Na kweli hili somo, inaonekana wewe hukuelewa kabisa.
Kutofungamana na upande wowote ilimaanisha kutokuwepo katika block yoyote katika zile mbili - Magharibi (Ubepari) au Mashariki (Ujamaa). Haikumaanisha kukosa msimamo katika kukemea uovu.
Tulitoa kauli kali dhidi ya Israel, na tukatamka wazi kuwa Wapalestina wanaonewa, Israel iache mauji dhidi ya Palestine. Kule Nigeria, tulilaani vita vya Biafra, tukapeleka mpaka makamanda wetu. Kule Comoro, tulilaani mapinduzi ya Serikali ya kiraia, tukapeleka na askari wetu, wakakaa huko kwa miaka mingi.
Kutofungamana na upabde wowote haikumaanisha kukosa ujasiri dhidi ya yale tunayoyaona hayapo sawa, bali ilikuwa ni kukataa kuamliwa mambo yetu kwa msingi wa kuwa kwenye block fulani, na kinachoamriwa na block hiyo, na wewe unafungwa nacho.