Putin alichofanya hapa Ni kuwahi TU ili kuogopa fedheha au kuyagawa mataifa ya Ulaya (Divide and Rule)
IKO HIVI
Mkataba wa Poland kununua Gas Urusi unaisha Mwezi Octoba mwaka 2022. Poland imeweka wazi kuwa Baada ya mkataba kuisha haitanunua Gas kutoka Urusi,badala yake itaanza kufungua mabomba ya Gesi ya Kutoka Norway ambayo yalijengwa tangu mwa 2011. Mabomba hayo yalichelewa kufunguliwa kwasababu ya Gharama nafuu ya Gesi ya Urusi dhidi ya Gas ya Norway. Kwahiyo Kitakachobadilika Huko Poland Ni Gharama za Gasi TU na Wala sio kwamba Wataganda kwa kukosa Gasi Kama ninavyoona wengi wakishadidia.
Kuhusu Bulgaria. Hapa Kuna Kichekesho. Bulgaria inaitegemea Gas ya Urusi kwa 97%,Lakini Gasi hiyo inachangia 11% ya vyanzo Vya Nishati nchini Bulgaria. Kila mwaka,Bulgaria Inaagiza kiasi Cha Gasi Cha 111M m^3 kwa Mwaka. Meli kubwa na kubeba LNG inabeba kiasi Cha Gas Cha 260M m^3. Kwamaana hiyo,Bulgaria akipata Oil Tanker Moja ya LNG kutoka Marekani atatumia miaka 2 bila kuhitaji Gasi nyingine. Hapo Ni Bei TU itabadilika na Wala sio kukosekana kwa Gasi.
MAONI YANGU
Tangu tishio la Urusi kukata Gasi kuelekea Ulaya lianze,Mimi niliamua kufuatilia Umuhimu wa Gas ya Urusi barani Ulaya hasa Kiuchumi. Nimekuja Kugundua kwamba,Nchi ya Ujerumani ndio Mateka wa Urusi linapokuja kwenye suala la Gasi. Ujerumani inatumia kiasi kikubwa Cha Gasi kutoka Urusi kuendesha uchumi wake,na mbaya zaidi Hakuna mbadala wa Gasi hiyo. Kwa maana hiyo,Kama Urusi itakata Gasi yake kuelekea Ujerumani,basi hapo Uchumi wa Ujerumani utaingia RECESSION. Na Kwa kuwa Ujerumani ndio yenye Uchumi mkubwa barani Ulaya,Basi Ni wazi Ulaya nzima itayumba Kiuchumi.