US honours Kilango


....."Hatua ya Rais Kikwete kumpongeza Kilango ni pigo kubwa kwa kundi la wana CCM wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya ufisadi na imekuja wakati chama hicho kimegawanyika katika makundi mawili, lile linalotuhumiwa kwa ufisadi na lile la wanaoongoza mapambano dhidi yao, akiwamo mbunge huyo wa Same Mashariki.

Rais Kikwete aliielezea tuzo hiyo kama ni tunda linalotokana na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 kuhusu vita dhidi ya rushwa......."


*******************

Ina maana anakubaliana na yote AK aliyokuwa akiyasema Bungeni? Kama vile, kwa mfano, fedha za EPA "zinazorejeshwa" lazima zionekane halisi (physically) na ikiwezekana ndani ya viroba ili wote wazione?

Sasa JK mbona hajawahakikishia wananchi hilo limetendeka -- yaani nani karejesha ngapi na lini? Au anampaka mafuta mama wa watu?

Ilipasa JK mwenyewe ndiyo angekuwa shujaa katika vita ya ufisadi kwa kunasa tuzo kama hiyo (iwapo Wamarekani wanayo kwa ajili ya wanaume pia), na siyo kungojea mtu mwingine apate ndiyo ampongeze! Anampongeza nini kwa mambo ambayo JK mwenyewe angeweza kuyasemea na kuwa na uwezo wa kuyatimiza?
 
JK ni hypocrite tu

Aka msanii/nyoka/popo/kinyonga/mnafiki/etc. Hawezi kutambua mchango wa Anna Kilango wakati bado kuna mafisadi wanadunda mtaani na hakuna jitihada za maksudi kuwashughurikia. Hawezi kudanganya umma kuwa ni ilani ya CCM ya 2005 kupambana na rushwa/mafisadi ikizingatiwa JF ndio waanzilishi na wafichuaji wa ufisadi wakifuatiwa na opposition parties kurusha live bungeni. Kama rais appreciation yake kwa Kilango/watanzania kwa ujumla ilikuwa ni kuonyesha jitihada za makusudi kuwashughurikia mafisadi sio mpaka alaazimishwe sana halafu bado anatupiga changa la macho
 

Ni mwepesi mno kutoa pongezi lakini yeye mwenyewe juhudi zake katika mapambano dhidi ya mafisadi hazionekani kabisa. JK why are missing in action!? 😕
 
Jamani labda mimi ni kipofu, naomba mtu yeyote aorodheshe mambo angalau matano ya ushujaa aliyofanya huyu tunayeambiwa ni shujaa.

Kama kupiga kelele za kiusanii kujijengea jina ni ushujaa, basi tumekwisha.
 
Jamani labda mimi ni kipofu, naomba mtu yeyote aorodheshe mambo angalau matano ya ushujaa aliyofanya huyu tunayeambiwa ni shujaa.

Kama kupiga kelele za kiusanii kujijengea jina ni ushujaa, basi tumekwisha.

Wewe si kipofu. Kama ungekuwa kipofu usingeona hii posti. Jukwaa la mbunge ni bungeni.
 
Wewe si kipofu. Kama ungekuwa kipofu usingeona hii posti. Jukwaa la mbunge ni bungeni.

- This is what we call kumkoma nyani giladi, bila ya kumuangalia usoni!

- Labda Mkulu naye aonyeshe aliyokwisha yafanya kwa taifa, zaidi tu ya matusi kila kukicha hapa JF!

FMES!
 
anna kilango nyange malecela alifukuzwa kazi kwa kosa la kuiba fedha za mwajiri wake--gulf air. anapiga kelele ili apewe madaraka apate nafasi ya kuiba. same mashariki tumeingia hasara kumchagua kuwa mbunge.
 
anna kilango nyange malecela alifukuzwa kazi kwa kosa la kuiba fedha za mwajiri wake--gulf air. anapiga kelele ili apewe madaraka apate nafasi ya kuiba. same mashariki tumeingia hasara kumchagua kuwa mbunge.

Naomba uanzishe thread nyingine katika celebrities forum na uje na evidence siyo kuweka vitu loosely, maana kama ni kuchafuana kuna ze utamu website wanapofanya kazi hii, lakini JF tunataka analysis.
Gulf Air imefungwa na haipo tena so it is easy kuitaja, pia kugeneralize kwamba anaiba haieleweki kwani hujasema aliiba nini na kitu gani. Acha personal attacks on people.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…