The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 838
Ursula Von der Leyen, kidomo domo sana na war monger, si ajabu hata habari hizi kaweka chumvi mno, anacho tafuta yeye ni kitengeneza mazingira ya kumshawishi Trump ajiingize kichwa kichwa kwenye vita nchini Ukraine, kanajifanyaga kinara wa kumpa ushauri potofu Zelensky kwamba hasikubari ushauri anao pewa na Trump.Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ameeleza hasira yake kufuatia shambulio kubwa zaidi la Uru fer der Lyern si mjini Kyiv tangu Julai, ambapo watu 23 akiwemo watoto wanne waliuawa na ofisi ya ujumbe wa EU pamoja na majengo jirani kuharibiwa.
Maafisa wa Ukraine wamesema makombora ya Urusi yaliharibu jengo la ghorofa tano katika wilaya ya Darnytskyi, na wengi wa waliokufa walikuwa humo.
Wengine kadhaa walijeruhiwa, wakiwemo watoto. Von der Leyen alisema makombora mawili yalipiga karibu na ujumbe wa EU umbali wa mita 50 pekee ndani ya sekunde 20, jambo alilolaani vikali.
Ofisi ya Baraza la Uingereza pia iliharibiwa. Jeshi la Ukraine liliripoti kuwa Urusi ilitumia karibu ndege zisizo na rubani 600 na zaidi ya makombora 30 ya masafa marefu katika shambulio hilo, likiwa kubwa zaidi mwezi huu.
Shambulio hilo lilitokea majira ya saa 9 alfajiri, likisababisha jengo la makazi kuporomoka. Vikosi vya uokoaji vilionekana wakiondoa kifusi na kutafuta manusura. Maafisa wamesema watoto waliouawa walikuwa na umri wa miaka 2, 14 na 17.
Source BBC
Binafsi naona shambulio hilo lililenga kuwa onyo kwa mataifa ya Ulaya yanayo jifanya kutaka kupeleka eti vikosi vya kijeshi nchini Ukraine kwa kisingizio cha kulinda AMANI eti baada ya vita kumalizika wao waende huko kwa kisingizio eti cha "kulinda AMANI" Urusi imewaonya mara nyingi tu kwamba haitavumilia vikosi vya mataifa ya NATO kuja nchini Ukraine kwa kisingizio chochote kile, wakijilazimisha kwenda watachukuliwa na Urusi kwamba wamehamua kutangaza vita dhidi ya Urusi na Urusi itachukuwa hatua stahiki ya kulinda taifa lao.Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ameeleza hasira yake kufuatia shambulio kubwa zaidi la Urusi mjini Kyiv tangu Julai, ambapo watu 23 akiwemo watoto wanne waliuawa na ofisi ya ujumbe wa EU pamoja na majengo jirani kuharibiwa.