Urusi: Mwana kayataka, Finland na Sweden wamekidhi vigezo vya NATO

Urusi: Mwana kayataka, Finland na Sweden wamekidhi vigezo vya NATO

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Urusi alijaribu kuparamia Ukraine kisa hakutaka wajiunge NATO, sasa ndio kama kafungulia lango kuu, maana Finland na Sweden sasa wameruhusiwa kujiunga NATO, wamekidhi vigezo, ifahamike Finland ina mpaka na Urusi wenye kilomita 1,271.8 km, hiyo ni zaidi ya umbali wa Dar hadi Kigoma au Dar hadi Mwanza au Bukoba, yaani hata umbali wa Dar hadi Kigali bado haujakidhi urefu huo.

Kwa kifupi, NATO ndio kama wamefika mpakani kwa Urusi, na ifahamike sheria za NATO, Urusi hawezi kujichanganya au kujisahau akashambulia hata kakijiji kamoja tu ndani ya mwanachama wa NATO, yeye Urusi ana hulka ya kudhulumu majirani lakini huwa ako makini sana kwa vitaifa vilivyo na uanachama NATO.

xVxyj8NB_T1o4GH7qwmrrNz04DNwQshU1R1xQibuzyk.jpg

=============================

NATO head Jens Stoltenberg said Finland and Sweden had fulfilled the conditions for joining the military alliance, although Turkey said it is not yet possible to judge if the July agreement has been fully implemented.
NATO Secretary General Jens Stoltenberg said on Thursday that Sweden and Finland were ready to join the military alliance.

Stoltenberg said the two Nordic states had delivered on Turkey's demands, paving the way for accession.

"It's time to welcome Finland and Sweden as members of NATO," he told a press conference alongside Turkish Foreign Minister Mevlut Cavusoglu in Istanbul.

"In these dangerous times it is even more important to finalize their accession, to prevent any misunderstanding or miscalculation in Moscow," Stoltenberg added.
 
Kwa hiyo zitafikia nchi 32 dhaifu kijeshi zimeungana ili kupambana na mwanaume mmoja akichukia?
Ndiyo maana mpuuzi mmoja akisema Urusi ni dhaifu au nchi ya kawaida namtoa maanani.
Urusi ndiye Super power wa ukweli na ndiyo maana nchi dhaifu myingi zinaamua kushirikiana kujilinda dhidi yake.
 
Kwa ambavyo ameteswa na kataifa kadogo Ukraine, binafsi sioni tija hata ya kujiunga NATO, sema tu manyuklia yake ndio shida, vinginevyo ni boya tu.
 
Urusi alijaribu kuparamia Ukraine kisa hakutaka wajiunge NATO, sasa ndio kama kafungulia lango kuu, maana Finland na Sweden...
Ili Mchakato wa Finland na Sweden wa kujiunga NATO ukamilike basi lazima Mabunge yote 30 ya nchi wanachama yapige kura ya kuidhinisha uanachama wa mataifa hayo. Kati ya Mataifa 30 mpaka Sasa Ni Mataifa 2 tu ambayo hayajaidhinisha rasmi uanachama wa Finland na Sweden. Mataifa hayo Ni Hungary na Uturuki. Mataifa hayo ikumbukwe kwamba Ni maswahiba wa Putin na ndiyo yanakwamisha Mchakato.

Juzi Wizara ya Ulinzi ya Marekani imeidhinisha Uuzwaji wa Makombora ya masafa marefu kwa Finland,na wakati huo huo Finland ikasema itakuwa tayari kuruhusu Marekani kuweka Makombora yake ya Nyuklia kule Finland. Sasa huenda haya yote Ni maandalizi ya nchi hizo kupokelewa rasmi kwenye muungano wa NATO.
 
Kwa hiyo zitafikia nchi 32 dhaifu kijeshi zimeungana ili kupambana na mwanaume mmoja akichukia?
Ndiyo maana mpuuzi mmoja akisema Urusi ni dhaifu au nchi ya kawaida namtoa maanani.
Urusi ndiye Super power wa ukweli na ndiyo maana nchi dhaifu myingi zinaamua kushirikiana kujilinda dhidi yake.
Hata Digidigi akijiingiza kwenye Target hushambuliwa na Simba zaidi ya 10 Hadi kifo na kufanywa kitoweo. Hiyo haimaanishi kwamba Simba mmoja atamshindwa Digidigi mmoja Bali Ni katika Kuonesha Ni jinsi gani Simba wanaweza kushirikiana hata kwa Jambo Dogo.
 
Kwa hiyo zitafikia nchi 32 dhaifu kijeshi zimeungana ili kupambana na mwanaume mmoja akichukia?
Ndiyo maana mpuuzi mmoja akisema Urusi ni dhaifu au nchi ya kawaida namtoa maanani.
Urusi ndiye Super power wa ukweli na ndiyo maana nchi dhaifu myingi zinaamua kushirikiana kujilinda dhidi yake.
Hiyo ndio tafsiri!
 
Back
Top Bottom