Urusi-Ukraine ni jaribio la ukoloni mpya. Tanzania ipo kimya, kwanini?

Urusi-Ukraine ni jaribio la ukoloni mpya. Tanzania ipo kimya, kwanini?

Na kweli hili somo, inaonekana wewe hukuelewa kabisa.

Kutofungamana na upande wowote ilimaanisha kutokuwepo katika block yoyote katika zile mbili - Magharibi (Ubepari) au Mashariki (Ujamaa). Haikumaanisha kukosa msimamo katika kukemea uovu.

Tulitoa kauli kali dhidi ya Israel, na tukatamka wazi kuwa Wapalestina wanaonewa, Israel iache mauji dhidi ya Palestine. Kule Nigeria, tulilaani vita vya Biafra, tukapeleka mpaka makamanda wetu. Kule Comoro, tulilaani mapinduzi ya Serikali ya kiraia, tukapeleka na askari wetu, wakakaa huko kwa miaka mingi.

Kutofungamana na upabde wowote haikumaanisha kukosa ujasiri dhidi ya yale tunayoyaona hayapo sawa, bali ilikuwa ni kukataa kuamliwa mambo yetu kwa msingi wa kuwa kwenye block fulani, na kinachoamriwa na block hiyo, na wewe unafungwa nacho.
Sasa hivi ni dhahiri hizo block ulizotaja zinapigana Vita ndio mana tumeshikilia msimamo wetu "hatufungamani na yeyote kati yao".
 
IMG_3621.jpg
 
Uvamizi wa Ukraine pamoja na maelezo ya rais wa Urusi ni jaribio la kuanzisha ukoloni mpya. Nchi nyingi zinadai Urusi itoke tena katika nchi jirani na kulipia fidia.

Balozi wa Kenya alihotubia Umoja wa Mataifa akilaumu matendo ya Urusi. Tanzania ni kimya. Kwa nini?

Serikali haielewi ni nini kinachoendelea?

Serikali haijali kinachoendelea (kinyume na hotuba zote eti taifa linapinga ukoloni na kujivunia) ?

Serikali inaogopa kusema kitu kuhusu rafiki wa China?
Huyo Balozi wa Kenya keshajibiwa na Putin,' Unaweza kujaribu kuutikisa Mbuyu badala yake Matako yako ndo yakaishia kutikisika.'
 
Uvamizi wa Ukraine pamoja na maelezo ya rais wa Urusi ni jaribio la kuanzisha ukoloni mpya. Nchi nyingi zinadai Urusi itoke tena katika nchi jirani na kulipia fidia.

Balozi wa Kenya alihotubia Umoja wa Mataifa akilaumu matendo ya Urusi. Tanzania ni kimya. Kwa nini?

Serikali haielewi ni nini kinachoendelea?

Serikali haijali kinachoendelea (kinyume na hotuba zote eti taifa linapinga ukoloni na kujivunia) ?

Serikali inaogopa kusema kitu kuhusu rafiki wa China?
Putin anaweza asijue kama kuna nchi inaitwa Tanzania, bora tukae kimya tu
 
Viongozi wetu, ni wana CCM hivyo kama kawaida ya watu hawa kutokuwa na msimamo. Msimamo wao inategemea atakae wapa pesa au madaraka. Hapa wanasubiri atakae shinda, kwa sasa wanaogoa kubeti
 
Uchumi wa dunia uko interconnected na dunia ivyo huwezi shugulika na mambo yako wakati sehemu zingine za dunia haziko sawa,ni ujinga
Hata hivyo serekali ilishatoa neno tayari kuhusu raia wake warudi au waende Poland. Its more than enough, haikukaa kimya. Aliesmart ni yule anaejua priority ziko wapi, vita ya urusi na ukraine au kushughulikia mlo kwanza ? Hio vita kama itatuathiri ni almost neglible. Wakati ukikosa mlo unakufa!
 
Tanzania hawezi sema chochote kama nchi rafiki zake wanafanya maovu?
Unafiki
Pia Putin hajatoa tamko lolote kuhusu Kenya
3 miti aina ya baobab haipatikani kule ulaya, Inayopatikana no miti ifananayo wanaoiita baob

Kenya ilitoa tamko maana no muwakilishi wa UNSC sasa Tanzania mnataka mseme msimamo wenu kwa jukwaa gani?
Jamii forums ama
 
Ukiwa maskini hakuna anayekusikiliza au kujali umesema nini na unaonekana mpuuzi tuu, hata kwenye familia anayekata check ndio anasikilizwa na kuheshimiwa...NATURE!
 
Ukiwa maskini hakuna anayekusikiliza au kujali umesema nini na unaonekana mpuuzi tuu, hata kwenye familia anayekata check ndio anasikilizwa na kuheshimiwa...NATURE!
Ni kweli tamko la Tanzania lisingekuwa na uzito mkubwa sana. Hata hivyo mataifa huangalia sana nani anasimama kwa haki na nani anapendelea kunyamaza. Umoja wa Mataifa ni jukwaa ya mataifa madogo. Mataifa makubwa yanajitahidi kupata mengi upande wao.
Mataifa madogo ni haraka kuomba usaidizi na ushikamano ya makubwa yakishambuliwa au kupambana na matatizo ya pekee (njaa, kimbunga....).
Tanzania ilikuwa na sifa zamani ya kusimama dhidi ya mabaki ya ukoloni. Msimamo huu ulipatikana wakati umaskini ulikuwa kubwa zaidi.
 
Yani tuseme chochote tu kwa kuwa Kenya wamesema? Huu ujinga wa hivyo sisi hatuna.
 
Uvamizi wa Ukraine pamoja na maelezo ya rais wa Urusi ni jaribio la kuanzisha ukoloni mpya. Nchi nyingi zinadai Urusi itoke tena katika nchi jirani na kulipia fidia.

Balozi wa Kenya alihotubia Umoja wa Mataifa akilaumu matendo ya Urusi. Tanzania ni kimya. Kwa nini?

Serikali haielewi ni nini kinachoendelea?

Serikali haijali kinachoendelea (kinyume na hotuba zote eti taifa linapinga ukoloni na kujivunia) ?

Serikali inaogopa kusema kitu kuhusu rafiki wa China?
Acha ufala usituchagulie maadui sisi hatufungamani na upande wowote.
 
Hata hivyo serekali ilishatoa neno tayari kuhusu raia wake warudi au waende Poland. Its more than enough, haikukaa kimya. Aliesmart ni yule anaejua priority ziko wapi, vita ya urusi na ukraine au kushughulikia mlo kwanza ? Hio vita kama itatuathiri ni almost neglible. Wakati ukikosa mlo unakufa!
Huwezi kushughulikia huo mlo wakati sehemu unapotoa huo mlo panawaka,apply akili kidogo.
 
Sijui mashuleni siku hizi watoto wanafundishwa nini? Enzi za nyerere mtoto wa primary anajua "Sera yetu ya nje ni Sera ya kutofungamana na upande wowote" yaani Tanzania hatuchaguliwi "Nani awe rafiki na nani awe adui" Nawaliojaribu kutulazimisha tuliondoa mabalozi wetu.

kama hatufangamani na upande wowote, kwanini Nyerere alisimama Palestina? ANC? wana Msumibiji?

Hapa hapana suala la kusimama na upande, hapa pana suala la kusimama kwenye haki.
 
Hakuna ukweli kwa ulichoandika. Wazenji wamejaa huku Bara na wanaishi vizuri sana mpaka baadhi ya watanganyika wanapiga kelele humu jukwaani.

Historia ya Russia na Ukraine ni tofauti sana na ile ya Bara na Visiwani.

MKuu utaendelea kuwa mjinga mpaka lini? Hivi kunahitaji nini uoneshwe mpaka ujue kuwa Tanganyika inaitawala Zanzibar kwa mabavu
 
kama hatufangamani na upande wowote, kwanini Nyerere alisimama Palestina? ANC? wana Msumibiji?

Hapa hapana suala la kusimama na upande, hapa pana suala la kusimama kwenye haki.
Nchi zote ulizotakwa zili/zinakaliwa kwa.mabavu. Russia haijakalia nchi yoyote kimabavu inajaribu kulinda maslahi yake kwa kumuondoa kiongozi asietaka kusikiliza onyo juu ya hatua hatarishi anazojaribu kutaka kumfanyia. Nimetoa mfano wa Amini alivyoondolewa Uganda.
 
MKuu utaendelea kuwa mjinga mpaka lini? Hivi kunahitaji nini uoneshwe mpaka ujue kuwa Tanganyika inaitawala Zanzibar kwa mabavu
Huhitaji kutumia matusi ukitaka kujenga hoja yako. Ni muungano ambao ushahidi wa picha na video upo mpaka kesho.

Zipo picha za Nyerere na Karume kusaini mikataba ya muungano, zipo picha za Nyerere kuchanganya udongo na mmoja wa wakinamama waliohusika yupo mpaka leo.

Yapo matatizo yanayotatulika watu wanapokaa pamoja. Russia na Ukraine ni jeuri yao ya kutunishiana misuli, Warusi wakiamini wanayo haki ya kuimiliki Ukraine na wenyeji wakipinga sera hizo za mabavu.
 
Nchi zote ulizotakwa zili/zinakaliwa kwa.mabavu. Russia haijakalia nchi yoyote kimabavu inajaribu kulinda maslahi yake kwa kumuondoa kiongozi asietaka kusikiliza onyo juu ya hatua hatarishi anazojaribu kutaka kumfanyia. Nimetoa mfano wa Amini alivyoondolewa Uganda.
Mkuu sijui historia yako ulikuta wapi?? Urusi ilianza kama utemi wa Moscow, ikaenea hadi Bahari Pasifiki (jirani ja Japani, Kaskazini mwa China) kwa uvamizi wa maeneo ya makabila, falme, sultani na kadhalika. Pia nchi nyingi upande wa kusini (leo Turkmenistan, Kazakhstan, Uzbekistan...).
Lenin alipotawala 1919 baada ya mapinduzi ya kikomunisti, aligawa Urusi kwa maeneo ya kiutamaduni akiamini itarahisisha utawala kupitia chama cha komunisti, akaunda "jamhuri" zilizokuwa 17 chini ya Moscow wakati wa mwisho wa ukomunisti, pamoja na sehemu iliyoendelea kuitwa "Urusi".
Mwaka 1991 sehemu hizo zilitengana rasmi, na Putin analia hadi sasa eti kosa kubwa la Wakomunisti kugawa Milki ya Urusi. Sasa anajaribu kuijenga milki hiyo upya. Belarus ameshapata, Ukraine anajaribu sasa, nyingine anatishatisha . . .
 
Hivi hujafundishwa kuwa hatuna adui wala rafiki yaani kote sawa
Leo mwarabu anatupa msaada wa kuwapigia magoti
Kesho tunamuomba Myahudi atusaidie Kilimo na maisha yanaenda

Hatufungamani na upande wowote sisi kwa njaa zetu hebu tuache
 
Back
Top Bottom