Urusi haijasahau ukarimu wake wa nyakati zote kwa Tanzania 🇹🇿 🇷🇺

Urusi haijasahau ukarimu wake wa nyakati zote kwa Tanzania 🇹🇿 🇷🇺

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
The Diplomat

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anaelezea mapokezi ya heshima aliyopata akiwa katika ziara rasmi ya kitaifa nchini Urusi.

Mapokezi aliyopewa Rais Dkt. Samia yanaakisi udugu wa miaka mingi na Taifa la Urusi.

"Urusi ni mshirika wetu mkubwa kuanzia miaka ya 1960, nimekuja kuwahakikishia kuwa Watanzania bado tuna mengi ya kufanya sisi na wao. Kuwahakikishia kwamba Tanzania tumefungua milango, unapofungua milango wa kwanza kumshika mkono ni ndugu yako," anaeleza Rais Dkt. Samia wakati akizungumza na waandishi wa Habari alioandamana nao kwenye ziara hiyo ya kihistoria.

"Ukarimu nilioonyeshwa ni wa kiwango cha mwisho, hata waandishi wa habari wa Urusi na kamera zao walikuwa wakiniamkia kwa Kiswahili, Shikamoo Mama. Kiswahili kinaenea kimepata nafasi," naendelea Rais Dkt. Samia.

Rais wa Urusi, Vladmir Putin ni miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa dunia. Kutokana na ukubwa wa nchi yake kiuchumi, kisiasa na nguvu ya kijeshi duniani.

Kushikwa mkono na Rais Putin
kunamaanisha kushikwa mkono na karibu nusu ya dunia, hasa ikiwa mkono wenyewe ni wa dhati unaotoka moyoni.

Kama ilivyo Mwalimu Nyerere hakujifunga upande mmoja pekee; na kusisitiza sera ya kutofungamana na upande wowote vivyo hivyo Dr. Samia atilia mkazo sera ya Tanzania kuto fungamana na Upande wowote

akizungumza Rais Samia ,” Tanzania tunafata sera ya kutofungamana na Upande wowote na kwa sisi kila anayetaka kufanaya kazi na sisi tunafanya nae, lakini pia tunaswala la Diplomasia ya Uchumi, kila unapoona kuna fursa ya kukuza uchumi wako hiyo fursa tunaitumia.”

Anaendele, “kwa muda mrefu hapa kati Urusi palikua hakuna mambo yanayoendelea baina yake na Tanzania kutokana na sababu kadhaa tumekua tukifanya kazi na wengine. Hatuchagui tunakusanya.”

Ziara hii kwa Ujumla imeonyesha kwa
kiasi kikubwa Jinsi Taifa la Tanzania
linavyoheshimika Duniani na namna Sera ya Diplomasia ya Uchumi inayochagizwa na Mh. Rais Dr. Samia inavyofanya kazi huku akisisitiza msingi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania ya Kutofungamama na Upande wowote.

Ziara hii inaendelea Kufungua fursa
kubwa za Kiuchumi katika sekta
Mbalimbali ikiwemo Nishati, Kilimo, Elimu hasa kwa Vijana , Madini na kadhalika.

Tanzania imeendelea kutumia Diplomasia kama chombo cha kutafuta maendeleo na kulinda maslahi yake ya taifa.

Katika nyakati mbili tofauti za historia mwaka 1969 na mwaka 2026 Urusi imewapokea viongozi wawili wa Tanzania kwa heshima kubwa.

Tofauti kati ya Moscow ya mwaka 1969 na Moscow ya mwaka
2026. Mwalimu Nyerere aliwakilisha Tanzania iliyokuwa ikitafuta njia ya kujenga Ujamaa wa Kiafrika; Rais Dkt. Samia anawakilisha Tanzania inayotafuta nafasi yake katika uchumi wa dunia unaotegemea biashara, uwekezaji na ushindani wa kimataifa.

Miaka 57 Rais Samia avunja ukimya wa Urusi na Tanzania.
IMG-20260607-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom