Urusi yazipa onyo Finland na Sweden mpango wao wa kujiunga na NATO

Urusi yazipa onyo Finland na Sweden mpango wao wa kujiunga na NATO

Halafu wakijiunga NATO watafanya nini? Kwani hao nchi 30 ambazo tayari zimejiunga NATO zimefanya nini mpaka sasa kwa urusi?
Sasa Russia anapata hofu gani kwa Ukraine kujiunga NATO? Huu mtazamo wa kuidharau NATO unao wewe tu hapaJF,wenzio pale Kremlin wanaitazama NATO kwa jicho tofauti kabisa,vinginevyo wasingeingia vitani kuizuia Ukraine isijiunge
 
Sweden , Finland , Ukraine zote zitajiunga NATO ni suala la mda tu.
Na Mrusi nimeshamuona hatafanya kitu atabaki analia lia tu wameshamuona ni dhaifu sana...Pale Ukraine alitakiwa aonyeshe nguvu yake kwa kupiga na kusambaratisha kila kitu ndani ya week 2 halafu aseme nani anabisha sasa aje!!!!...Sasa kalegea kama mlenda anarudi nyuma hovyo kabisa....yaani Putin umetutia aibu sana kabisa....

NILIVYOKUA Namkubali Putin na kile amefanya Ukraine ni udhaifu mkubwa sana....Kwa udhaifu huu aliouonyesha Ukraine NATO wamemsoma ipo siku watajipigia....
 
Ameanza kulewa sifa Mzee wetu Putin.

Atulie aendeleze kipigo pale Ukraine paishe.

Asijikute Mwanaume sana kuvimba vimba watamtia Kidole huko mbeleni kama hatumii akili yake vizuri.

Wahuni walikuwa wengi tu kama yeye huko nyuma.Ni muda tu uliwasubiri.

Aile Ukraine tujisifie kwa hapo.

Likivuma sana hupasuka.
Umesema kitu cha maana sana Mkuu,wakati ya Ukraine bado yanamtoa jasho anataka kurukia kwingine,huo uwezo wa kupigana kote kwa wakati mmoja hana
 
Na Marekani nchi ambayo haipo ulaya ndio inachagiza hizo nchi zijiunge.halafu baadae ziingie vitani na Urusi Kisha zibaki magofu Huku Marekani ikifurahi kwamba Sasa Urusi itadhoofika.
Aisee sikujua kumbe wazungu ni wajinga pia.
Hapa sioni nchi hata moja ya ulaya ikizichagiza nchi hizi.
Mrusi wa Songambele Inyonga Katavi unaijua Marekani kuliko wanavyoijua Ulaya
 
Wasicho kijua.. Au wanacho kijua ni viburi vyao tu na tamaa za wachache ni kuwa nchi zao zitageuzwa uwanja wa vita endapo lolote likitokea baina ya NATO na urusi. Huku mmarekani yeye kazi yake itakuwa kusafirisha silaha tu hadi uwanja wa vita
 
Nani anakaa upande wa masikini, watu wanataka kuwa karibu na matajiri, na Russia kama anataka watu wawe upande wake basi atajirike kwanza, aige mfano wa US na China.
 
Back
Top Bottom