Mwanamkiwi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 2,023
- 2,402
Uvamizi wa Ukraine pamoja na maelezo ya rais wa Urusi ni jaribio la kuanzisha ukoloni mpya. Nchi nyingi zinadai Urusi itoke tena katika nchi jirani na kulipia fidia.
Balozi wa Kenya alihotubia Umoja wa Mataifa akilaumu matendo ya Urusi. Tanzania ni kimya. Kwa nini?
Serikali haielewi ni nini kinachoendelea?
Serikali haijali kinachoendelea (kinyume na hotuba zote eti taifa linapinga ukoloni na kujivunia) ?
Serikali inaogopa kusema kitu kuhusu rafiki wa China?
Watasema tanzania ni huru hatulazimishwi kuwa upande fulani,ni wanafiki wa kiwango cha juu kwelikweli.Uvamizi wa Ukraine pamoja na maelezo ya rais wa Urusi ni jaribio la kuanzisha ukoloni mpya. Nchi nyingi zinadai Urusi itoke tena katika nchi jirani na kulipia fidia.
Balozi wa Kenya alihotubia Umoja wa Mataifa akilaumu matendo ya Urusi. Tanzania ni kimya. Kwa nini?
Serikali haielewi ni nini kinachoendelea?
Serikali haijali kinachoendelea (kinyume na hotuba zote eti taifa linapinga ukoloni na kujivunia) ?
Serikali inaogopa kusema kitu kuhusu rafiki wa China?
Na kweli hili somo, inaonekana wewe hukuelewa kabisa.Sijui washuleni siku hizi watoto wanafundishwa nini? Enzi za nyerere mtoto wa primary anajua "Seea yetu ya nje ni Sera ya kutofungamana na upande wowote" yaani Tanzania hatuchaguliwi "Nani awe rafiki na nani awe adui" Nawaliojaribu kutulazimisha tuliondoa mabalozi wetu.
Watanzania, hawakusomeshwa na warusi tu. Mwalimu alusoma UK, ja wengi walipewa scholarship za Commonwealth, na zilikuwa zinapiganiwa sana. Wapo waliosomeshwa na US, kama akina Chenge, wapo waliosomeshwa na Cuba, wapo waliosomeshwa na Ujerumani. Wapo waliosomeshwa na Israel na Canada, hasa makamanda wa Jeshi. Wapo waliosomeshwa na USSR. Kusomesha watu wetu isiwe sababu ya kutufunga vinywa vyetu - hii ndiyo ilikuwa msingi ule wa sisi kuchagua siasa za kutofungamana na upande wowote. Msaada kama ni wenye kutifaa, hatuchagui, ja wala ule msaada siyo sababu ya kutuweka upande ule uliotupatia msaada.Mleta mada kwa vyovyote siyo muelewa wa siasa za dunia.
Afrika mzima imetulia, siyo bure ila ni kwa makusudi kabisa.
Kumbuka NATO walipoivamia Libya hakuna mtu Ulaya aliyelaani badala yake walirusha na picha ya marehemu Ghaddafi bila hata staha.
Sasa kihistoria wewe kijana tambua kwamba kipindi nchi za kiafrika zinapigania uhuru, Urusi alikuwa nasi bega kwa bega kwa kutufundishia majeshi na kutupa silaha. Nadhani unawajuwa watawala wetu walikuwa kina nani.
Urusi aliamua kutusomeshea watu wetu ambao baadae walikuja kuongoza nchi zetu. Kumbuka wakoloni hawakutaka tuwe na elimu ili tuweze kujitawala.
Marekani na NATO wamevamia nchi nyingi, wameua viongozi wengi wa mataifa mengi hususani Afrika akiwemo Lumumba, Samora Mashel, usidhani Afrika imesahau msaada wa Urusi.
Kwa sasa Urusi analinda maslahi yake, wewe unamlaani kwa lipi wakati amechokozwa?
Masikini huwezi kuwa na upande hata kidogoWatanzania, hawakusomeshwa na warusi tu. Mwalimu alusoma UK, ja wengi walipewa scholarship za Commonwealth, na zilikuwa zinapiganiwa sana. Wapo waliosomeshwa na US, kama akina Chenge, wapo waliosomeshwa na Cuba, wapo waliosomeshwa na Ujerumani. Wapo waliosomeshwa na Israel na Canada, hasa makamanda wa Jeshi. Wapo waliosomeshwa na USSR. Kusomesha watu wetu isiwe sababu ya kutufunga vinywa vyetu - hii ndiyo ilikuwa msingi ule wa sisi kuchagua siasa za kutofungamana na upande wowote. Msaada kama ni wenye kutifaa, hatuchagui, ja wala ule msaada siyo sababu ya kutuweka upande ule uliotupatia msaada.
Hakuna laana ya ulinzi wa maslahi ya nchi, kuna laana ya occupation, kupiga na kuikalia nchi kwa mabavu tena kwa kuwanyanyasa wenye nchi. Ingalikuwa hivyo Tanzania tungelaaniwa kwa kumpiga na kumuondoa Amin lakini hatukuikalia kwa mabavu, tuliqasaidia kubadili uongozi na kulinda maslahi ya mpaka wetu. Hata wakati wa hizo blocks ambazo ndio chanzo cha vita ya leo. Bado nchi zilipigana na kugawanywa ( 2 Germans. 2 Koreas) hatukuwahi kuingilia magomvi yao yote yalikuwa ya maslahi yamipaka kupinga kutoingiliwa na blocks. Unamsogezea jirani majeshi ya adui akae kimya?Na kweli hili somo, inaonekana wewe hukuelewa kabisa.
Kutofungamana na upande wowote ilimaanisha kutokuwepo katika block yoyote katika zile mbili - Magharibi (Ubepari) au Mashariki (Ujamaa). Haikumaanisha kukosa msimamo katika kukemea uovu.
Tulitoa kauli kali dhidi ya Israel, na tukatamka wazi kuwa Wapalestina wanaonewa, Israel iache mauji dhidi ya Palestine. Kule Nigeria, tulilaani vita vya Biafra, tukapeleka mpaka makamanda wetu. Kule Comoro, tulilaani mapinduzi ya Serikali ya kiraia, tukapeleka na askari wetu, wakakaa huko kwa miaka mingi.
Kutofungamana na upabde wowote haikumaanisha kukosa ujasiri dhidi ya yale tunayoyaona hayapo sawa, bali ilikuwa ni kukataa kuamliwa mambo yetu kwa msingi wa kuwa kwenye block fulani, na kinachoamriwa na block hiyo, na wewe unafungwa nacho.