Kateni misaada na mikopo vinginevyo mambo haya kamwe hayatakoma.
Sijui kwanini nchi wahisani wanashindwa kuweka shariti la kutoa misaada na mikopo kuwa ni lazima nchi husika iwe na Tume Huru ya Uchaguzi inayokubalika na makundi yote.
Ningekuwa na ushawishi, ningeanzisha movement ya kuzitaka nchi tajiri na mashirika ya fedha ya kimataifa kuweka shariti kwamba, kila nchi inayotaka msaada au mkopo, ni shariti nchi hiyo iwe na Tume Huru ya Uchaguzi inayokubalika na wadau wote wa uchaguzi katika nchi hiyo.
Au kama hili gumu,basi movement yangu nyingine ingekuwa ni kuzishawishi nchi hizi kuweka shariti linaloweza kuwa kama incentive ambapo nchi yenye kuonyesha demokrasia ya kweli, kwa kuwa na Tume Huru na Katiba inayokubalika na makundi yote katika nchi, inakuwa ni moja ya kigezo kwa nchi husika kupunguziwa au kufutiwa madeni.
Jitihada za nchi wahisani na mashirika ya fedha ya kimataifa za kuondoa umasikini katika mataifa yanayoendelea, hasa Afrika, haziwezi kufanikiwa iwapo katika nchi hizi hakuna demokrasia ya kweli, hivyo kuna ulazima wa kulazimisha nchi hizi kuwa na demokrasia vinginevyo maendeleo yatachukuwa muda mrefu kufikiwa katika nchi hizi.
Demokrasia ya kweli inafanya watawala wawajibike kwa watu wao na nchi zao na hivyo kuwezesha maendeleo kupatikana kwa haraka zaidi.