetu nasi tutakuwa mwili mmoja! Hayatuelekezi kwamba tutaambatana na wazazi wetu!
 
Mnaposema eti wazazi ndio wawarithishe watoto wao mnakuwa na maana ya hawa wazazi wetu wa bongo au wa USA?
Wengi wetu tumetokea familia masikini wazazi wanaishi kwenye nyumba ya matope wakifuga mbuzi au kulima.
Ndio mnasema huyu mzazi asipewe urithi? Tena unakuta wakati huo mzazi ni mzee hana hata nguvu huyu ndio mnamnyima mgao wa mali ya mwanae?
Ndugu zangu mtapata laana. Wapeni wazazi sehemu ya urithi wa mtoto wao
 
Wakristo hawana sheria ya urithi wa mali, Wakristo urithi ugawanywa kwa mujibu wa mila na sheria za Serikali, Wakristo wanaojitambua hawajasurrender taratibu zao kwa dini yao, dini ni sehemu ya kuabudu tu lakini mila na tamaduni zao zinaendelea kama kawaida zikilindwa na sheria ya Jamhuri.
Sheria nyingi za nchi ziliwekwa kwa mfumo kristo
 
Kwanini Ukristo haujali wazazi kwenye urithi ?

Inauma kuona kwamba mwanaume anaweza kufariki akiwaacha wazazi wake. yeye ndie alikuwa akiwatunza wazazi wake waliozeeka. Lakini kifo kinapobisha hodi, kinachoacha siyo tu huzuni, bali pia pengo kubwa la haki.

Kwenye mgawanyo wa urithi, wazazi wake hawaambulii chochote. ZERO. Ni kama hawakuwahi kumlea, kumpa elimu, au kumsindikiza katika safari ya maisha.

Mali zote zinarithiwa na mke na watoto lakini kiuhalisia mali zote zinakuwa ni za mke kwasababu watoto bado ni wadogo hawajitambui, Mke huyo ataolewa tena na mwanaume mwingine, mali alizorithi zitakuwa ni za ndugu zake na mme wake mpya.

Wazazi wanaambulia SIFURI / ZERO, labda iwe ni kwa huruma tu au kuna usia uliachwa.
Ataacha baba na mama ataambatana na mkewe
 
Ukristo hauna sheria yake kwenye urithi.

Bali unafata sheria ya serikali na sheria za kimila za wanandoa

Kwenye sheria ya serikali wazazi wanaingia kwenye urithi
Hakuna sheria ya serikali (Tanzania) ambayo inaeleza kina nani watastahili kurithi mali kupitia mirathi pale ambapo kunakua hakuna wosia. Sheria za Tanzania zinasema waombaji wa usimamizi wa mirithi wanatakiwa wawe watu wenye maslahi na mali za marehemu, na kisha huyo msimamizi ndio atawatambua warithi ni kina nani na ndiye atayeamua nani arithi na nani asirithi.

Sasa inapotokea mabishano, na ikiwa enzi za uhai wake marehemu amethibitika kuwa aliishi kikristo na amekufa pasipo kuacha wosia halali, basi sheria inayotumika ni ya India inaitwa the Indian Succession Act ambapo katika sheria hiyo sasa wazazi watarithi mali pale ambapo marehemu atakua alikuwa na ndoa lakini hakufanikiwa kupata mtoto, na hapo atayerithi ni baba wa marehemu, ikitokea baba amekufa ndio mama wa marehemu atarithi, na ikiwa hawapo wote basi ndio wataingia kaka, dada wa marehemu nk Ikiwa alikuwa na watoto basi warithi wanakua ni mke/mme wa marehemu na watoto.

Kwa hiyo mleta mada yupo sahihi, sheria ya mirathi kwa wakristo inakataa wazazi kurithi mali. Yupo sahihi pia kuona sio fair, kwa kuwa kibongobongo wazazi wengi ni tegemezi kwa watoto wao.
 
Kwanini Ukristo haujali wazazi kwenye urithi ?

Inauma kuona kwamba mwanaume anaweza kufariki akiwaacha wazazi wake. yeye ndie alikuwa akiwatunza wazazi wake waliozeeka. Lakini kifo kinapobisha hodi, kinachoacha siyo tu huzuni, bali pia pengo kubwa la haki.

Kwenye mgawanyo wa urithi, wazazi wake hawaambulii chochote. ZERO. Ni kama hawakuwahi kumlea, kumpa elimu, au kumsindikiza katika safari ya maisha.

Mali zote zinarithiwa na mke na watoto lakini kiuhalisia mali zote zinakuwa ni za mke kwasababu watoto bado ni wadogo hawajitambui, Mke huyo ataolewa tena na mwanaume mwingine, mali alizorithi zitakuwa ni za ndugu zake na mme wake mpya.

Wazazi wanaambulia SIFURI / ZERO, labda iwe ni kwa huruma tu au kuna usia uliachwa.

Urithi unatoka kwa mzazi kwenda kwa Mtoto.
Hiyo ndio maana ya msingi ya urithi

Hizo maana zingine zimekuja kitapeli
 
Back
Top Bottom