Tangu Urusi aivamie Ukraine Feb 2022 ni miezi 15 sasa, kuna mengi tumeona na kusikia kwa kila upande katika uwanja wa vita.
Kuna maeneo matano (5) ambayo Urusi na Ukraine wameyafanya kuwa ni ngome za mapigano. Miji hii ni Bakhmut, Soledar, Avdiivka, Kreminna na Vuhledar.
Katika miji hii miwili tu ndo imekuwa maarufu zaidi ambayo ni Bakhmut na Soledar. Hii ni kwa sababu ina umuhimu wake katika medani za kivita. Miji hii ni millitary strategic positions.
Urusi iliwekeza nguvu kubwa sana Bakhmut na Soledar, kwa maana ya millitary equipments na personnel. Waliwekeza nguvu kubwa kwa sababu waliamini kuwa wakiiteka Soledar na Bakhmut basi itakuwa rahisi kwao kusonga mbele kwenye miji mingine muhimu kama Slovyansk, Kramatorsk, Sivers'k, na Kostyantynivka. Bakhmut ndio Center (Military Hub) ya kuifikia miji hii sababu ni makutano ya njia kuu kutoka Horlivka, Luhans'ke, Popasna na Lysychans'k.
Urusi Kuichukua Bakhmut na Soledar kajihakikishia kuwa supply logistic (kwa barabara na Reli) itakuwa imara kwenda frontline.
Ni kweli Bakhmut na Soledar ziko mikononi mwa Urusi kwa 100% hilo halina ubishi, akibisha mtu basi ujue tangu akiwa tumboni alikuwa mbishi. Lakini ukweli ni kwamba Hasara ni kubwa kuliko Faida aliyopata.
Nakiri kuwa pande zote mbili zimepoteza resources kubwa (military equipment and personel). Lakini zaidi Urusi imepoteza wanajeshi wake wengi zaidi ya 30,000 waliokufa achilia mbali majeruhi kwa eneo dogo lenye jumla ya SQKM 53.9. Bakhmut ina SQKM 41.6 na Soledar 12.3. Bado nasisitiza Hasara aliyopata Urusi ni kubwa kuliko Faida aliyopata.
Kuna maswali mengi ya kujiuliza. Mimi nitauliza maswali machache na mengine mtaongezea;
1. Nguvu kubwa na rasilimali aliyowekeza Urusi kwa miezi 15 kwa Bakhmut na Soledar zenye eneo la jumla ya SQKM 53.9 zimempa hasara au faida?
2. Kama anaweza kupigana kwa miezi 15 na kufanikiwa kuchukua eneo la SQKM 53.9 ambao ni wastani wa SQKM 3.6 kwa mwezi. Itamchukua muda gani kuichukua Ukraine yote kwa eneo ambalo hajalichukua zaidi ya SQKM 482,960 ?
3. Kama imemchukua miezi 15 kuichukua Bakhmut na Soledar tu kwa direction ya Donetsk ni kweli ataweza kuichukua miji ya Slovyansk, Kramatorsk, Sivers'k, na Kostyantynivka, ukizingatia kuwa kila siku Ukraine wanazidi kuimarisha frontline na anga lao?
4. Urusi ataweza kuishikilia Bakhmut na Soledar kwa miezi 3 ijayo.? Au utakuwa ni ushindi wa muda kama ilivyokuwa Kwa Kherson city, Kharkiv na maeneo mengine?
5. Kwa kuwa Prigozhin amesema tarehe 25/05/2023 atawaachia Russian Regular troops ili wakapate mapumzika na mafunzo zaidi. Je, Russia regular troops watamudu peke yao kuushikilia mji wa Bakhmut bila Wagner?