Urusi-Ukraine ni jaribio la ukoloni mpya. Tanzania ipo kimya, kwanini?

Urusi-Ukraine ni jaribio la ukoloni mpya. Tanzania ipo kimya, kwanini?

Nchi zote ulizotakwa zili/zinakaliwa kwa.mabavu. Russia haijakalia nchi yoyote kimabavu inajaribu kulinda maslahi yake kwa kumuondoa kiongozi asietaka kusikiliza onyo juu ya hatua hatarishi anazojaribu kutaka kumfanyia. Nimetoa mfano wa Amini alivyoondolewa Uganda.
Kaka usisahau historia halisi. Amin aliwahi kuvamia nchi nyingine, yaani akavamia Kagera. Ukarine haijavamia nchi yoyote.
Kinyume Ukraine kwa hiari yake ilikabidhi silaha za kinyuklia (zilizobaki huko baada ya mwisho wa Umoja wa Kisovyeti ambamo Ukraine ilikuwa jimbo la pili kwa ukubwa) kwa Urusi kwenye mwaka 1994. Mkataba wa Budapest ulitiwa sahihi na Urusi, Marekani na Uingereza pamoja na Ukraine (pia Belarus, Kazakhstan). Hapo Urusi iliahidi kutetea umoja na usalama wa Ukraine.

Nguvu ya ahadi hiyo unaona sasa!

(kama hujui habari hizi, jisomee hapo, angalia marejeo yyanayotajwa! Budapest Memorandum on Security Assurances - Wikipedia)
 
Wale ni ndugu wanapigana. It is not the business of anybody kuingilia.
It cannot lead to WW Three. Hiyo haiwezekani. The world will not permit. Ati ndugu wapigane and drag us all into war?
 
Mleta mada ya tz yamekushinda unaleta mdomo kwa yasiyokuhusu kabisa. Huo ndiyo tunaita uswahili Tabia mbaya sana hii.
 
Mkuu sijui historia yako ulikuta wapi?? Urusi ilianza kama utemi wa Moscow, ikaenea hadi Bahari Pasifiki (jirani ja Japani, Kaskazini mwa China) kwa uvamizi wa maeneo ya makabila, falme, sultani na kadhalika. Pia nchi nyingi upande wa kusini (leo Turkmenistan, Kazakhstan, Uzbekistan...).
Lenin alipotawala 1919 baada ya mapinduzi ya kikomunisti, aligawa Urusi kwa maeneo ya kiutamaduni akiamini itarahisisha utawala kupitia chama cha komunisti, akaunda "jamhuri" zilizokuwa 17 chini ya Moscow wakati wa mwisho wa ukomunisti, pamoja na sehemu iliyoendelea kuitwa "Urusi".
Mwaka 1991 sehemu hizo zilitengana rasmi, na Putin analia hadi sasa eti kosa kubwa la Wakomunisti kugawa Milki ya Urusi. Sasa anajaribu kuijenga milki hiyo upya. Belarus ameshapata, Ukraine anajaribu sasa, nyingine anatishatisha . . .
Upande mwingine wa shilingi ni huu.
 
Upande mwingine wa shilingi ni huu.

Kaka nauliza tena: Historia yako unapata wapi? Huyu mama ana huruma mwingi kwa Urusi anataja mifano ambako Urusi ilishambuliwa.
Sema wewe (maana ulimteua na kuleta): katika mfano gani Urusi ilishambuliwa tu? Si zaidi ilijikuta katika vita iliyowahi kushiriki yenyewe? (Hadi Vita Kuu ya Pili ambako iliwahi kupatana na Ujerumani na kuvamia Poland Mashariki pamoja na Latvia, Estonia, Lithuania - ili kujiuta Wajerumani walishambulia ghafla Urusi?)
Pamoja na hayo: Je NATO iliwahi kuvamia nchi gani katika historia yake? Kinyume Urusi iliamua kushambulia Hungaria mwaka 1956 na Chekoslovakia 1968 (ambayo mama mrembo wa video yako hajui? au hataji?)
Halafu je kuna nchi yoyote iliyolazimishwa kujiunga na NATO? Nchi zote zilizojiunga nayo zilifanya vile kwa hiari.
Ukraine imeomba kupokelewa tangu miaka 20, hadi sasa NATO hawakukubali.

Sasa kaka, je utakuwa na majibu? Au utaleta tena youtube?
 
Pamoja na wa ukraine kupiga jeki sekta ya utalii Zanzibar kipindi cha covid ,inasikitisha Mtanzania kushangilia nchi ya Ukraine kuvamiwa . Hadi leo baadhi ya wapo Zanzibar wanasubiri taratibu za usafiri.
 
Huu ndio ushenzi wa nchi za kidikteta. Polisi Moscow wanasimisha rai njiani na kusoma message za simu.
 
lakin hat mrus ni mteja wet mkubwa inabid kuwafanyia wote dua. leta bukhuri shari tupige uban

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Sasa Tanzania ina ushawishi gani duniani? Africa mashariki tu bado tunastruggle.Sisi ombaomba kwahiyo lazima tuwe neutral tu
Tanzania ya sasa inadharaulika sana.
Ile ya Mwalimu hivi sasa UN, NATO, Warusi, Ukraine wangekuwa wanapisha kutafuta busara yake.
 
Huu ndio ushenzi wa nchi za kidikteta. Polisi Moscow wanasimisha rai njiani na kusoma message za simu.

Tanzania ina msimamo wake. Lakini kwa kweli anachokifanya Urusi kwa Ukraine si sawa. Masharti anayompa ni sawa na udhalilishaji.
Urusi akiachwa aendelee atakuja kuota mapembe na ipo siku atataka kuvamia na kumiliki pakubwa zaidi.

NB: Nimejifunza masharti anayotoa Urusi kwa Ukraine ni sawa na ya Tanganyika kwa Unguja na Pemba.
 
Tanzania ya sasa inadharaulika sana.
Ile ya Mwalimu hivi sasa UN, NATO, Warusi, Ukraine wangekuwa wanapisha kutafuta busara yake.
Nimeshangaa ushauri wa waziri wetu eti wanafunzi wakitanzania waliopo Ukraine wabebe bendera ya Tanzania na kuelekea Urusi border. Hivi huyu waziri anawatakia mema vijana wetu? Watanzania Ukraine wapo salama chini ya bendera ya Kenya ambao walilaani uvamizi,kuliko bendera ya Tanzania ambayo inaegemea Urusi zaidi. Huo ndio ukweli.
 
Na kweli hili somo, inaonekana wewe hukuelewa kabisa.

Kutofungamana na upande wowote ilimaanisha kutokuwepo katika block yoyote katika zile mbili - Magharibi (Ubepari) au Mashariki (Ujamaa). Haikumaanisha kukosa msimamo katika kukemea uovu.

Tulitoa kauli kali dhidi ya Israel, na tukatamka wazi kuwa Wapalestina wanaonewa, Israel iache mauji dhidi ya Palestine. Kule Nigeria, tulilaani vita vya Biafra, tukapeleka mpaka makamanda wetu. Kule Comoro, tulilaani mapinduzi ya Serikali ya kiraia, tukapeleka na askari wetu, wakakaa huko kwa miaka mingi.

Kutofungamana na upabde wowote haikumaanisha kukosa ujasiri dhidi ya yale tunayoyaona hayapo sawa, bali ilikuwa ni kukataa kuamliwa mambo yetu kwa msingi wa kuwa kwenye block fulani, na kinachoamriwa na block hiyo, na wewe unafungwa nacho.
Case closed:
 
Case closed.

Siku moja baada ya Ujumbe wa mabalozi wa nchi za Ulaya nchini Tanzania kuitaka Tanzania na nchi nyingine za Afrika kupaza sauti kukemea uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, nchi hiyo imetoa msimamo wake leo na kusema yenyewe haifungamani na upande wowote.

Msimamo huo unapigiwa mstari na uamuzi wa taifa hilo la Afrika Mashari la kutokupigia kura azimio la baraza Kuu la Umoja huo, UNGA kupitisha lililopitishwa mapema mwezi huu, kuitaka Urusi kusimamisha mara moja mashambulizi yake dhidi ya Ukraine na kuyaondoa majeshi yake katika nchi hiyo.

Waziri wa Masuala ya kigeni wa nchi hiyo, Liberata Mulamula amesema kwa miaka mingi sasa Tanzania inaamini katika kutafuta muafaka na marudhiano kwa kutumia njia ya diplomasia ili kumaliza migogoro.

Kutokana na muafaka na maridhiano kutopatikana katika mzozo wa Urusi na Ukraine, Waziri Mulamula anasema: “ndio maana katika kupiga tukaamua kutofungamana na upande wowote, lakini ilikuwa sio kutofungamana na pande zote mbili lakini ni kutoa ujumbekuonyesha kwamba sisi msimamo wetu na sera yetu na msingi wetu wa sera ya mambo ya nje ni kutokufungamana na pande zozote hasa katika hali kama hii”, alisema Mulamula.

Back
Top Bottom