Urusi kaonesha mfano mbaya, Venezuela naye anafuata: Dunia inaanza kuharibika

Urusi kaonesha mfano mbaya, Venezuela naye anafuata: Dunia inaanza kuharibika

Issue kubwa ni hii tabia mbaya kuvamia majirani na kujimegea ardhi zao. Urusi ni nchi yenye ardhi kubwa sana kuliko nchi nyingine yoyote duniani, lakini bado wana tamaa ya kujimegea ardhi kutoka nchi ndogo kama Ukraine. Dunia tunaelekea pabaya!
Wewe unafikiri watu wanataka Ardhi???Nenda kachimbe zaidi...sababu sio nyepesi kama unavyoongea wewe
 
Urusi imeonyesha mfano kuwa taifa moja linaweza kumega ardhi ya Taifa jingine na kuifanya yake, Venezuela naye sasa anafuata, anataka kumega nusu ya Guiyana ajichukulie. Hii lawlessness itaishia wapi, Je Tanzania nasi tujitwalie Burundi na Rwanda zote kwa vile wakati wa Mjerumani tulikuwa nchi moja?
Labda Venezuela lkn Russia yuko sahihi ijapo sijui unafikiri ni kwa nini Russia imelazimikia kufanya hivyo.
 
Upo
pk mwenyewe anatamani walau aichukue karagwe na ngara na huko goma mashariki mwa kongo tz itawezaje kuitwa rwanda na burundi? Kwanza tz haina tamaa ya kujiongezea maeneo kwenye nchi za watu ila wakileta uchokozi wanavamiwa tu na kuzimega hizo nchi.
Kwel kbs,mwaka 2007 nilikuwa Rwanda nilinunua gazeti la newtimes.muhariri aliweka kichwa Cha Habari kuwa kujiunga kweku EA Wacha waturudishie ardhi yao.sasa Habari yenyewe walizungumzia wilaya ya karagwe na ngara jinsi ilivyo na ukaribu na kifanana mazingira mpk majina na vitu vingi tu pia akazungumzia mashariki ya Drc mpk majina ya miji na vitongoji vinamausiano na Rw.hivyo ndoto ya muhariri kuwa vitarudi kwao.toka siku hiyo nikawa nafuatilia Hilo gazeti maana ni la serikali.washenz sn
 
Ila Uingereza kuvikalia visiwa vya Falk Island ni sawa?

Ufaransa mpaka Leo kuishikilia Mayotte ni sawa?

Marekani na Hawaii, unataka kusema nini?

Israel na maeneo ya Wapalestina?

China na Tibet, Xinjiang, Macau?

Angola na Jimbo la Kabinda?

Wewe kwa maono yako mafupi unazani yameanza kutokea Jana?

Dunia haipo fair na mwenye nguvu ndio mtawala.
Mkuu raia wote wa mayotte wanafurahi na kuridhika kuwa ufaransa.
 
Ila Uingereza kuvikalia visiwa vya Falk Island ni sawa?

Ufaransa mpaka Leo kuishikilia Mayotte ni sawa?

Marekani na Hawaii, unataka kusema nini?

Israel na maeneo ya Wapalestina?

China na Tibet, Xinjiang, Macau?

Angola na Jimbo la Kabinda?

Wewe kwa maono yako mafupi unazani yameanza kutokea Ja

Dunia haipo fair na mwenye nguvu ndio mtawala.
Hao ndio waliogawa mataifa na pia kujigawia ingawa mataifa mengi yalikuwa mamoja
Angalia kuna Guayana city, Venezuela na Guyana ni ndugu zao na walikuwa wamoja
Acha wawasogeze ndugu zao tu hata mimi naona sawa tu

Na sisi tujiongeze hao jirani kina Slim na mwenzake ila tatizo la zitto kuwatetea kila siku liishe
Kutwa Uhamiaji kuwatishia maisha maana naona hata lugha wanaelewana vizuri sana
Kila leo maneno sasa tujipange kwa miaka kadhaa halafu tuwabade kama panzi tu
Tena hao watafurahi sana maana watapata pa kulima na kufuga
 
Tusiidharau Rwanda eti kwa sababu ni "kanchi kadogo," tunajidanganya. Vita vya siku hizi ushindi wake unategemea sana Ubora/ Viwango vya Sayansi na Teknilojia na ubora wa akili wa akili walizonazo wapiganaji lakini siyo ukubwa wa nchi au wingi tu wa wapiganaji. Mfano mzuri ulio hai ktk hili ni nchi ndogo ya Israeli ambayo inasumbua mataifa mengi majirani zake.
Usisahau huyo unayemtolea mfano, nyuma yake ipo nchi kubwa kum-back up.

Acheni ku-overrate Rwanda kiasi hiko mzee. Hamna lolote la kuitisha Tz.
 
Back
Top Bottom