Urusi kaonesha mfano mbaya, Venezuela naye anafuata: Dunia inaanza kuharibika

Urusi kaonesha mfano mbaya, Venezuela naye anafuata: Dunia inaanza kuharibika

Una capacity ndogo sana kuajdiliana na mimi kwenye swala lolote iwapo unaanza kuniita mpumbavu. Kajifuze namna ya kujenga hoja kuliko kutumia matusi. Nimekuwapo hap JF zaidi ya miaka 16, ninajua matusi sana ila leo sitatumia lugha ya matusi kwako ila ninakushauri utafute watu wenye lugha za matusi huwa ninawajibu vipi; tena kwa lugah chafu kas=bisa kuliko walizotumia kwangu. Halafu uje unijibu kabisa sitakujibu rasmi kwa hii post hii.
Hakuna mahali nimekuuliza wewe upo JF muda gani ? acha kuleta vijihoja visivyo kuwa na maana tubaki kwenye topic
 
Urusi imeonyesha mfano kuwa taifa moja linaweza kumega ardhi ya Taifa jingine na kuifanya yake, Venezuela naye sasa anafuata, anataka kumega nusu ya Guiyana ajichukulie. Hii lawlessness itaishia wapi, Je Tanzania nasi tujitwalie Burundi na Rwanda zote kwa vile wakati wa Mjerumani tulikuwa nchi moja?
Mwarabu nae kajimegea loliondo na Ngorongoro kwa kuwafukuza wenyeji wamasai.
Sasa hivi dunia ni vululu vululu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dalali lama ni kiongozi wa dini na pia alikuwa ni land lord.

Tibet ni sehemu ya China kabla hata wazungu hawajapanda meli kwenda kuvamia North America.
Kwani huju pia kuwa Vatican City inaongozwa na Pope wa kikatoliki na ina mabalozi karibu dunia nzima?
 
Hauna mahali nimekuuliza wewe upo JF muda gani ? acha kuleta vijihoja visivyo kuwa na maana tubaki kwenye topic
Bado niakusubiri kabla sijakurushia matusi ya nguoni na wewe baada ya kuniita mimi mpumbavu badala ya kujadili mada iliyoko mbele yetu. Hujakiri kuwa hukuniita mpumbavu kwa makusudi ila uliteleza ulimi tu.
 
Kwani huju pia kuwa Vatican City inaongozwa na Pope wa kikatoliki na ina mabalozi karibu dunia nzima?
Nimekuambia dalai lama alikuwa kiongozi wa dini na land lord.

Hiyo ya utaifa toka lini ? Mpaka sasa hujanijibu
 
Tusiidharau Rwanda eti kwa sababu ni "kanchi kadogo," tunajidanganya. Vita vya siku hizi ushindi wake unategemea sana Ubora/ Viwango vya Sayansi na Teknilojia na ubora wa akili wa akili walizonazo wapiganaji lakini siyo ukubwa wa nchi au wingi tu wa wapiganaji. Mfano mzuri ulio hai ktk hili ni nchi ndogo ya Israeli ambayo inasumbua mataifa mengi majirani zake.
Kijeshi Rwanda tumeizidi mbali sana. Kama Rwanda inashindwa kuimega DRC itaweza kuimega Tz?
Kuhusu Israel haina nguvu za kuyahenyesha mataifa ya mashariki ya kati, isipokuwa Israel ni taifa lililoundwa na UK na USA ili kulinda maslahi yao hapo mashariki ya kati. Ndio maana wakati wowote ambapo Israel inaingia vitani utaona misaada inayomiminwa hapo. Mfano mzuri ni hii vita ya Israel na Hamas, Israel kupigana tu na wanamgambo anagalia ndege za kijeshi zilizotua hapo kutokea UK na USA kupeleka misaada mpaka Ukraine imesahaulika. Je, Israel ingepigana na nchi kama Iran si lingekuwa balaa zito?
 
Wana Jf, Marekani iliivamia Iraq "kihalali". Hivyo kosa la Urusi ni kutotumia kidude kinachoitwa UN kuhalalisha kuivamia Ukraine.

Funzo kwenu wanajf ukitaka kujichukulia sheria mkononi kimataifa "kihalali" basi kitumie kidude UN. Mmeelewa?

Hii imenikumbusha satire ya yule Comedian Bassem Youssem alipowakejeli baadhi ya Pro-zionists pale aliposema "IDF ndio jeshi pekee duniani linalowaonya raia kabla ya kuwapiga mabomu! Ni jambo zuri lilioje hilo!.. Hivyo kwa mantiki hiyo hata majeshi ya Urusi kama yatawaonya na kuwapa tahadhari raia wa Ukraine kabla ya kulipua majumba yao basi tuko poa tu na Putin sio?, Habibi umeshawaonya vamia tu"
Acha kusema uwongo hapa marekani alivamia Iraq kihalali kwa amri ya nani? Weka ushahidi hapa. UN ilithibitisha Iraq hakua na silaha za maangamizi lakini marekani alitumia nguvu kuivamia Iraq na kumuua Sadam hussein.
 
Ila Uingereza kuvikalia visiwa vya Falk Island ni sawa?

Ufaransa mpaka Leo kuishikilia Mayotte ni sawa?

Marekani na Hawaii, unataka kusema nini?

Israel na maeneo ya Wapalestina?

China na Tibet, Xinjiang, Macau?

Angola na Jimbo la Kabinda?

Wewe kwa maono yako mafupi unazani yameanza kutokea Jana?

Dunia haipo fair na mwenye nguvu ndio mtawala.
Unadhani hayo ya uk us france nk mtoa mada hayajui anayajua sana
Ila kwao west hata wakifanya ovu gani wanakua wamefanza jema
Nandio maana nikamwambia nayeye na nchi yake kama anaweza wavamie huko wanapotaka baadae hatutaki lawama
Anadhani kama watu wote humu wajinga hatujui kama haya ya papa kumla dagaa na kibua hayajaanzja Crimea 2014 kwa Russia na ukraine wala hayajaendelea mwisho kwa ukraine na Russia mwaka 2022 na wala hayataishia kwa Venezuela mwaka 2023
Venezuela nipo nyuma yako vamia tu mzee baba
 
Mtazamo mfupi huo uliojaa mawazo ya ugombea uhuru wa miaka sitini; Uingereza, Ufaransa na Israel wamevamia nchi gani. Mgawanyo wa ardhi baina ya Israel na Palestina ulifanywa na Umoja wa mataifa mwaka 1947 kufuatia mapendekezo ya United Nations Special Commission on Palestine. Waarabu wengine hawataki kuwapo kwa Tiafa la Israel, na ndiyo maana ya mgogoro huo. Wangetambua tu mipaka hiyo iliyowekwa na umoja wa mataifa kama Tanganyika ilivyotambua mipaka baina yake na nchi za Rwanda na Burundi ambayo iliweka na umoja wa mataifa baada ya vita ya kwanza, kusingekuwapo mgogoro.
Boss wewe unazungumzia Ramani ya 1947 mbona mwaka 1967 Israel iliiteka milima ya Golan ambayo ni sehemu ya nchi ya Syria na hakuna anayeibughudhi Israel kuikalia milima hiyo?
 
Issue kubwa ni hii tabia mbaya kuvamia majirani na kujimegea ardhi zao. Urusi ni nchi yenye ardhi kubwa sana kuliko nchi nyingine yoyote duniani, lakini bado wana tamaa ya kujimegea ardhi kutoka nchi ndogo kama Ukraine. Dunia tunaelekea pabaya!
Mumeiona Russia tu mlivyokua mnajitoa ufaham
Yaani mnajifanya munajua tabia mbaya wakifanya msio wapenda ila mnao wapenda hamjawahi kuwaambia kama wanafanya tabia mbaya
Kwani lini mliwahi kukemea us kuikalia Cuba
Nasema tena Venezuela mega ukiwa mpaka unapoona panatosha
 
Hivi unaielewa Rwanda vuzuri?
Tz inaweza kuishia kumegwa kilaini tu
Haya Mawazo mlikuwa nayo Kwa Israel Lakini kile kikundi tu kule Gaza Mziki.Msiikuze Rwanda kiivyo baadae mkakimbilia haki za binadamu.Huyo PK anajua pa kuchovya mikono Tz athubutu.
 
Hakuanza Urusi alianza baba lao US na wapambe wake. Wamefanya hivyo nchi nyingi tu wakiondoa tawala zilizopo na kuzikalia nchi kimabavu. Sijui ni kitu gani huwa kinawafanya muone US anachofanya ni sawa ila wengine si sawa.
Nchi zote ziliundwa kimabavu miaka hiyo hata Tanganyika bila ubabe wa mjeruman haipo. kwa sasa mfumo wa dunia ni tofauti.
 
Nchi zote ziliundwa kimabavu miaka hiyo hata Tanganyika bila ubabe wa mjeruman haipo. kwa sasa mfumo wa dunia ni tofauti.
Sio miaka hiyo nchi za America Kusini zilikuwa tayari zinajitawala achana na mambo ya miaka 1880 huko.
Vipi Iraq maana hili limetokea hapa miaka 2000s
 
Back
Top Bottom