Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Russia na China wameendelea na mazoezi ya pamoja yanoitwa Vostok 2022 ambayo yajumuisha nchi zingine zipatazo 12.
Mazoezi hayo yaendelea huku bado kukiwa na vita ya Russia na Ukraine pamoja na mgogoro wa China na Marekani kuhusu kisiwa cha Taiwan.
Mazoezi hayo yaloanza Alhamisi ilopita yanatarajia kukamilika jumatano ijayo yajumisha nchi za India, Mongolia, Belarus, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Armenia, Azerbaijan, Tajikistan, Laos, Nicaragua, Syria, na Algeria.
Mazoezi hayo yafanyikia eneo la mashariki mwa Russia na bahari ya Japan na vikosi vya majeshi vipatavyo 50,000 silaha 500 ndege za kivita 140 na meli za kivita 60 na yasimamiwa na mnadhimu mkuu wa majeshi ya Russia jenerali Valery Gerasimov.
Mazoezi haya ni yamepunguza idadi ya majeshi kulinganisha na mazoezi yalofanyika mwaka 2018 ambapo majeshi yapatayo 300,000 yalifanyika. Ushirikiano huu wa sasa kati ya Russia na China unafanya mazoezi ya safari hii kushirikisha vikosi vya China vipatavyo 2000, magari ya kivita 300, ndege za kivita 21 na meli tatu za kivita.
Akizungumzia mazoezi hayo naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia bwana Alexander Fomin amesema mazoezi haya yalenga kulinda mawasiliano ya baharini, maeneo yenye shughuli za kiuchumi baharini na maeneo yote ya pwani za bahari.
Hii ni mara ya kwanza kwa China kutuma sehemu tatu za jeshi lake yaani ardhini, majini na angani kwenye mazoezi ya aina hiyo wakisaidiana na Russia ambayo ndo kiongozi wa operesheni hiyo na ni hatua inoonyesha ushirikiano wa karibu na wa ndani pamoja na kuaminiana.
Kuthibitisha hilo, China haijaikosoa Russia hadharani pale Russia ilipoivamia Ukraine mwezi Februari mwaka huu na badala yake kuilaumi Marekani na NATO kwa kuichokoza Russia na pia vikeazo vya kiuchumi ambavyo Marekani na NATO wameviwelka dhidi ya Russia.
Wachambuzi wasema, uhusiano huu wa China na Russia wadhamiria kuionyesha Marekani kuwa ikizidisha changamoto kwake basi haitakuwa na namna bali kuimarisha ushirikiano wa kijeshi kati yake na Russia.
Marekani imelaumu mazoezi hayo kwa kudai kuwa maziezi ya aina hiyo hayapaswi kufanywa ndani ya mipaka au nje ya mipaka yao.
Source: News 360, China Global Times.