Urusi kujaribu silaha mpya za nyuklia muda wowote Marekani akifanya hivyo

Urusi kujaribu silaha mpya za nyuklia muda wowote Marekani akifanya hivyo

HERY HERNHO

Senior Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
110
Reaction score
458
Rais wa Urusi Vladimir Putin amekuwa akilihutubia Bunge la la nchi hiyo.

Ametumia mwanzo wa hotuba yake kurudia nadharia ambazo amekuwa akitumia mwaka mzima uliopita: anadai kuwa ni Washington ambayo "ilianzisha vita" na mapema mwaka 2022 iliitaka Ukraine kushambulia Crimea na Sevastopol.

Urusi, kulingana na Putin, "ilitumia na inaendelea kutumia nguvu kukomesha vita," ambayo inadaiwa kuanzishwa nchi za Magharibi.

Putin alisema kuwa mnamo 1939 " Nchi za Magharibi zilitoa nafasi" kwa wanajeshi wa Ujerumani ya Wanazi, na sasa inaendeleza "upinzani dhidi ya Urusi."

Putin pia alisema kwamba alama za kijeshi za Wanazi zinadaiwa kutumiwa kwa wingi nchini Ukraine, na nchi za Magharibi "hazijali ni nani anashiriki katika vita dhidi ya Urusi''

''Hakuna mtu katika nchi za Magharibi anayezingatia majeruhi ya binadamu, kwa sababu matrilioni ya dola yamo hatarini," Putin alisema.

Kuhusu masuala ya uchumi Putin anasema anataka kujenga mfumo salama wa malipo ya kimataifa ambao utapunguza utegemezi kwa nchi za Magharibi.

“Hatupaswi kurudia makosa yetu. Tusiharibu uchumi wetu”.

Anasema vikwazo vya Magharibi vilivyopangwa kuwafanya watu wa Urusi "kuteseka" havijafaulu, na anadai sarafu ya rubles ya Urusi "imeongezeka mara mbili" katika soka la kimataifa.

b515a785-66e6-4633-b596-0e022458f8cc.jpg
Chanzo BBC SWAHILI
 
Licha kwamba Urusi iko katika dhiki kubwa na imezika wanajeshi wengi sana, ila ni ujinga kama raisi wa nchi kuonyesha udhaifu, uwoga na hofu itokanayo na mataifa mengine anapohutubia hata kama mambo ni magumu zaidi!

Ni lazima ajitie moyo na kuwafariji wananchi licha kuwa wanaumia sana na vita hivi
 
Last kicks of the dying horse 🐴 one year on, the belligerent Russians have completely failed to achieve their goal of deposing the Ukrainian government a situation that has resulted into losing much of their soldiers and resorting to using para military force and the prison inmates.
 
Last kicks of the dying horse [emoji206] one year on, the belligerent Russians have completely failed to achieve their goal of deposing the Ukrainian government a situation that has resulted into losing much of their soldiers and resorting to using para military force and the prison inmates.
SMO inaendelea kama ilivyo pangwa
 
Last kicks of the dying horse [emoji206] one year on, the belligerent Russians have completely failed to achieve their goal of deposing the Ukrainian government a situation that has resulted into losing much of their soldiers and resorting to using para military force and the prison inmates.
Lala kijana kwa kingereza chako cha kuiba malengo hubadilika kulinga na wakati wale si mbulula kama viongozi wa nchi yako hii
 
Ametumia mwanzo wa hotuba yake kurudia nadharia ambazo amekuwa akitumia mwaka mzima uliopita: anadai kuwa ni Washington ambayo "ilianzisha vita" na mapema mwaka 2022 iliitaka Ukraine kushambulia Crimea na Sevastopol.

Urusi, kulingana na Putin, "ilitumia na inaendelea kutumia nguvu kukomesha vita," ambayo inadaiwa kuanzishwa nchi za Magharibi.
Putin anakomesha vita kwa kuendeleza vita ?...
 
Licha kwamba Urusi iko katika dhiki kubwa na imezika wanajeshi wengi sana, ila ni ujinga kama raisi wa nchi kuonyesha udhaifu, uwoga na hofu itokanayo na mataifa mengine anapohutubia hata kama mambo ni magumu zaidi!

Ni lazima ajitie moyo na kuwafariji wananchi licha kuwa wanaumia sana na vita hivi

Vita ni vita mura, hakuna vita ndogo wala kubwa.
 
Tatizo ni pride, hii ndo inamfanya Putin asisitishe vita hataki surrender kama 1991
Akikubali shindwa maana yake kuna nchi kibao zitamdindia

On the other hand yupo China anasoma mchezo kabla hajaivamia Taiwan
 
Back
Top Bottom