Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Urusi imesema leo kuwa itajibu kwa njia sawa kama Ujerumani itaumaliza mzozo kuhusu vyombo vyao vya habari, lakini itauongeza mvutano huo hata zaidi kama Berlin itaamua kufanya hivyo.
Urusi ilisema jana kuwa inazifunga shughuli za shirika la habari la Ujerumani - DW mjini Moscow na kuwapokonya wafanyakazi wake vibali vya kazi katika hatua ya kulipiza kisasi baada ya Berlin kuyafungia matangazo ya televisheni ya Russia Today nchini Ujerumani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Urusi Maria Zakharova amesema mpira sasa upo katika upande wa Ujerumani.
Mkurugenzi Mkuu wa DW Peter Limbourg ameapa kuwa shirika hilo la utangazaji la umma litaendelea kuripoti kuhusu matukio ya Urusi bila kuzuiwa. Umoja wa Ulaya umelaani uamuzi huo wa Urusi huku msemaji wake wa masuala ya kigeni Peter Stano akisema haukubaliki na hauna uhalali wowote.