Mwalimu Demitria Gibure
Member
- Jul 27, 2022
- 94
- 134
Urithishaji wa maarifa na uwajibikaji katika familia
Uwajibijikaji kwa tafsiri ya kikamusi ni kitendo cha mtu mwenye wadhifa kuchukua dhamana ya kosa lililofanywa ama na yeye mwenyewe au mtu mwingine aliye chini yake, agh. kwa kujiuzulu.
Neno lingine la Kiswahili linaloweza kufanana kimaana na uwajibijikaji ni Masuuli
Inawezekana tunapata changamoto ya kukutana na jamii ya watu wasio wawajikaji kwa sababu ya misingi yetu iliyotenguka kidogo kimalezi. Tunaamini kwamba Kiongozi mzuri huanzia ngazi ya familia na misingi ya uwajibijikaji huanzia hapohapo kwenye ngazi hii kwa kutengeneza kanuni na Taratibu zitakazosimamia kipaji ama kutoa muongozo kwa mwanafamilia mwenye vinasaba vya kuwa Kiongozi.
Kuna baadhi ya mambo yaliyofanyika kwenye jamii miaka ya 1980-1990 yaliweza kutengeneza viongozi wawajibikaji na wenye kuchukua hatua baada tu ya kushuhudia jahazi linakwenda mrama ama kupisha wengine wenye uwezo wa juu zaidi katika utatuzi wa changamoto mbalimbali za jamii. Tukisimama hapa tutashudia malezi ya watoto wa miaka hiyo ni tofauti kabisa na malezi ya kizazi kipya cha miaka hii ya 2000 (Millenials).
Tukumbuke zile adhabu zilizopangwa na familia pindi tunapoenda kinyume na taratibu za familia zetu zilitufanya tujitengenezee kanuni zilizotujenga kujisimamia katika ngazi yoyote ya maisha na kujihoji vema pale tunapoenda kinyume kitendaji.
Nakumbuka kuna namna malezi ya mtoto mmoja yalifanywa na jamii nzima inayomzunguka mtoto huyo. Pindi mtoto huyu anapokosea alionywa na kila jirani na mtoto huyu hakulalamika na wala hakuona anaonewa.
Leo hii tuna jamii ya wanaongoza majahazi wasiotaka kukosolewa, wasiotaka kutoa boriti kwenye macho yao na kubaki kutazama vibanzi kwenye macho ya wengine na kuishia kuonekana ni viongozi walalamishi na wasiokubali kukosolewa.
Leo hii tuna jamii ya watu wasiohitaji kujifunza mbinu mpya za kiutawala na kuishia kuyaishi maisha yasiyorndana na kasi ya mabadiliko ya Kisayansi na teknolojia.
Bado tunashuhudia uwepo wa jamii yenye chuki pindi mmoja wa wanajamii akikabidhiwa majukumu yaliyoshindikana kufanywa na mmoja wa wanajamii husika na kutengeneza vikundi vya majungu vyenye kumsimanga aliyewekwa kwenye nafasi ya Kiongozi aliyewajibishwa kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu walizojipangia.
Wingi wa imani potofu juu ya kukosolewa na kujawa kwa fikra hasi zinazohusiana na uwajibijikaji kwa kufikiri Kiongozi hakosei na akikosea kategeshewa ama karogwa jambo ambalo huwafanya wanajamii fulani kukesha kwenye nyumba za ibada ama kwa waganga wa jadi walidhibiti nafasi zao hata kama zinakwenda kombo.
MAMBO YA MSINGI YA KUJENGA JAMII YA WAWAJIBIKAJI
1. MISINGI YA MALEZI YA MTOTO KWENYE FAMILIA. Naamini tukiwalea watoto katika misingi ya kuwawajibisha itasaidia kujenga jamii yenye kizazi cha viongozi bora kabisa. Huwezi kuikana familia yako pale mambo yanapokwenda kombo bali tunaweza kuwafundisha watoto kuomba msamaha pindi wanapoenda tofauti na taratibu, kuwa tayari kujifunza kwa wengine ili wasiyumbishe maendeleo, kuwaelekeza kupisha nyadhfa mbalimbali pale wapoona kushindwa kufikisha jahazi salama kwa kutumia utashi, busara, hekima na upendo mkuu. Hii itapunguza migogoro ya fikra inayowakuta viongozi wanaowajibishwa na kutengeneza wigo wa kujifunza kuwajibika na kuendelea na maisha mengine kama mwanajamii mwenye manufaa kwa jamii husika.
2. KUTOA ELIMU YA MALEZI KWA VIJANA WA SASA Ili tutengeneze viongozi bora ni muhimu kuelimisha vijana wanaojiandaa kuanzisha familia namna ya kuwalea watoto wanaotarajia kuwapata kwa kuwapa miongozo mbalimbali ya namna ya kukuza vipaji mbalimbali vya watoto na kuwafundisha ama kuwarithisha maarifa ya uadilifu katika maisha yao ya baadae. Kwa kufanya hivi tutengeneza kizazi chenye uadilifu mkubwa kabisa.
3. URITHISHAJI WA SIASA SAFI ZENYE KUHESHIMU UTU Kwenye jamii zetu tuna viongozi bora kabisa wenye misingi ya siasa safi na Uongozi uliotukuka kabisa. Lakini kundi kubwa la wazee hawa hawajajitoa kuelimisha vijana ama watoto juu ya namna walivyopita wao na kuoata tuzo mbalimbali za uongozi. Nadhani kuna changamoto pia ya kutojifunza mbinu mpya ya urithishaji wa maarifa haya. Mfano: ni viongozi wachache mno wa zamani ambao wanajihusisha na mitandao ya jamii hivyo kuwawia vigumu vijana wengi kupata maandiko ama mafunzo ya uongozi kutoka kwa Viongozi wazuri wa mfano (Role models) wa zamani.
4. KUURITHISHA UPENDO, UKWELI NA UWAZI KWA WATOTO Katika malezi inatubidi tuuoneshe upendo wa kweli kwa watoto wetu, tuwafundishe uzalendo, tuwaelekeze faida za kuwa wakweli, tuwaambie faida za kufanya jambo lolote la umma kwa uwazi mkubwa ili kupunguza mashaka kwa wanajamii. Haya yote huanzia nyumbani haswa kwa sisi walezi/wazazi kwa kuwa mifano bora kwa watoto wetu kwa kuweka tofauti za mahusiano yetu pindi tu linapokuja suala zima la malezi ya watoto.
Kuna namna tunatakiwa kurejea kwenye upendo wa asili, upendo usio na mawaa, upendo wenye kuthamini bindamu wengine. Upendo ambao humfanya binadamu ajisikie vibaya pindi anaposhindwa kumshauri vizuri ama kumsaidia binadamu mwenzake kwa hali na mali pindi anapohitaji msaada wa kimawazo, hali ama mali. Upendo huu utarahisisha kabisa urithishaji wa maarifa kwa yoyote anayekuzunguka bila kuangalia tofauti zetu.
Kwa kuhitimisha, Naamini hakuna mabadiliko chanya yanoyokosa vipingamizi, changamoto na misukosuko. Ili kuyafikia maendeleo endelevu lazima tupate viongozi waliojaa Upendo, Uadilifu, Utu, usawa na wapenda umoja. Na viongozi hawa tunaweza kabisa kuwapata kwa kuwaandaa watoto wetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo. *Mabadiliko huanza na mimi.
Mimi mwalimu ninayejifunza,
Demitria Thomas Gibure.

Upvote
21