Urusi imezikatia gesi nchi za Poland na Bulgaria. Putin alivyosema walipe kwa ruble hakuwa anatania

Urusi imezikatia gesi nchi za Poland na Bulgaria. Putin alivyosema walipe kwa ruble hakuwa anatania

Hii imekaa powah sanaa , ajabu utaona wanaanza kulalamika kuwa Urusi kakosea, wakati wanataka kujitoa kutegemea gesi ya Urusi, Putin kawasaidia kujitoa kwa haraka
shida sio serikali inayotaka kujitoa bali shida ni ana mkataba na kampuni ya kipoland so mboyoyo za Putin na Poland zisiingilie mkabata wa kampuni ya gas ya kipoland wao sio sehemu ya serikali wala hawajapewa zuio na serikali kusambaza gas poland
 
Under the Russian payment scheme, energy importers have had to open two bank accounts with Gazprombank — a foreign currency account and a rubles account. The proceeds of sales are paid in foreign currency (dollars or euros) which is then converted by Gazprombank into the ruble account.

Several other countries are reportedly using the scheme. A European Commission document release last week advised that it “appears possible” to comply with the new Russian rules without getting into conflict with EU law.
 
Putin ni bogus, hakuna popote ambapo mkataba unaongelea hayo madafu yake for the terms of payment, tayari wamemwambia akaye na gesi yake kuna sources nyingi.

Kuanzia mwakani atatembeza hiyo gesi kama karanga.
if the agreement requires payment to be made in USD then why US has frozen Russian USD reserves as one of the economic sanctions for Russia??
do you want them to give up their gas for free?
 
Hata sasa hivi inapatikana bei ya kutupwa na wauza gesi za magendo wa kirusi huko deep sea

Ulaya itaingia tu kwa magendo ila vita ikiisha wataipaata kwa bei kama bure
Hii ni habari ya Buza, unafikiri warusi hawana kamera na setillati ya kuona nchi yao.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Putin alichofanya hapa Ni kuwahi TU ili kuogopa fedheha au kuyagawa mataifa ya Ulaya (Divide and Rule)

IKO HIVI

Mkataba wa Poland kununua Gas Urusi unaisha Mwezi Octoba mwaka 2022. Poland imeweka wazi kuwa Baada ya mkataba kuisha haitanunua Gas kutoka Urusi,badala yake itaanza kufungua mabomba ya Gesi ya Kutoka Norway ambayo yalijengwa tangu mwa 2011. Mabomba hayo yalichelewa kufunguliwa kwasababu ya Gharama nafuu ya Gesi ya Urusi dhidi ya Gas ya Norway. Kwahiyo Kitakachobadilika Huko Poland Ni Gharama za Gasi TU na Wala sio kwamba Wataganda kwa kukosa Gasi Kama ninavyoona wengi wakishadidia.

Kuhusu Bulgaria. Hapa Kuna Kichekesho. Bulgaria inaitegemea Gas ya Urusi kwa 97%,Lakini Gasi hiyo inachangia 11% ya vyanzo Vya Nishati nchini Bulgaria. Kila mwaka,Bulgaria Inaagiza kiasi Cha Gasi Cha 111M m^3 kwa Mwaka. Meli kubwa na kubeba LNG inabeba kiasi Cha Gas Cha 260M m^3. Kwamaana hiyo,Bulgaria akipata Oil Tanker Moja ya LNG kutoka Marekani atatumia miaka 2 bila kuhitaji Gasi nyingine. Hapo Ni Bei TU itabadilika na Wala sio kukosekana kwa Gasi.

MAONI YANGU

Tangu tishio la Urusi kukata Gasi kuelekea Ulaya lianze,Mimi niliamua kufuatilia Umuhimu wa Gas ya Urusi barani Ulaya hasa Kiuchumi. Nimekuja Kugundua kwamba,Nchi ya Ujerumani ndio Mateka wa Urusi linapokuja kwenye suala la Gasi. Ujerumani inatumia kiasi kikubwa Cha Gasi kutoka Urusi kuendesha uchumi wake,na mbaya zaidi Hakuna mbadala wa Gasi hiyo. Kwa maana hiyo,Kama Urusi itakata Gasi yake kuelekea Ujerumani,basi hapo Uchumi wa Ujerumani utaingia RECESSION. Na Kwa kuwa Ujerumani ndio yenye Uchumi mkubwa barani Ulaya,Basi Ni wazi Ulaya nzima itayumba Kiuchumi.
Mbona mkuu inasemekana Ujerumani alipunguza uingizwaji wa Gas ya mrusi hivi karibuni?
 
Waliokatiwa Gasi wananunua kiasi Kidogo Sana Cha Gasi ya URUSI na hawana athari Kiuchumi kwa URUSI. Mfano,Bulgaria inatumia $ 50M kwa Mwaka kununua Gasi kutoka Russia. Poland inatumia $ 190M kununua Gasi kutoka Urusi kwa Mwaka. Baba lao Ni Ujerumani. Ujerumani inatumia $ 420M kila siku kununua Gasi ya Urusi. Hiki Ni kiasi kikubwa kwa siku moja,Kwa Mwezi pekee Ujerumani anatumia $ 17B kununua Gas ya Urusi.

MARK MY WORDS

Siku Urusi akiikatia Gas Ujeremani,Basi Uchumi wa Ulaya yote na Urusi utaporomoka kuliko unavyofikilia. Urusi itapoteza 60% ya Mapato kwenye GDP ,Uchumi wa Ujerumani Utasambaratika na Ulaya yote.

Ndio maaana nasema,Urusi atakata Gasi kote Ulaya lakini sio Ujerumani,MARK MY WORDS.
Wewe subiri uje uone hii karata itakavyochezwa mkuu, US kuna kitu hapa atafanya endapo alishakipanga.
 
shida sio serikali inayotaka kujitoa bali shida ni ana mkataba na kampuni ya kipoland so mboyoyo za Putin na Poland zisiingilie mkabata wa kampuni ya gas ya kipoland wao sio sehemu ya serikali wala hawajapewa zuio na serikali kusambaza gas poland
Kwa nini hiyo kampuni haikulipa je huko si kivunja mkataba ⁉️
 
shida sio serikali inayotaka kujitoa bali shida ni ana mkataba na kampuni ya kipoland so mboyoyo za Putin na Poland zisiingilie mkabata wa kampuni ya gas ya kipoland wao sio sehemu ya serikali wala hawajapewa zuio na serikali kusambaza gas poland
Zile mali za Warusi ambao sio za Serikali zilizozuiliwa nazo ukihoji kijinga hivi hivi? Mavi yako
 
if the agreement requires payment to be made in USD then why US has frozen Russian USD reserves as one of the economic sanctions for Russia??
do you want them to give up their gas for free?
US was not party to Russia-Europe Gas Deal.
 
Under the Russian payment scheme, energy importers have had to open two bank accounts with Gazprombank — a foreign currency account and a rubles account. The proceeds of sales are paid in foreign currency (dollars or euros) which is then converted by Gazprombank into the ruble account.

Several other countries are reportedly using the scheme. A European Commission document release last week advised that it “appears possible” to comply with the new Russian rules without getting into conflict with EU law.
View attachment 2203654
Screenshot_20220428-115123.jpg
 
hata Kama yalikuwa ni ya magharibi ,yaliingiaje kufanya biashara urusi!?? walikuwa na mikataba na urusi!! Na walikuwa wanalipa Kodi,hivyo wembe unakata kotekote!! Putin Safi Sana,Katia gesi hao kenge!!! na kipindi Cha kuganda ndo kimeingia,watageuka barafu kenge hao!!
Nilipofika hiyo sentensi ya mwisho ya "kipindi cha kuganda kimeanza" ndiyo nikajua kumbe hata hujui majira ya Nchi hizo.Wenzio wanaelekea kwenye summer wewe unasema wataganda [emoji3]
 
Waliokatiwa Gasi wananunua kiasi Kidogo Sana Cha Gasi ya URUSI na hawana athari Kiuchumi kwa URUSI. Mfano,Bulgaria inatumia $ 50M kwa Mwaka kununua Gasi kutoka Russia. Poland inatumia $ 190M kununua Gasi kutoka Urusi kwa Mwaka. Baba lao Ni Ujerumani. Ujerumani inatumia $ 420M kila siku kununua Gasi ya Urusi. Hiki Ni kiasi kikubwa kwa siku moja,Kwa Mwezi pekee Ujerumani anatumia $ 17B kununua Gas ya Urusi.

MARK MY WORDS

Siku Urusi akiikatia Gas Ujeremani,Basi Uchumi wa Ulaya yote na Urusi utaporomoka kuliko unavyofikilia. Urusi itapoteza 60% ya Mapato kwenye GDP ,Uchumi wa Ujerumani Utasambaratika na Ulaya yote.

Ndio maaana nasema,Urusi atakata Gasi kote Ulaya lakini sio Ujerumani,MARK MY WORDS.
Mkuu,hapa kwenye swala la gesi utachoka tu kuwaelewesha,watu wenyewe ndiyo hawa bila aibu mtu anasema "kipindi cha baridi kali kimeanza,wataganda" unabaki unajiuliza kama huyu mtu hata kujua majira katika hizo Nchi hajui itakuwa hii complex issue ya gas.
 
elewa urusi alikuwa hauz direct kwa serikali ya poland bali anafanya biashara na kampuni ya kipoland so kampuni ndo inaishitaki urusi kwa kuvunja mkataba

Hata kama,, hawana ubavu wa kumshitaki urusi,, watulie tu otherwise kitawakuta kama Ukraine
 
Russia yawakatia gesi Wapoland, sarafu za Euro na Pound ya Uingereza zaporomoka

Sarafu za Euro na Pound ya Uingereza zimeporomoka thamani yake baada ya Russia kuamua kuzikatia gesi nchi za Poland na Bulgaria kutokana na kufuata kwao kibubusa siasa za Magharibi.

Hayo yameripotiwa na televisheni ya Euro News ambayo imesema kuwa, sarafu ya Euro imeporomoka mbele ya dola ya Marekani baada ya Russia kuzikatia gesi Poland na Bulgaria. Thamani ya Euro imeporomoka kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Pound ya Uingereza pia imeporomoka mbele ya sarafu ya dola kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita baada ya Russia kuamua kusimamisha kupeleka gesi yake katika nchi mbili za Poland na Bulgaria za mashariki mwa Ulaya.

Bei ya gesi katika nchi za Ulaya jana Jumatano iliongezeka kwa zaidi ya asilimia 23 baada ya kuchukuliwa hatua hiyo ya Russia ikiwa ni kujibu vikwazo vya Magharibi dhidi ya Moscow.

Nchi za Ulaya ni tegemezi mno kwa nishati ya Russia

Hatua hiyo ya Russia imechukuliwa baada ya msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia kusema kuwa nchi za Magharibi zinachuana kutuma silaha Ukraine. Maria Zakharova ameashiria madai ya nchi za Magharibi kwamba zinafanya juhudi kurejesha amani huko Ukraine na kusisitiza kuwa: "Hatua hii ya Magharibi inakinzana na matamshi ya nchi hizo."

Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameongeza kuwa, nchi za Magharibi zinafanya kila kinachowezekana ili kuchelewesha oparesheni amilifu ya jeshi la Russia nchini Ukraine.

Ikumbukwe kuwa, juzi Jumanne, Christine Lambrecht Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani alisema kuwa, Berlin itatoa kibali cha kuikabidhi Ukraine vifaru; hatua inayodhihirisha kubadilika wazi sera za tahadhari za Berlin katika suala la kuiunga mkono kijeshi serikali ya Kiev.
 
Back
Top Bottom